Lawrence Masha: Kutoka Uwaziri hadi kukusanya takataka Dar

First time naingia kiwanja, nikakutana na dada mmoja mnyamwezi, katika kumdodosa small talk - tulikuwa stuck in an awkward position ambayo small talk muhimu, siyo kwamba nilikuwa namtokea wala nini- nikamuuliza, wewe una goals gani? Unataka kufanya nini baada ya kazi hii sorta dead end?

Basi mie nina mentality zile zile za "lawyer and doctor". Mdada akaniambia anataka kufanya kazi katika Waste Management, and not in those refined terms. Nikamuangalia mara mbili kutafuta any hint of sarcasm, lakini nikaona yuko serious kabisa.

Akanielewesha vizuri kabisa kwamba she has a passion for preserving the environment, she sees waste management as the perfect career kwake yeye kufanya kitu ambacho kitam satisfy intellectually/emotionally etc na at the same time ata make good money.

Huku nimetoka bongo mjomba alitaka kuwa accountant partly kwa sababu hakutaka kufanya kazi itakayomchafua.

The dichotomy in the thought process can be staggering.

Basi mwenyewe

Huyo dada kwa kweli naweza kusema aliokoka, maana wengi wetu hatufikii kiwango cha uamuzi huo. Na mara nyingi tunapokuja kuangukia uamuzi huo ni too late kwa vile wakati ambao tungepata nafasi zaidi tulidharau na matokeo tumechakaza kandambili kupitisha resume huku na kule bila mafanikio. Nimeipenda post yako Kiranga.
 
Pale alikuwa anasafisha jina tu taka zenyewe anazoa maeneo ambayo ni masafi eti masaki, oysterbay, acean road si ndio kupeana kindugu huku kwani hawakuona mbagala, tandale nk anadai walianza na magari 4 now wanayo 24 so wanafaidika still jiji linanuka kwa harufu ya takataka....Aaaaaaaggggghhhhhhrrrrrrrrr kupeana huku hadi lini?????????
 
Point aliyoongea siku ile ni kwamba ukienda kenya utakuta vitabu kuhusu nchi yao na hata viongozi wao akatolea mfano raila odinga, mwai kibaki kisha akadai mwanae anayesoma South Africa aliporudi nchini akamwambia anataka kitabu kichoelezea nchi yetu mzee akapaki na kigugumizi....kweli hatuna vitabu vinavyoelezea nchi yetu????

2. Alimwambia mwanae pesa zangu ni zangu si zenu hili niliikubali lazima mtoto achakachue ubongo
 
Pale alikuwa anasafisha jina tu taka zenyewe anazoa maeneo ambayo ni masafi eti masaki, oysterbay, acean road si ndio kupeana kindugu huku kwani hawakuona mbagala, tandale nk anadai walianza na magari 4 now wanayo 24 so wanafaidika still jiji linanuka kwa harufu ya takataka....Aaaaaaaggggghhhhhhrrrrrrrrr kupeana huku hadi lini?????????

________________
jogoooooo.jpg
 
Amini usiamini yupo jamaa kaanza kufuatilia hii issue ya taka takribani miaka miwili sasa. na hiyo manispaa ya dar-es-salaam sijui or whatever they call themselves walikuwa hawana lolote kuhusu mbinu za kisasa. jamaa kawaandikia namna za kufanya kazi na kila siku wanakuja na maswali mapya anawajibu. Last i heard alikuwa anategemea mbivu leo tena huyu pimbi katokea wapi. Anyway this is not the first he's lost a good idea in Tanzania. Nakuhakikishia hapo kuna plans za skips na incinerators watch that space.
mkuu Waste Management sio issue ngeni kama unavyoielezea.
Imekuwepo for a long long time.
Waste collection,seperation into bio- degredable and solid waste,hatmaye kuseperate ferrous,metl from other solid materials ni study ambazo zinaozea makabatini mwa wasomi kwenye taasisi nyingi.
Ninacho mpongeza Masha ni at least ameanza from somwhere-waste collection/ mechanised.

Hii si biashara ndogo, inahitaji capital kubwa na si pesa tu, bali haa ardhi kwa ajili ya waste collection.

Ukiingia stage ya waste separtion inabidi mtaji uwe mkubwa zaidi kwa ajili ya hizo separation systems.
Manufaa yake ni katika kurecycle the recovered solid waste be it chupa,plastics,chuma(aluminium,steel) au hata hizo bio degradable wate zinzoweza kuoza na hatimaye kuzalisha mbolea.

It is big business , mtaji wako tu.
 
Sawa masha anaubaya wake. Ila sasa mulitaka aendee bar anywe bia asubuhi mpaka jioni? Ni funzo tosha kuwa yeye hategemei vyeo tu bali hata ujasiria mali anauweza na zaidi anaweza kubana matumizi kwa kuacha bia na kupiga chai.
 
Brother! Irregardless is same as regardless though some people like you think it is incorrect,and the meaning is 'Without being affected or influenced by something'
Lawyer's lawyer hawezi kuandika "irregardless" wewe.

Taja mwingine lakini huyu si "Lawyer's lawyer".
 
Wabongo wanafiki sana, wameleta mada kumponda Masha humu kuwa kachoka kwa vile anasomba taka, mara biashara ya kusomba taka imeonekana dili sasa wanahoji kaipata vipi, yaani vituko vitupo :frusty:
 
I would radher not wander into semantics, but I have made my point very clear, endind with a kudos for Masha.

Between myself and you, with your "agreeing to differ", who is wandering in semantics?

Wewe sema tu tuna differ, the agree in n"agree to differ" is as useless as the "ay" in okay.
 
Brother! Irregardless is same as regardless though some people like you think it is incorrect,and the meaning is 'Without being affected or influenced by something'

The ir in irregardless is redundant and needless as it does the same thing as the less.

I can understand "irrespective" being the difference of "respective"

But irregardless is redundant as you can drop the ir, write regardless, and mean the same thing.

This is an attempt at pomposity that actually exposes one's lack of mastery in this foreign language.

And this guy is supposed to be a "lawyer's lawyer" in bongo.

Irregardless | Define Irregardless at Dictionary.com
 
Kwenye kubeba taka taka,kapiga hela kibao.
Ni mradi unao dhaminiwa na EEC.
 
Between myself and you, with your "agreeing to differ", who is wandering in semantics?

Wewe sema tu tuna differ, the agree in n"agree to differ" is as useless as the "ay" in okay.
Well, it was just a polite way of getting you off the hook!
Shall I go further?
You win brother, you win!
But in case you havent noticed, a very wise fellow summerised my feelings about you,

Wabongo wanafiki sana, wameleta mada kumponda Masha humu kuwa kachoka kwa vile anasomba taka, mara biashara ya kusomba taka imeonekana dili sasa wanahoji kaipata vipi, yaani vituko vitupo :frusty:
Sayonara!!!
 
Wabongo wanafiki sana, wameleta mada kumponda Masha humu kuwa kachoka kwa vile anasomba taka, mara biashara ya kusomba taka imeonekana dili sasa wanahoji kaipata vipi, yaani vituko vitupo :frusty:

Kwa nini kuzoa taka iwe ni ishara ya mtu kuchoka? Mimi nilitolea mfano wa kampuni ya Waste Management, Inc. ambayo ni multi billion dollar company ili kuonyesha kwamba kuzoa taka siyo ku-lost kama ambavyo watu walikuwa wanadhania.

Ingekuwa jamaa ana dumpster-dive au anazoa taka kwa matoroli hapo ningeelewa. Lakini kwangu mimi kazi ni kazi tu alimuradi mtu anajipatia riziki yake kihalali.

Wengine hapa tumefanya sana kazi za maintenance (read: janitorial) wakati bado tunasoma na hiyo kwetu ni tajiriba yenye thamani sana kwani ilitufundisha mambo mengi muhimu yakiwemo nidhamu ya kazi, heshima ya kazi, na uthamini wa kazi yoyote ile impatiayo mtu riziki yake kihalali.
 
Pale alikuwa anasafisha jina tu taka zenyewe anazoa maeneo ambayo ni masafi eti masaki, oysterbay, acean road si ndio kupeana kindugu huku kwani hawakuona mbagala, tandale nk anadai walianza na magari 4 now wanayo 24 so wanafaidika still jiji linanuka kwa harufu ya takataka....Aaaaaaaggggghhhhhhrrrrrrrrr kupeana huku hadi lini?????????

Ever heard of 'target market'? we unadhani taka tandale litaisha? utalipwa kiasi gani?
Hata mi ningeenda MASAKI tu na ningewachaji kimasaki kwa 'dola'
Waswahili wanaambiwa kulipa 3000 kwa mwezi wanaona nyingi, sasa wewe operating costs utaweza kwa staili hiyo?

In fact kama Mh. anasoma JF ani PM nipige kibarua kwake.
 
Sijasikia ufisadi wa Masha katika pitapita zangu. Alikuwa kiongozi na mbunge kama wengi walivyo ambaye hakuwa na misukosuko kama ya akina vijisenti. Kushindwa ubunge Nyamagana si hoja ya ufisadi ila sera kwa wananchi. Kushindwa kuingia mjengoni Dodoma si kushindwa maisha, kama mwenyewe alivyosema sasa anajisikia ana nafasi ya kuitunza familia yake na pesa kuingia mfukoni kuliko alipokuwa mbunge.

Kutokana na upe wetu wa kupata bure na kuuza kura kwa wagombea, kila aliyeingia mjengoni hujisikia anasakamwa na wapiga kura wake kupata cho chote jambo linalofanya wabunge wadai ziada wawapo vikaoni. Huu ni ugonjwa mbaya, njaa ndiyo inayotuumbua na kuwaumbua wabunge. Tunawanyooshea vidole wabunge kumbe ni sisi wenyewe ndio tunaosababisha wadai zaidi. Tukishakuwa na mbunge tunataka chakula restaurant atununulie bure, bia bure, vinywaji bure na pengine hata nguo bure, ukishindwa kulipa rent unaenda kwa mbunge akumegee ukalipe. Akina dada kujipitisha kwa waheshimiwa hawa kuwasalimia eti hawana ada ya chuo au pesa ya mkopo imechelewa mheshimwa nisaidia, hayo ndiyo yawapatayo wabunge.

Nakubaliana na wewe kuhusu haya uliyoyasema. Nami pia natambua kuwa kazi za mmbunge ni pamoja na kuwawakilisha wapiga kura wake katika bunge ambapo hujenga hoja kwa madhumuni ya kuwatetea wao. Kila mwananchi anao wajibu wa kufanya kazi ili kujiletea maendeleo. Kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira murua ili wananchi wawezi kutekeleza kazi zao vizuri. Hivyo ni jukumu la mbunge kuisimamia serikali ili itekeleze wajibu wake kwa wananchi.

Hata hivyo hoja yako haijajibu swali langu " kwa nini unamtetea masha?
 
Nakubaliana na wewe kuhusu haya uliyoyasema. Nami pia natambua kuwa kazi za mmbunge ni pamoja na kuwawakilisha wapiga kura wake katika bunge ambapo hujenga hoja kwa madhumuni ya kuwatetea wao. Kila mwananchi anao wajibu wa kufanya kazi ili kujiletea maendeleo. Kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira murua ili wananchi wawezi kutekeleza kazi zao vizuri. Hivyo ni jukumu la mbunge kuisimamia serikali ili itekeleze wajibu wake kwa wananchi.

Hata hivyo hoja yako haijajibu swali langu " kwa nini unamtetea masha?

Binafsi sina sababu za wazi za kumtetea Masha ila najadili mada iliyoletwa. Anayofanya Masha sasa hivi kuendesha maisha yake ni jambo ambalo limenikuna sana. Pamoja na kwamba ni shughuli kwa ajili ya kuendesha maisha yake lakini kuna la ziada ambalo analifanya kuwatumikiwa wananchi bila ubaguzi kwa kuangalia matatizo na mahitaji ambayo miji yetu inakabiliana nayo na hayo aliyaona wakati yuko katika nafasi yake ya uongozi.

Viongozi wetu wametengewa kila mmoja chumba chake ndani ya nyumba yetu kuhakikisha anafanya vema, na aonapo kitu kingine katika chumba cha mwingine hata kama ana uwezo nacho kwa taratibu na mfumo wa ugawiwaji vyumba hivyo na mahitaji yake hawezi kuingia chumba cha mwingine kwa kuwa si himaya yake, kwani kila mmoja kuna ukuta unaotenganisha vyumba vyao. Mara nyingi mgawiaji wa vyumba kwa wahusika huwa hawaulizi chumba gani angependelea na anajisikia anauwezo wa kukitunza ikiwa ni pamoja na madhari na ukubwa wake, makandokando yake na miundombinu yake iwe ya sakafu, vumbi au kusanifiwa kwa misala, ni kumpachika tu kadiri ya mwono wake ili mradi pale kuna mtu.

Huyu Masha baada ya kuondolewa uringoni kwa
knockout ya ballot voters, awali alichanganyikiwa kidogo kiasi cha kuhamisha sponji ya kupangusia madirisha na milango, lakini baadaye katuliza kichwa na kuona maisha si kwenye siasa tu ila mradi bongo linafanya kazi na muhimu ni kubuni njia ya kuendesha maisha tokana na taaluma, uwezo ambavyo pamoja vinaweza kumtengenezea mazingira ya kuwatumikia wananchi wengi kwa uhuru ambao hatasumbuliwa au kunyoshewa kidole cha akipatacho awagawie kama alipokuwa mbunge. Hali kadhalika kufanya afanye mengi kwa ajili ya familia yake kuliko alipokuwa bungeni alichanacho alipaswa kuwaona wapiga kura wake kitu ambacho si wajibu wake ila mazingira ya mwono wa wapiga kura wengi wameleweshwa hivyo kwa miaka kadhaa sasa na kuona wabunge wanawajibika kwao kwa cho chote ambacho ni ziada ya wajibu wao na pia kinyume cha utumishi wao kwa wapiga kura wao.

Huduma anayotoa Masha wengi wenye nafasi hawajafikiria kabisa. Nilishuhudia kipindi cha Pasaka nilitembelea rafiki yangu Maeneo ya Keko, nikaona gari la Kisasa la kusomba uchafu na wafanyakazi wakizoa taka maeneo ambayo hapo awali yalisahaulika kabisa uchafu uliishia ukikauka ni kuchoma moto yawe majivu na kuchafua mazingira.

Masha ni mfano wa kuigwa kwa ujasiri mali na ubunifu wa njia za kusafisha jiji, kwani wafanyakazi wa Jiji miaka yote walikuwa na magari lakini maeneo mengine kama hayo hayakuguswa. Pia anatoa funzo kwa wengi ambao wakishashindwa siasa wanahaha kurudia huko kwa njia mbalimbali badala ya kubadili mwelekeo na kufanya mengine ambayo yanaweza kuwafanya watulize kichwa na hata kuwa na huduma bora kwa wananchi kwa utulivu kuliko ukiwa mbunge wengi wetu kwa upeo finya wanataka kupewa fadhila kwa kura waliyokupa na hata kama hawakukupigia wakati huo watakuonyehsa kuwa walikupa kura huna budi uwalipe fadhila ya kukuingiza mjengoni.

Watanzania tusiwe watu wa kuona mtu akishindwa upande huu basi maisha yawe yamemshinda na hata akigeukia upande mwingine hakuna kitakachomwinua, tujifunze kwa wenzetu ambao kwenye ukweli mtu akifanya kitu kizuri wanampongeza na hata kumpa nishani kwani ni huduma ya umma. Waafrika wengi wetu tuna hulka ya wivu usio wa maendeleo na huo ndio unaotusumbua. Wazungu wangemtengea mtaa utakaoitwa kwa jina lake sababu ya huduma yake kwa jamii lakini bongo hiyo watasoza wee kama ilivyotokea kipindi cha Meya wa jiji la Dar Kitwana Kondo kuzienzi baadhi ya barabara kuu jijini Dar es Salaam kwa majina ya waheshimiwa fulani akina Nyerere, Mwinyi, Kawawa nk. ilikuwa nongwa lakini leo wametulia na majina ya mitaa hiyo yanaendelea.

thereitis@ umekuwa na mwona mzuri kuhusu wajibu wa mbunge kwani wengi wetu tungekuwa tunajua fika wajibu wa mbunge kwa wananchi na serikali tusingekuwa tunawasumbua kuwaomba nauli tukiwa Dodoma bila kufikiria tulifikaje Dodoma bila kupanga njia ya kurudia nyumbni.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom