Lawrence Masha: Kutoka Uwaziri hadi kukusanya takataka Dar

thanks, nijuavyo mimi jamaa alifanikiwa.... sasa mengine naomba unijuze ili nielimike

Sasa kwa nini unaweka comment heavy namna hiyo wakati hauna sufficient information?? Habari zake zote zimo humu humu ndani, get trouble and search sina mpya.
 
Hawa ma-lawyer si ndiyo tunaambiwa wanajua sana Kiingereza...? Sasa iweje huyu jamaa anukuliwe akisema "there's a lot of works"?

Or that was just a slip of the tongue?

Masha siku moja kaandika "irregardless", nikasema huyu ndiye super-lawyer wetu kakulia NY!!!

Ukiona hivyo mara nyingine unakuwa tempted kumsamehe Zitto Kabwe by fiat makosa yote ya lugha atakayoyafanya maisha yote.
 
Hapa some comments utafikiri kuna simpletons wanafikiri Masha anazama kwenye majalala anaokota takataka kwa mikono bila gloves, halafu analipwa thumni kwa kila pipa.

Hizi habari za kujifanya uungwana usio na tija ndizo zinazokosesha watu deals. tai shingoni, njaa tumboni.

Mie sina beef na ukweli kwamba kazi anayofanya ni nzuri. Hata kama isingekuwa nzuri, social statement tu ya mtu anayesafisha mji ni kazi ya heshima. Ndiyo maana mie hata vile vibibi vya City vilivyokuwa vinafagia barabara bila gear nilikuwa naona wanafanya kazi ya heshima sana iliyotusetiri.

Lakini watetezi wa Masha bado hawajaweza kutupa imani kwamba hakuna some oligarchy moves zilizotembea ku secure deal.

Yaani Masha is on the brink of being exemplary, except for this one troubling aspect which remains murky.

Kama yeye ni msafisha takataka kweli akiweza kusafisha na hili atakuwa kacheza.

Mkienda ndani sana ya huu mradi wake mtakuta hayo magari yote ameyakopa na mkopo uko guaranteed na serikali zaidi ya asilimia 85. Muulizeni Zitto.
 
Swali hapa si anachokifanya, bali, anavyokifanya. Tunaangalia kama hili deal limefanywa bila mushkeli. Ushaelewa issue?

Ukiwa mzinzi uta project uzinzi wako kwa kitakachopitia macho yako. Ukiwa na roho mbaya, hata mtu anayesimamia standards utamuona anafanya hivyo kwa sababu ya roho mbaya. Huna exposure ya kuelewa core principles za fre trade zinasemaje.Hujui "oligopoly" ni nini. Huelewi kwa nini Wa Rusi wanaandamana kuipinga oligarchy ya Vladimir Putin na wenzake. Hata sie tukiwa tunaelekea huko huko pole pole utashangilia tu. Halafu kesho utarudi hapahapa kupinga ufisadi.

Mie siwezi kupinga ufisadi superficially halafu ikija nafasi ya kuuliza some core principles za free trade (transparency, open tenders etc) unasema roho mbaya. Kitu kibaya ninachokiona hapa ni exposure ndogo ya watu kuhusu free trade na precepts zake.

Kwanza sijasema nakubaliana au sikubaliani na Masha. My issue is solely about making sure that standards are followed. Nimesema hapo juu napenda viongozi wanaojua biashara, lakini hili halimaanishi hata wakijikwapulia biashara bila kufuata sheria tukubali tu. Si tumemsema sana Mkapa na Kiwira hapa? Mimi nataka kuhakikishiwa tu kwamba hii biashara si a mini-Kiwira for a mini-Mkapa. What's wrong with that? Nataka uthibitisho tu kwamba mambo yameenda sawa, hata sija mu accuse kwamba kafanya vibaya, ni swala la due diligence tu.Kwamba kabla hatujaanza kumsifia Masha, tujue kwamba anafaa kusifiwa.

But I am sure some of y'all hata due diligence hamjui ni nini, by the looks of your posts at least I am justified to say so.

Trade secrets zinahusika na jinsi gani unafanya kazi yako, mitambo unayotumia, client list, etc.

Mimi nauliza biashara ilivyopatikana.Ilitakiwa kuwa na open tender, ilitakiwa kuwa na open and fair competition to all.Hakuna trade secret katika kuniambia ndiyo, tender ilitangazwa, kampuni fulani na fulani zilishindania, Masha hakutumia influence peddling na kwa kweli ndiye aliyeibuka mshindi kihalali, nikiridhika sitakawia kumsifu.

Lakini hatujajua hata kama tender ilikuwapo? Kwamba inawezekana Masha kapewa biashara mezani bila ya tender kushindaniwa? Unataka nione huyu ni enterpreneur? Huyu ni robber baron tu, kitu ambacho wenzetu wanakip[iga vita kila siku.

Biashara gani unayoongelea wewe? Biashara ya kinamama kuuza vitafunio Maandazi Road?

Unafahamu rules of free trade? Unafahamu free market ni nini? Unafahamu oligopoly ni nini? Unafahamu fair access to market ni nini? Unafahamu role of competition in free trade ni nini? Unafahamu influence peddling ni nini? Unafahamu open tender ni nini?

Mkuu waachie wafanyabiashara wafanye biashara zao.
Stop poking your nose there, ukitaka kufanya biashara , kata leseni uingie ngoma na ucheze.

We inaelekea ni msomi , tena mzuri tu, endelea kukata na kudisseminate issues kwa kwenda mbele lakini ukifikiri mtu(private business man) atakuja kukupa data za bishara zake hadharani, is being naive.

Nimeipenda hii ya Masha pamoja na kuwa utendaji wake serikalini ulikuwa na mushkeli.
Lakini you can always note an entrepreneur-making money from dirt to cash!-is a novel idea !

Sasa mkuu wewe endelea kukata issues hapa JF.
 
Mkienda ndani sana ya huu mradi wake mtakuta hayo magari yote ameyakopa na mkopo uko guaranteed na serikali zaidi ya asilimia 85. Muulizeni Zitto.

Oooo,

Guaranteed na serikali kwa minajili gani? Au ndo kapewa bailout ya fedha za walipakodi baada ya kushindwa siasa?
 
Masha anaweza kuwa na mapungufu yake kama mwanadamu, lakini nimependa jitahada zake za kuleta magari ya kisasa kuzoa taka. Tumechoka na malori yanayomwaga matakataka njiani. Kazi nzuri kijana Lau, ukisafiri iga mazuri.

Hongera zake Masha. Ni bora kutoa jasho kuliko kula vya bure kama wana siasa wengine
 
Leo nimemsikia aliepata kuwa waziri wa Mambo ya ndani Lawrence Masha akihojiwa na EATV akasema anafanya kazi ya kukusanya/kusomba taka toka ktk makazi ya watu, alikana kuwa alikuwa anafanyia kazi zake ROSE GARDEN ila alikubali kuna wakati alikuwa anashinda pale na akasema alikuwa anaenda pale na chupa yake ya chai anakaa hadi usiku mnene.
Lakini pia kuna tetesi toka Mwanza kuwa alikuwa akienda club anasindikizwa na Defender mbili za polisi na zinalinda club mpaka atakapoondoka, bado ana ndoto za kutumikia umma kama watu watamuomba.

My take: Sikio la kufa...

hapa mwanza aliwatesa na kuwanyanyasa sana askari wake. siwezi bisha kama alikuwa anaagiza lindwe villa, mwanza hotel na delux. kwani kuna askari waliokuwa wakipangiwa kulinda kwenye geti la nyumba yake, mauzi waliyokuwa wanayapata kutoka kwa mahawara zake, walitamani kupiga risasi mtu, lakini waliamua kuvumilia yote. ndiyo maana kwenye kura, aliambulia kura 3 tu kwenye kambi ya polisi mabatini
 
We inaelekea ni msomi , tena mzuri tu, endelea kukata na kudisseminate issues kwa kwenda mbele lakini ukifikiri mtu(private business man) atakuja kukupa data za bishara zake hadharani, is being naive.

Kinachoombwa ama kinachohojiwa hapa ni kama Masha na hiyo kampuni yake walipata hiyo zabuni kihalali pasipo na mizengwe yoyote. Kufanya hivyo si kuomba data za biashara zake. Hata mimi napenda kujua kama kweli taratibu na kanuni zote halali zilifuatwa. Kuna ubaya gani kwenye hilo?
 
Oooo,

Guaranteed na serikali kwa minajili gani? Au ndo kapewa bailout ya fedha za walipakodi baada ya kushindwa siasa?
Kind of. Kama kachukua mkopo kufinance hii investment swala la kuwa na Government Guarantee sio la kuprove, ni given kwamba ni part of the loan facility, kwamba sasa ameamua kuifanya hii investment a going concern tujipe muda, sababu namtambua kama mtu anayeamini katika kufilisi makapuni and he always get out of it safe.
 
Mkuu waachie wafanyabiashara wafanye biashara zao.
Unajuaje kama mie si mfanyabiashara? unajuaje kama sina interest kubwa tu kwenye kuhakikisha business culture Tanzania inakuwa na standards nzuri za fairness?

Stop poking your nose there, ukitaka kufanya biashara , kata leseni uingie ngoma na ucheze.

Unajuaje kama sina leseni ya biashara? Unafanya assumptions sio? kwa nini nisiulizie mambo ya biashara yanavyokwenda katika nchi yangu?

We inaelekea ni msomi , tena mzuri tu,

Sijawa na sitakuwa msomi.

endelea kukata na kudisseminate issues kwa kwenda mbele

Hapa una ji contradict. Mara don't poke your nose, mara endelea kukata na ku disseminate issues, which is which now?

lakini ukifikiri mtu(private business man) atakuja kukupa data za bishara zake hadharani, is being naive.

Wala sifikiri hivyo. Kuna swala jingine kabisa la kuamshana hapa kwamba jamani eeeh, kumfanya Masha kama mtu wa mfano bila hata ya kujua deal limeendaje na kama kuna mushkeli katika deal hilo ni ujuha.

What's wrong with that?

Nimeipenda hii ya Masha pamoja na kuwa utendaji wake serikalini ulikuwa na mushkeli.

Mimi sijapenda hizi habari kwamba kapata mkopo 85% guaranteed kutoka serikalini. Maana yake biashara ikifilisika walipa kodo ndio wanalipa deni.

Sasa hapo cha kufurahia ni nini?
Lakini you can always note an entrepreneur-makinh money from dirt!-its a novel idea into cash!

Sasa mkuu wewe endelea kukata issues hapa JF.

Nashindwa kukuelewa, mara don't poke your nose, mara endelea kukata issues. Which is which? Stick to one line.
 
Hata majambazi yanayoua watu na kuiba yanafanikiwa, kufanikiwa si swala. Swala hapa, kafanikiwaje?

ndio maana nikasema nijuzwe, sasa kurudia swali hakusaidii, all i wanted ni kujua from jamaa aliyeniquote kwamba masha alipataje utajiri?
 
Sasa kwa nini unaweka comment heavy namna hiyo wakati hauna sufficient information?? Habari zake zote zimo humu humu ndani, get trouble and search sina mpya.
what i see is what i get, and this is what i saw;
  • he was educated and became a well seasoned lawyer with IMMMA...
  • he became a success because of his law firm
  • he then went on politics and failed
  • he is back to the streets and doing business plus he is now back to the legal firm

generally kwa vipimo vya kwaida hii ni success

it is easy to point fingers... Yawezekana hata wewe uko succeful (indicators differ), na hatujui umepataje success hivyo our first reaction ni kukubali uko successful, and then we would be interested to learn how you got the success

siwezi kuanza na miwsho halafu nikamalizia na mwanzo

thank is how i approached my observations
 
Kinachoombwa ama kinachohojiwa hapa ni kama Masha na hiyo kampuni yake walipata hiyo zabuni kihalali pasipo na mizengwe yoyote. Kufanya hivyo si kuomba data za biashara zake. Hata mimi napenda kujua kama kweli taratibu na kanuni zote halali zilifuatwa. Kuna ubaya gani kwenye hilo?

swali gumu hilo
 
Leo nimemsikia aliepata kuwa waziri wa Mambo ya ndani Lawrence Masha akihojiwa na EATV akasema anafanya kazi ya kukusanya/kusomba taka toka ktk makazi ya watu, alikana kuwa alikuwa anafanyia kazi zake ROSE GARDEN ila alikubali kuna wakati alikuwa anashinda pale na akasema alikuwa anaenda pale na chupa yake ya chai anakaa hadi usiku mnene.
Lakini pia kuna tetesi toka Mwanza kuwa alikuwa akienda club anasindikizwa na Defender mbili za polisi na zinalinda club mpaka atakapoondoka, bado ana ndoto za kutumikia umma kama watu watamuomba.

My take: Sikio la kufa...

du, mimi simdharau kabisa, bado yupo juu, unafikiri kupata hiyo tenda ni mchezo, jamaa anapata ela nyingi
 
Nashindwa kukuelewa, mara don't poke your nose, mara endelea kukata issues. Which is which? Stick to one line.

Mkuu unashindwa kunielewa kwa sababu pamoja na disseminations zako zilizoenda shule, biashara kitu ingine kabisa, na kama unafanya biashara na una leseni basi you might get some insight as to what I am talking about.
 
1. Naelewa biashara kitu kingine kabisa, na hata nchi zilizoendelea ambako watu wana rule of law, educated populations, higher transparency, dedicated watchdogs, the works, bado wafanyabiashara wanafanya milungula.
2. Ukweli huu hapo juu haumaanishi tukae kimya kama hatuna hata the most basic of scrutiny.

Yaani hapa basically kinachotokea ni kwamba, kuna uwezekano wizi -impropriety of sorts- umetokea katika deal hili. Hapohapo watu wanamsifu Masha kwamba ni mfano wa kuigwa. Mtu anakuja anataka habari zaidi kuhakiki kwamba hakuna wizi, wewe unachosema ni "wewe acha tu, huku uswahilini ni sehemu tofauti kabisa hamna sheria wala utaratibu"

Hii ndiyo attitude ya kututoa katika umasikini kweli?
 
Back
Top Bottom