Lazaro ajitetea: Asema "Mimi ni Mtanzania"; abeza makundi ya wagombea Urais 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lazaro ajitetea: Asema "Mimi ni Mtanzania"; abeza makundi ya wagombea Urais 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Jan 15, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ....Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini DSM,huyu jamaa amesema kuwa hana lengo la kugombea uraisi na yeye ni mtanzania na anashangaa wanaompakazia sio raia wa Tanzania.

  Amesema kwa wanaomfahamu kazaliwa Tanzania na Baba yake na baba yake wapo hai mpaka sasa. Amesema kuwa kuna watu wanataka kumchafua kuwa sio raia kwasababu ya njama zao za kugombea uraisi.

  Ameomba makundi yafutwe na kuondoa uadui wakati huu wa kugombea hizo nafasi. Na amesema isije ikafikia kiwango mtu unashindwa kunywa chai na mtu mwingine kwasababu ni kundi tofauti...


  My take;
  Huyu jamaa anajikosha inaonekana kweli ana haya mawazo.Kuhusu urai wale wanaomfahamu wanaweza kusema.Kwa kweli mwaka huu tutapata mengi.

  Source: Channel ten news bulletin

  UPDATE:

  NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu amewataja vigogo watatu ambao amekuwa akihusishwa nao kwamba anawaunga mkono katika harakati za mbio za urais wa 2015. Vigogo hao ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe.

  Nyalandu alitaja majina hayo katika mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akizungumzia hali ya kisiasa nchini na athari za siasa za makundi katika vyama vya siasa, huku akisema kuwa hali hiyo inaathiri utendaji kazi katika taasisi za umma.

  Alisema imefika wakati inakuwa vigumu kuwa na uhusiano hata wa kirafiki na mtu kwani kila unapoonekana ukisalimiana na wale wanaotajwa kuwa katika mbio hizo basi unawekwa alama kuwa mtu mwenye nia hiyo au kuwa katika moja ya makundi.

  "Makundi haya yanadaiwa kuwa na wafuasi, endapo haupo kwenye kundi fulani, basi unadhaniwa kuwa adui mkubwa wa kundi hilo, wakitumia dhana isemayo, kama hauko nasi wewe uko kinyume nasi," alisema Nyalandu na kuongeza:"Taifa limejaa malalamiko, hisia za kupigana vijembe, kutafutana ubaya na kuoneana kisiasa."

  Alisema wanasiasa vijana wanapoonekana kujitolewa kufanya kazi kwa moyo na kujitoa zaidi ya wito wa kazi wanawekwa katika darubini na kupaswa kusema wako katika kundi gani.

  Naibu Waziri huyo alisema kuendelea kushamiri kwa siasa za aina hiyo kunaliweka taifa katika hatari kutokana na kuzorotesha shughuli za maendeleo za kila siku.

  "Wanapokataa kurubuniwa, wanawekwa kwenye kundi lililo kinyume na kundi husika na kuanza kushambuliwa, kwa kifupi, nchi yetu ni kama nyumba moja na imesemwa zamani, nyumba iliyotengana haiwezi kusimama," alisema.

  Alisema hali hiyo inaliweka taifa katika wakati mgumu na hasa kipindi hiki ambacho inakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi, kijamii na kukuza demokrasia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa.

  "Tunaowajibu wa kuhakikisha uwajibikaji unaongezeka nchini na kila mtu anatimiza wajibu wake kwa kufanya kazi kwa bidii ili taifa liweze kuhimili ushindani utakaotokana na ushirikiano wa Afrika Mashariki, zikiwemo fursa na changamoto zake," alisema Nyalandu.
  Alisema hana nia ya kugombea urais wala kujihusisha na kundi lolote akisema hali ya kuwapo kwa makundi ni hatari kwa taifa na inapunguza kasi ya uwajibikaji kwa baadhi ya viongozi wenye nia ya kufanya hivyo.

  "Hali ya kisiasa iliyopo sasa na hasa kwa baadhi ya viongozi kujikita katika kutafuta urais wa 2015, huku wafuasi wao wakiendeleza mapambano dhidi ya wale wasiokubali kuwa ndani ya makundi husika inasikitisha na ina lengo la kukatisha tamaa viongozi wenye nia ya kufanya kazi walizopewa kwa bidii," alisema. Nyalandu alisema kwa sasa Rais Jakaya Kikwete bado anatumikia miaka minne katika nafasi ya Urais na kusisitiza hakuna sababu ya kundi lolote wala mtu kufikiria urais wa 2015.

  Lowassa, Membe na Sitta
  Nyalandu ambaye ni Mbunge wa Singida Kaskazini, alilalamika kwamba amekuwa mwathirika wa siasa hizo kwani amekuwa akihusishwa na makundi mbalimbali ya wanaotajwa kuutaka urais mwaka 2015 na kwamba hali hiyo kutokana na uhusiano alionao na wanaotajwa.

  "Wapo walioniona Monduli na kudai kuwa eti ninaelekea kuwa katika kundi la Lowassa. Mimi sina uhusiano na kundi lolote hata kama makundi hayo yapo," alisema Nyalandu.

  Alisema yeye amekuwa na uhusiano wa muda mrefu na Lowassa kutokana na kufanya naye kazi alipokuwa Waziri Mkuu hasa kufanikisha ujenzi wa shule za sekondari katika Jimbo la Singida Kaskazini.

  Kuhusu Membe alisema ni rafiki yake wa muda mrefu. "Membe ni rafiki yangu wa muda mrefu, nimezoeana naye tangu siku nyingi na pia nimefanya naye kazi hata nikifika nyumbani kwake naweza kuingia bila hodi na kula hata chakula bila tatizo lolote," alisema Nyalandu.

  Alitaja pia uhusiano wake na Sitta akisema kiongozi huyo ni kama mshauri wake na mwalimu anayemsaidia katika mambo mengi.Alisema watu kutoka katika makundi tofauti wanapomwona na watu hao wamekuwa wakifikiri kwamba na yeye ni sehemu ya kundi husika jambo ambalo alilipinga.


  Source: Mwananchi
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jan 15, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Amesema wapi?
   
 3. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Viumbe wazito kweli binadamu wengine, aseme lipi liwe sahihi na kweli? Mna haraka gani kwani kura mnalazimishwa kumpigia hata angegombea? Em tushughulikie masuala muhimu kama Katiba mpya, ubadhirifu wa mali za umma na mengineyo yenye manufaa, si kila kukicha fulani anautaka urais.
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Ukizaliwa Tanzania kwa wazazi Watanzania haina maana kuwa huwezi kuchukua uraia wa nchi nyingine, weak defence.

  Mie nilifikiri atasema aliye na ushahidi aulete hapa.
   
 5. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  ukiona hivyo hana msimamo yaani anayumba yumba kama machela. julikana upo wapi, simba au yanga?. mia
   
 6. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  maaumivu ya kichwa huanza pole pole
   
 7. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Nani aliyemtuma aseme kwamba USA imemtuma agombee uikulu?
   
 8. Kibona

  Kibona JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 1,021
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Anatakiwa aeleze kama hakununua uraia huko US au alinunua, hiyo habari ya wazazi wako hai haina mashiko.
   
 9. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  If wote humu ndani tungekuwa na mawazo chanya kama wewe naamini hata huu Upupu(Uzi) usingekuwepo hapa.
   
 10. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  alternatively kama kuna mtu ana ushahidi kwamba mheshimia alisema anaungwa mkono na US auanike hapa pia
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks, such a weak defense... we have hundred of Tanzanians with other countries passports and their parents are still alive in Tanzania

  the boy needs some improvement kwenye kupanga hoja
   
 12. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kila mtu anataka u Rais wa JMT! Mwambieni Nyalandu asifananishe kazi hiyo takatifu na kum manage miss TZ
   
 13. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Huyu jamaa ni mwongo mkubwa. Analidanganya bunge kuwa alimaliza shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Wartburg, Waverly, Iowa. Sisi tuliokuwa naye darasani tunashangaa maana hakumaliza chuo kwa kushindwa kumaliza madai kulikotokana na kutoroka toroka kila wakati. Ilifika wakati akawa anatafutwa na FBI kwa kosa la human trafficking pale alipokuwa anawatapeli watu kwa kuwapa makaratasi ya kuingia Marekani.

  Aidha yeye ana Green card ambayo watu wengi wanadhani huo ndio uraia wa Marekani.


   
 14. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mbona mnamuandama sana huyu jamaa aisee...kuna nini hapa?mbona hamfanyi hivi kwa nchimbi ama kwa mfutakamba?huyu anawatisha nini?au ni kweli kwamba mti wenye matunda ndio hupopolewa kwa mawe ?kuna kitu hapa.
   
 15. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mzee green card sio uraia wa marekani...
   
 16. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Hilo ni kweli kabisa Mkuu, December kuna vijana wawili wa Kinondoni walikuwa wanavuka Tunduma Border post wakitokea South Africa na Passport za Huko, na walipofika pale wakapewa two weeks za kukaa Tanzania, na wakaanza kupiga kelele kuwa wao ni watoto wa kinondoni na wazazi wao wapo Kinondoni, wale MAaafisa wa uhamiaji wakawaambia sawa lakini wao sasa ni wa South Africa na Hawana pesa za kukaa zaidi ya hizo wiki mbili
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kusema kweli nyalandu ni mbabaishaji,mjanja mjanja na mpenda maslahi binafsi.utetezi wake ni dhaifu kwa mtu mwenye akili timamu.
  kuwa na wazazi hai watanzania haikuzuii wewe kuwa na uraia wa nchi nyingine,tena kwa marekani wanafrai kiintalijensia.aseme ukweli.
   
 18. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ​hana tofauti na bendera
   
 19. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Mtanzania halisi hana haja ya kuutetea uraia wake kwa waandishi wa habari, ukiona hivyo ujue there is something fishy over there....
   
 20. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwa nn isiwe membe au mtu mwingine yeyote ije kuwa yeye tu kuna kitu kwa huyu jamaa.Nayo ccm sasa imefikia pabaya kuhusiana na hizo kambi zao mpaka kunywa chai na mtu wa kambi nyingine inakuwa tatizo.
   
Loading...