BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,124
Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru tuwekee ushahidi hadharani wa kuonyesha uhalali wa kampuni ya Simon Group kumiliki 51% ya shirika la UDA. Tunataka kujua ni akina nani ambao walihudhuria kikao cha kuidhinisha kuuzwa kwa 51% ya hisa za UDA kwa Simon Group na kama hao waliotoa idhinisho hilo walikuwa na uhalali wa kufanya hivyo.
Pia tunataka kujua ni kiasi gani kilicholipwa kununua hisa husika kupitia cheque namba ngapi ya tarehe ngapi na cheque hiyo na ilitoka bank account ipi ya Simon Group. Pia tunataka ufafanuzi kuhusu malipo ya shilingi 320 million ambayo yaliingia katika bank account binafsi ya Idd Simba na yeye kudai hayo ni malipo yake toka kwa Simon Group kama mshauri wao kuhusu ununuzi wa hizo 51% ya hisa za UDA.
Tunataka kujua ni nani mkweli kati yako na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali ambaye amesema kwamba kiasi kilicholipwa ni 24% ambayo kwa malipo haya Simon Group haistahili kujipa umiliki wa UDA na pia katamka kwamba kikao cha hao waliodhinisha kuuzwa kwa 51% ya hisa za UDA hakikuwa kikao halali. Pia anaendelea kusema kwamba, “Kwa mujibu wa majibu ya Mlipaji Mkuu wa Serikali, Serikali haitambui uuzwaji wa hisa hizo.”
Tunachoona hapa ni juhudi zako binafsi kutaka kuhalalisha wizi wa shirika la umma mchana kweupe huku Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali akidai Serikali haitambui uuzwaji wa hisa hizo 51% na kiasi kilicholipwa ni robo tu ya thamani ya hisa husika. Pia anaendelea kusema kwamba, “Kwa mujibu wa majibu ya Mlipaji Mkuu wa Serikali, Serikali haitambui uuzwaji wa hisa hizo.”
CAG alisema alitoa mapendekezo ya kukiukwa kwa kanuni za uuzaji wa hisa hizo tangu mwaka 2011/2012 lakini yalipuuzwa. Alisema Uda iliuzwa bila kibali cha Serikali na hisa zilithaminishwa kwa Sh744.79 kwa kila moja Oktoba 2009, lakini Novemba 2010, zikashushwa mpaka Sh656.15.
Tuna kauli mbili za watendaji wa Serikali ambazo zinakinzana. Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kaweka ushahidi wake hadharani kwanini kafikia hitimisho kwamba uuzwaji wa hisa 51% za UDA kwa kampuni ya Simon Gropu ni haramu, na wewe unatwambia kwamba uuzwaji ule ni halali lakini bado hatujaona ushahidi wako wa kuthibitisha kile ukisemacho.
Tunasubiri kuuona ushahidi wako.