Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,277
- 105,475
Masha ni raia mwenye haki ya kupata tenda hiyo. Kama tenda hiyo angegawiwa mgeni wa kutoka nje ya nchi tungelalama kwamba wazawa wananyang'anywa haki zao. Sasa nini tunalalama?
Completely off topic. Swali halikuwa kwamba Masha si raia, wala Masha hana haki ya kupata tenda. Swali lilikuwa kwamba anaweza kuuthibitishia umma kwamba hakutumia influence yake kama Waziri wa Zamani kupata biashara hii? Mpaka hapa hujajibu swali.
Kwa vyo vyote halmashauri au viwanda anakochukua uchafu na kuutupa wanamlipa na ni haki yeke.
Hili hapa hata sijui linahusikaje katika mjadala. Mjadala ulioibuliwa na post uliyoinukuu si kwamba Masha analipwa au halipwi. Bali kama anaweza kuithibitishia jamii kwamba hakutumia influence yake kama Waziri wa Zamani vibaya.
Tenda nyingi zinatangwazwa wengi wetu hatuna uwezo. Mfano nimeona wanaofyeka kando ya barabara kuu hutumia tengo badala ya matrecta ya kufyekea. Barabara mail zote ataimaliza lini?
Kwamba watu wana uwezo au hawana uwezo kwa kiasi gani huwezi kujua mpaka utangaze tenda. All the more reason vitu vifanywe kwa kutumia tenda iliyo wazi.
Masha amejitahidi kuwa na magari ya kisasa ya kusomba takataka, nini tatizo?
Tatizo mpaka sasa hujajibu swali langu, kwamba biashara hii ilikuwa na tenda iliyotangazwa peupe na watu wakapata nafasi ya kushindanisha proposals zao, Masha akashinda bila kutumia influence ya "Waziri wa Zamani" ?
Sio tunaona oligarchy inachanua kwa kutumia shortcat utafikiri Putin's Russia hapa halafu tukae kimya. Mara Kingunge ambaye hana historia wala uzoefu wa kuendesha kituo cha daladala anapewa Dar Bus terminal, Mara Marsha ambaye hana uzoefu wa kusomba taka- wait a minute- Masha na kusomba taka? Hili si deal la mshkaji wake William Malecela jamani? Maana William Malecela ndiye mwenye uzoefu na kazi ya kusomba taka, na huyu Swahiba wake mkubwa, wamesuka deal wote hawa au vipi? But that is no crime, let me not digress.
My point is, was this deal tranparent? Was it adhering the rules of free trade? Or was Masha using his oligarchs passport to gain a shortcut to this business?
Hujajibu swali.
Hata kama amepata tenda kwa uzito wa kivuli cha hadhi aliyo kuwa nayo, lakini je, uwezo anao?
Mwenye uwezo hahitaji kupata tenda kwa uzito wala kivuli cha hadhi aliyowahi kuwa nayo kisiasa. Akishafanya hivyo tu huyu mtu hana uwezo, ametumia "kubebwa" kwa sababu ya jina na connections.
vinginevyo asingekuwa nao asingekuwa na magari ya kusombea uchafu, angetumia mikokoteni kama wanaofyeka barabara kwa tengo badala ya mashine za grass eater.
Uwezo ni zaidi ya mitambo. Unaweza kuwa na mitambo ukashindwa kuitumia.
Masha ameacha shughuli za siasa na kuamua kujiajiri, tumpe moyo kuliko kuipa pesa za walipa kodi kama mawazili walifukuzwa.
Tatizo lako unaangalia graft - kuiba pesa za walipa kodi- katika upana mdogo.
Lazima nchi iheshimu business culture, fairness, free trade ili nchi ipate maendeleo katika biashara.
Sasa kama Masha hawezi kututhibitishia kwamba hakutumia influence vibaya katika kupata biashara hii anakuwa hana tofauti na yule anayeiba pesa za walipa kodi.kwa sababu anaweza kuwa si mtu halisi anayeweza kuifanya biashara hii kwa ufanisi kabisa, anaweza kuwa anawagharimu walipa kodi hao hao hela nyingi zaidi ya yule anayeiba fedha za walipa kodi moja kwa moja.
Lazima tuyaangalie mambo kwa undani zaidi ya kushabikia tu "Masha anafanya biashara badala ya siasa, therefore tumpe moyo" tumpe moyo bila kujua biashara kaipata vipi? ili iweje?