Lazaro Nyalandu alijaribu kubinafisisha Mbuga ya Wanyama ya Katavi kwa Wamarekani

Binafsi sioni kama tatizo ni Nyalandu au mtanzania yeyote yule, shida hapa iko kwenye katiba yaani sheria mama haibainishi nini cha kufanya na nani, chukulia mfano tu rais akiingia madarakani ana unda baraza la mawaziri ni sawakuwa ni moja ya jukumu lake lkn kuna sheria inayo mtaka baraza liwe kubwa kiasi gani? au kunasheria inayo bainisha idadi ya mawaziri?
Sasa kama kila mtu akifanya vitu kwa utashi wake itakuja kutokea waziri wa aridhi akauza aridhi ya nchi yote. Kwani mikataba anaandaa waziri sijui na akina nani huko yaani vuruvuruuuu tu
Katiba ni Muongozo tu. Kuna nchi tena kubwa sana duniani hazina katiba bali zina sheria lakini zinafanya vizuri katika maendeleo , cha msingi ni uzalendo tu na kujituma kimisha.
 
Nyie endeleeni kufukua ila mjue mtaishia kwa mkwere, mnafikiri nyalandu hajui figusi za alikotota kajiandaa.
 
Aliyekuwa Waziri wa Utalii Mheshimiwa Lazaro Nyalandu katika kipindi cha serikali ya awamu ya nne alijaribu Kubinafisisha mbunga ya wanyama ya Katavi kwa wamarekani.

Mwanzoni mwaka 2016 aliwaalika wajumbe wa senete ya Marekani kuja kuonana na Rais Magufuli ili kukamilisha mpango huo lakini Rais Magufuli alikataa kuonana na ujumbe huo.

Namuunga mkono Waziri wa Maliasili Hamisi Kigwangwala kwa kutaka mikataba yote iliyofanywa na Nyalandu ichunguzwe na ukweli ubainike.

Chadema isitumike kama Safe Haven ya kulinda watu ambao serikali ya awamu ya tano inataka kuwachunguza.
Ndugu wewe ni muhifadhi? Kama sio acha KBS kuleta hoja usizozijua. Ingawa la Nyalandu silijui ila nataka kutoa hoja hapa. Private -Public-Partnership ni modal ambayo inayotrend kwa sasa. Ni modal inayotakiwa kuweka chachu ktk ukuaji wa uchumi na kuborsha huduma kwa jamii. Hatujawahi kuwa wakwanza kufanya Haya na tuna good lessons duniani huko. Read read! Changamoto tuliyonayo ni usimamizi na aina ya mikataba. Ila it is a good thing tuwe makini ktk utekelzaji. Zipo huduma ambazo ni state controlled na lazima iwe hivyo. Its about choices!
 
Bowie
Kwa nini unaandika leo? Siasa zenu chafu hizo ni hatari kwa taifa.
 
Mkuu kwani ubinafsishaji nchi hii ilipigwa marufuku lini? Waziri kuwaleta wawekezaji lini imekuwa haramu? Shida yako hasa kwenye uzi huu ni ipi, nyalandu kubinafsisha katavi, kuleta wawekezaji, kutaka kubinafsisha , kumuona JPM ili abinafsishe au ? Halafu nawewe inawezekana una walau degree moja.
Aitoe wapi?!...labda lumumba
 
Aliyekuwa Waziri wa Utalii Mheshimiwa Lazaro Nyalandu katika kipindi cha serikali ya awamu ya nne alijaribu Kubinafisisha mbunga ya wanyama ya Katavi kwa wamarekani.

Mwanzoni mwaka 2016 aliwaalika wajumbe wa senete ya Marekani kuja kuonana na Rais Magufuli ili kukamilisha mpango huo lakini Rais Magufuli alikataa kuonana na ujumbe huo.

Namuunga mkono Waziri wa Maliasili Hamisi Kigwangwala kwa kutaka mikataba yote iliyofanywa na Nyalandu ichunguzwe na ukweli ubainike.

Chadema isitumike kama Safe Haven ya kulinda watu ambao serikali ya awamu ya tano inataka kuwachunguza.
Kweli Mkuu?umekaa chini na kufanya home work yako katika hili na ukafikia mwafaka huu wa kutoa huu uzi ndani ya JF? sio mbaya pia kuwa msomaji wa wenzio hadi hapo utakapo kuwa na uwezo wa kutoa hoja makini,always FACTS ni muhimu;kutokuwa na chama au kutoka kwenye chama ni haki yako ila public elewa unakuhukumu kwa matendo,tabia ,msimamo wako,kama unakerwa na rushwa za aina hii basi mkuu anzia Loliondo,uuzaji wa nyumba za serikali kwa bei ya chee bila ya kufuata utaratibu wa kisheria,kesi yetu ya samaki ambayo tumeshindwa mahakamani(tunalipa fidia),mikataba ya madini iliyoitia nchi kwenye madeni makubwa,tuna miaka zaidi ya 50 ya uhuru lakini hakuna maji safi kwa zaidi ya nusu ya watanzania etc etc;kuvurugwa kwa mfumo wetu wa elimu na matokeo ndio haya tunayoyaona sasa
 
Binafsi sioni kama tatizo ni Nyalandu au mtanzania yeyote yule, shida hapa iko kwenye katiba yaani sheria mama haibainishi nini cha kufanya na nani, chukulia mfano tu rais akiingia madarakani ana unda baraza la mawaziri ni sawakuwa ni moja ya jukumu lake lkn kuna sheria inayo mtaka baraza liwe kubwa kiasi gani? au kunasheria inayo bainisha idadi ya mawaziri?
Sasa kama kila mtu akifanya vitu kwa utashi wake itakuja kutokea waziri wa aridhi akauza aridhi ya nchi yote. Kwani mikataba anaandaa waziri sijui na akina nani huko yaani vuruvuruuuu tu
Mkuu naomba kujuzwa jambo.
Hivi marekani kuna sheria au katiba yao inakifungu kinachosema idadi fulani kimili ya mawaziri anaotakiwa kuteuliwa na raisi wao?
Kama ni hivyo mbona waziri/sekritari wa mashauri ya mambo ya afrika hajateuliwa na Trump kwa muda mrefu sana?

Hawa wamerekani si ndio baba wa denokrasia na inasadikika wana katiba bora sana kuliko yetu? Na sisi tunapaswa kuiga katiba yao.
 
unadhani hii Nchi tunaweza endelea bila Investment..ebu acheni ujuha nyie..mmekalia vicheap facts..kwan kubinafsishiaha kuna ubaya gani kuna maslahi ya taifa...akili zenu za kiduni na kijamaaa
Hifadhi ya katavi ni ya tatu kwa ukubwa nchini ni kama wilaya ukisema hifadhi ibinafsishwe ni kusema sehemu ya nchi iuzwe
 
Aliyekuwa Waziri wa Utalii Mheshimiwa Lazaro Nyalandu katika kipindi cha serikali ya awamu ya nne alijaribu Kubinafisisha mbunga ya wanyama ya Katavi kwa wamarekani.

Mwanzoni mwaka 2016 aliwaalika wajumbe wa senete ya Marekani kuja kuonana na Rais Magufuli ili kukamilisha mpango huo lakini Rais Magufuli alikataa kuonana na ujumbe huo.

Namuunga mkono Waziri wa Maliasili Hamisi Kigwangwala kwa kutaka mikataba yote iliyofanywa na Nyalandu ichunguzwe na ukweli ubainike.

Chadema isitumike kama Safe Haven ya kulinda watu ambao serikali ya awamu ya tano inataka kuwachunguza.
ulikuwa wapi kuyasema haya?
 
Kweli Mkuu?umekaa chini na kufanya home work yako katika hili na ukafikia mwafaka huu wa kutoa huu uzi ndani ya JF? sio mbaya pia kuwa msomaji wa wenzio hadi hapo utakapo kuwa na uwezo wa kutoa hoja makini,always FACTS ni muhimu;kutokuwa na chama au kutoka kwenye chama ni haki yako ila public elewa unakuhukumu kwa matendo,tabia ,msimamo wako,kama unakerwa na rushwa za aina hii basi mkuu anzia Loliondo,uuzaji wa nyumba za serikali kwa bei ya chee bila ya kufuata utaratibu wa kisheria,kesi yetu ya samaki ambayo tumeshindwa mahakamani(tunalipa fidia),mikataba ya madini iliyoitia nchi kwenye madeni makubwa,tuna miaka zaidi ya 50 ya uhuru lakini hakuna maji safi kwa zaidi ya nusu ya watanzania etc etc;kuvurugwa kwa mfumo wetu wa elimu na matokeo ndio haya tunayoyaona sasa
Hakuna Dhambi inahalalisha dhambi nyingine mkuu.
 
Hifadhi ya katavi ni ya tatu kwa ukubwa nchini ni kama wilaya ukisema hifadhi ibinafsishwe ni kusema sehemu ya nchi iuzwe
Unachokisema mkuu kinanitatiza..
Ubinafsishaji = Kuuza?
Kama ndio.. Tumebinafsisha Migodi... Sehemu za Bandari, Viwanda, Mabenki, Gesi nk.. Kwa mantiki hiyo je tumeviuza?! Tusiweke panic kwa watu wanaokuja kusikia na kujifunza humu jf.. Sera ya ubinafsishaji imeletwa na Rais Mkapa.. Na alikiri ilikuwa ilikuwa na changamoto na imetugharimu ila hakukataa kwamba sio mfumo sahihi..

UAE inamiliki kwa asilimia kubwa Bandari za Newyork, Newark, Baltmore & Philadelphia marekani, Mozambique kwa sababu za kukosa usimamizi madhubuti..kukosa fedha wamebinafsisha mbuga ya zaidi ya ekari 900,000 ..yenye tabia kama ya sadani.. Na kutoka katika mipango itaongeza mapato..ajira na kupunguza ujangili huku ikitunza wanyama kwa vizazi vijavyo...

Tusichafue majina ya watu kwa hearsay.. Huwezi kumuadhibu mkeo kisa katumiwa SMS ya mapenzi.. What if mtu aliyemtumia kaiba namba na kaituma bila ridhaa ya mkeo.. Kama Mh. Nyalandu aliomba waonane na rais ni swala la kumsifu hakutaka kufanya maamuzi makubwa sana bila ushauri wa Mkuu wake wa kazi.
 
Mkuu tofautisha uwekezaji kwenye sehemu ulizotaja na mbunga ya wanyama ya Katavi. Kubinafisisha ni sawa sawa kuruhusu uwindaji haramu kufanyika kama wanavyofanya waarabu wa Loliondo ambao pia mktaba wao umesitishwa
Huwezi ukahama chama halafu ukailaamu kwa mabaya yake wakati wewe ni mmoja uliohusika na matatizo hayo. Hapa hatuchafuani jina ila tunataka ku discuss mambo kwa uwazi
 
Uongo mwingine hatari sana. Waziri anabinafsishaje ardhi iliyo chini ya dhamana ya Rais?
Kwanini aliwapeleka wale wamarekani Ikulu Mheshimiwa Rais Magufuli akakataa kuonana nao. Tafuata maana Lobbiest utajua Nyalandu alikuwa anataka kufanya nini
 
Back
Top Bottom