Lawrence Masha: Kutoka Uwaziri hadi kukusanya takataka Dar

Sikusema kuwa turudi kwenye Vyanzo Vya Vyuma kitu cha kunishangaza ni wachangiaji kuabudu kuwa ni Lau Masha ndie atakayeleta Hayo Magari ya Matakataka sio Mwingine.

Ndio Maana nikasema kama kutakuwa na fair privatization; Mtu anapewa Maeneo sio Lau Masha ana Monopolize the Market kama Sasa hivi hakuna Mwingine wa kufanya hiyo Biashara Isipokuwa Lau Masha, na hajui Socialist Economy his Mind is all about Profit Maximization Capitalistic Economy; Lini Unadhani faida anayopata atasaidia kijiji Umeme au watoto wazururaji?

Well, kama huyu utamwita Enterpreneur Nchi yetu Imeisha; Kwahiyo Unaona Lau Masha sio FISADI?

Sasa, NGELEJA akiingia kwenye Biashara akianzisha something New Very Motivational as an Enterpreneur pia hautaangalia his Past; Utaangalia sasa hivi kama nani? a Best Enterpreneur

Kama nilivyosema kuna Wanaomodernize Business in a good heart for the betterment of the country

There are some who are ME ME ME; Sasa hivi Lau Masha hawezi kuifanya hiyo Biashara ya kuzoa Matakataka Mwenyewe
Unajua hakuna mtu Mpya wa kupewa kibali?; labda aingie Ubia na Lau Masha?

Ni kama vile CLOUD's wao wanaita Wanamuziki wa USA; kuna watu mbalimbali Watanzania Walioka Dar na USA wanataka kufanya hivyo lakini hawapewi kibali lazima Uende kwa CLOUD's yaani Wamemonopolize hiyo Biashara

Sasa hapo itabidi kweli Uwalambe Miguu kama unataka hiyo Biashara yako; Lakini SIWEZI KUFANYA HIVYO I'M FREE SITAKI KUTAWALIWA TENA na VICAPITALIST.

Mkuu nashukuru tumeelewana japo 50%... i dont think lau ni msafi, na ndio maana nikasema napenda enterpreneur na sio fisadi... i looked at kuzoa taka, kwani mleta mada alitaka kutuaminisha kwamba kuzoa taka ni ku-lost

kuhusu modernization with good heart, wapo, na kaa ujue kwamba ile biashara si ya marsha pekee... na kuhusu monopoly, sioni tatizo, kwa wenzetu hizo kazi zinaenda kwa zone, na mgeni anaweza kufanya kazi eneo lako kama mtakubaliana kufanya kazi pamoja... sio blue cab zote ni mali ya mtu mmoja, bali huwa ni mali ya wanachama. so far waliojiingiza kwenye hiyo biashara ni wachache, wakiongezeka, competition itakuwepo na tenders zitakua floated na vendors wataungana tu, hilo halina ubishi, ila ku-judge kama alipata kihalali au wengine vipi nadhani ni mapema sana kwani yeye na manispaa ndio wa mwanzo kabisa kuleta hayo magari (manispaa zilianza hiyo biashara miaka kibao sasa.... wengine walioingia kwenye hio biashara walikuja na ma-skrepa kufnya biashara

kuhusu kibali cha kuleta mwanamuziki kanataaa.... east africa walishawahi kuleta wanamuziki bila kupitia clouds kwahiyo hapo umedanganya

pamoja
 
Maisha ni safari kuna kupanda na kushuka.

we ndiyo umesema ukweli. Uchumi wa dunia wenyewe unapata shake up sembuse Masha!
Kinachotakiwa kufanywa na waliopewa dhamana ni kwamba watambue kuna kupanda na kushuka.
 
You guys have failed to understand Lau... he is a great success businesswise

Kampuni yake ni kubwa, bado ni lawyer (sio ganga njaa), na majibu aliokua akitoa kama ulimsikiliza vyema alikua anakebehi wauliza maswali zaidi ya kuweka vitu wazi

Ati anatoka na chupa ya chai home kwenda kushinda rose garden hadi usiku mnene!!

He is way too ahead of the game

kazi kwenu

bado hajafikia hatua ya kusemwa kafulia!tell them bro!
 
Masha anaweza kuwa na mapungufu yake kama mwanadamu, lakini nimependa jitahada zake za kuleta magari ya kisasa kuzoa taka. Tumechoka na malori yanayomwaga matakataka njiani. Kazi nzuri kijana Lau, ukisafiri iga mazuri.

Wewe acha ujinga unajua mkataba aliongia na manispaa hayo magari unayaona maeneo ya manzese na kwa mfuga mbwa hii nchi wanakula wenye meno si ww msifia mambo usio yajua.
 
Wakati mwingine inakuwa ni vigumu sana kuwaelewa watanzania ni watu wa aina gani wao kila kitu wanapondea hakuna jambo zuri machoni pao na hili ni tatizo sitaki kusema sana ila wewe mtoa mada acha negativity pamoja na wachangiaji wengine wengi.Msikimbilie kuandika vibaya kuhusu mtu kama hukumuelewa.
 
yaani anazoa taka kama mjasiriamali au ni mambo ya mpanda ngazi hushuka
 
Masha anaweza kuwa na mapungufu yake kama mwanadamu, lakini nimependa jitahada zake za kuleta magari ya kisasa kuzoa taka. Tumechoka na malori yanayomwaga matakataka njiani. Kazi nzuri kijana Lau, ukisafiri iga mazuri.
Safi sana.
Namuunga mkono kijana Lau kwa jitihada za wazi za kujiingizia kipato kuliko kutegemea mapato toka jitihada za kisiasa tu.

Mtu anayemzomea Masha kwa hakika ni mbumbumbu na hajui kupata kupitia jitihada za kibiashara.
Hao ndio wanatumika kuandamana tu na kutumika kisiasa kwa ujira wa kupewa bendera na scarf za blue/red.
Lau apewe hongera kwa kupata kipato cha uhakika wakati wengine wanasubiri ruzuku huku wakipiga miayo.
 
Hana lolote masha, alipokuwa waziri wa mambo ya ndani alishindwa kumshauri Rais kuwawekea maisha mazuri askari polisi na magereza.
 
Safi sana.
Namuunga mkono kijana Lau kwa jitihada za wazi za kujiingizia kipato kuliko kutegemea mapato toka jitihada za kisiasa tu.

Mtu anayemzomea Masha kwa hakika ni mbumbumbu na hajui kupata kupitia jitihada za kibiashara.
Hao ndio wanatumika kuandamana tu na kutumika kisiasa kwa ujira wa kupewa bendera na scarf za blue/red.
Lau apewe hongera kwa kupata kipato cha uhakika wakati wengine wanasubiri ruzuku huku wakipiga miayo.

Asante kwa kauli yako nzuri dhidi ya Masha. Wengine baada ya kuenguliwa serikalini au kukosa nafasi ya kuendelea kula za walipa kodi wanafanya kila njia kupenya chamani au kupata udc au ubalozi ili mradi kuendeleza ulazi na mapato kwa njia ya mkato. Huo ni utumwa wa kifikra na uvivu uliokithiri. Wengi waliosoma wanafikiri kupata ajira au kujiajiri ni kushinda kwenye viyoyozi, hizi ni fikra finyu. Bila shaka wala hofu nasema wengi wetu ni wavivu na legelege wasiojituma

Masha ni mfano mzuri wa kuigwa na wengi. Napenda jitihada zake hizo. Tunatakiwa kuangalia nini kinakupatia pato lako la kuishia au kujikimu kimaisha papo unawezaje kwa shughuli zako kusaidia huduma kwa umma. Ndivyo Masha anavyofanya. Vijana wengi kuanza shamba la mifugo au shamba la mazao wanaona ni aibu bora kwenda kuuza vocha au kuanya kazi kwenye maduka ya wahindi. Kumbe mama mtilia kipato chake ni kikubwa kuliko hata askari posili wenye wa daraja la chini wanaolipwa mishahara na serikali. Kwani kuna idadi kubwa tu ya mama ntilie ambao wamejijengea nyumba zao tokana na jasho lao tunalolidharau wasomi kila leo. Wale samaki wa feri wanawafanya waishi. Wasomi tungetazamia mambo hayo wayainue kisomi ila ni dharau wanataka kushinda kwenye viyoyozi.

Masha kuishi kwake Marekani kumemfungua macho, kwani Marekani hawaangalii elimu au shahada za mtu, ila bongo lako linavyofanya kazi na ubunifu wako ndio utakaokupa neema. Wasomi wameacha kazi tunazofikiri za kisomi na kuingia kazi ambazo wanaona zinawasaidia kupanda kimaisha. Bongo bado tunachofikiria ni kazi za kuvaa vizuri na kumeremeta, je zinaingiza nini mfukoni mwako kama si kukutoboa mfuko kuliko kuuziba? Maprofesa baada ya kumaliza tuition wanaingia kufagia vyoo na maofisi ya viwanda kama part time, pato hilo ndilo linalowasaidia kutengeneza ziada ya kuendeshea maisha, sisi tunaweza?
 
Masha anaweza kuthibitisha kwamba kapata hii biashara bila ya kutumia influence yake ya "Waziri wa zamani" ?

Hii kazi inaendaje? Analipwa na nani? Ilitakiwa kutangazwa tenda? Kama ilitakiwa ilitangazwa?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Masha anaweza kuthibitisha kwamba kapata hii biashara bila ya kutumia influence yake ya "Waziri wa zamani" ?

Hii kazi inaendaje? Analipwa na nani? Ilitakiwa kutangazwa tenda? Kama ilitakiwa ilitangazwa?

Masha ni raia mwenye haki ya kupata tenda hiyo. Kama tenda hiyo angegawiwa mgeni wa kutoka nje ya nchi tungelalama kwamba wazawa wananyang'anywa haki zao. Sasa nini tunalalama?

Kwa vyo vyote halmashauri au viwanda anakochukua uchafu na kuutupa wanamlipa na ni haki yeke. Tenda nyingi zinatangwazwa wengi wetu hatuna uwezo. Mfano nimeona wanaofyeka kando ya barabara kuu hutumia tengo badala ya matrecta ya kufyekea. Barabara mail zote ataimaliza lini? Masha amejitahidi kuwa na magari ya kisasa ya kusomba takataka, nini tatizo? Hata kama amepata tenda kwa uzito wa kivuli cha hadhi aliyo kuwa nayo, lakini je, uwezo anao? vinginevyo asingekuwa nao asingekuwa na magari ya kusombea uchafu, angetumia mikokoteni kama wanaofyeka barabara kwa tengo badala ya mashine za grass eater. Masha ameacha shughuli za siasa na kuamua kujiajiri, tumpe moyo kuliko kuipa pesa za walipa kodi kama mawazili walifukuzwa.
 
Back
Top Bottom