Lawrence Mafuru toka hadharani, madai ya hisa za wananchi kuuzwa

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,534
8,619
Siku ZA karibuni kuna MADAI mazito ambayo yanaongelewa kwenye Corridor ZA Hazina ,Bank Kuu , na maeneno mengine ..Juu ya serikali kuuza kinyemela shares zake kwenye mashirika Muhimu kwa nchi ....yenye faida...shares Hizo in zile ambazo kwa mujibu wa sharia serikali inazishikilia kwa niaba ya WANANCHI ...ikiwa na maana Kama ikiamuliwa KUUZWA basi umuhimu wa kwanza...ni KUUZWA kwa WANANCHI wa kawaida....Kama ordinary shares ....

Wakubwa nilioongea nao wanasema Kijana Lawrence Mafuru ...analalamika chini chini .....kwa watu wake wa karibu sana...,Mimi namshauri tu Kama kalazimishwa basi atunze ushahidi ...., wa waliomlazimisha ,Hasa ukizingatia yaliyomkuta DAUDI BALALI...Ambaye alilazimika kukimbia na " kufa " kwenye upweke na kuzikwa ugenini ...kwa vyovyote itakavyokuwa Kama jambo hili ni Kweli basi Ashinde Lowassa AU Magufuli lazima walioshiriki hili wataishia jela ...na kampuni inayonunua Hizo shares wananunua at own risk .....

Ni lazima itungwe sharia nchi hii ya kuelezea mambo ambayo Rais wa nchi na serikali yake hawawezi kuyafanya muda mfupi angalau Miezi Sita Kabila hawajamaliza muda wao ...naamini kabisa kuna mambo ya kuhusisha pesa nyingi Hivi hayafanyiki kwa Baraka zake Bali kwa hofu ya watu wake ambao wanahofia hawatakua kwenye serikali inayofuata na kupiga ZA mwisho ..mwisho ...ikiwemo kutumia mwavuli wa "Chama kimeelemewa".....wakati Hizo pesa hata kwenye Chama hazifiki Bali zinaishia kwenye matumbo Yao ..

Naamini wana Chama Kama wana uzalendo watapinga hili la Baadhi ya maafisa kuiba mabilioni kila uchaguzi kwa kigezo chao wakati si Kweli ...wanachafua chama ..

Hadi Sasa Gavana wa Bank Kuu bado hajaingia kwenye kashfa Hasa baada ya kujiapiza KUWA hawa watu wasimfuate kwa deal Hizo kwa KUWA hataki limkute la boss wake wa zamani la kutumika na kutolewa sadaka...


---------------------------------- ---------------------------



MAJUKUMU YA OFISI YA MSAJILI WA HAZINA:

Kukusanya mapato yasiyo ya kodi (non tax revenue) kutoka katika Mashirika na Taasisi za Umma yanayotokana na gawio, michango ya asilimia 10 ya mapato ghafi na marejesho ya mikopo.

Kuchambua taarifa za Hesabu zilizokaguliwa kutoka katika taasisi na mashirika ya Umma kwa lengo la kuchunguza mwenendo wa utendaji na kushauri Serikali ipasavyo.

Kuchambua taarifa za robo mwaka za taasisi na mashirika ya Umma kwa lengo la kupima na kubaini mwenendo wa ufanisi wa taasisi au shirika hilo.

Kuchambua na kuidhinisha nyaraka mbalimbali zinazohusu mashirika ya umma kama vile nyaraka zinazohusu kanuni za fedha, kanuni za utumishi, miundo ya utumishi, ikama na mifumo ya mishahara ya taasisi.

Kushirikiana na CHC kufanya uperembaji wa mashirika ya Umma yaliyobinafsishwa kwa lengo la kubaini tija na ufanisi wa mashirika hayo kulingana na mikataba ya mauzo, mikataba ya hali bora ya wafanyakazi.

Kufanya uhakiki wa Kimenejimenti kwa lengo la kubaini utekelezaji wa nyaraka/miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali.
Kupitia, kuhakiki na kuidhinisha bajeti na mipango mikakati ya mashirika ya umma na taasisi.

Kusimamia na kuishauri Serikali kuhusu uwekezaji katika mashirika na taasisi za umma.

MAFANIKIO

Kwa kipindi cha zaidi ya miongo miwili Ofisi ya Msajili wa Hazina imekuwa na mafanikio yanayotokana na utekelezaji wa majukumu yake. Baadhi ya mafanikio hayo ni pamoja na: usimamiaji wa mchakato wa ubinafsishaji wa mashirika ya Umma. Katika kipindi hicho mashirika yapatayo 320 yalibinafsishwa kati ya mashirika 363 yaliyotakiwa kubinafsishwa. Mashirika hayo yamendelea kuchangia mapato ya ndani ya Serikali, kutoa ajira kwa watanzania, kuleta teknolojia mpya katika uzalishaji na kuchangia katika utoaji wa huduma za jamii. Mafanikio mengine yamepatikana katika maeneo yafuatayo:


Ukusanyaji wa mapato yatokanayo na gawio, michango ya asilimia 10 ya mapato ghafi na marejesho ya mikopo kutoka katika taasisi na mashirika ya umma uliongezeka. Kwa kipindi cha 2011/2012 Ofisi ya Msajili wa Hazina ilikusanya shilingi bilioni 208.1 ikilinganishwa na shilingi bilioni 28.8 zilizokusanywa mwaka 2010/2011.

Uperembaji wa mashirika ya Umma yaliyobinafsishwa kwa lengo la kubaini tija na ufanisi wa mashirika hayo kulingana na mikataba ya mauzo. Kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2012 mashirika 170 yalifanyiwa uperembaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi kati ya mashirika 320 yaliyobinafsishwa.

Uhakiki wa Kimenejimenti kwa lengo la kubaini utekelezaji wa nyaraka/miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali. Katika mwaka 2011 uhakiki wa kimenejimenti ulifanyika katika taasisi na mashirika mbalimbali ambapo kiasi cha shilingi bilioni 3 kilibainika kulipwa kwa watumishi hewa.

Uwekezaji (mitaji) katika mashirika na taasisI za Umma kwa mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 June, 2012 uliongezeka kutoka shilingi 10,275,149,624,561.50, mwaka 2011 hadi kufikia shilingi 12,215,057,310,133.70 mwaka 2012 sawa na asilimia 189.

Ongezeko hili limetokana na mitaji iliyotolewa na Serikali kwa taasisi na mashirika ya Umma na hivyo thamani za mashrika na taaisi kuongezeka. Aidha, Serikali iliendelea kuwekeza katika mashirika na taasisi za nje ambapo hadi kufikia tarehe 30 June, 2012 mitaji katika mashirika hayo ulifikia shilingi 145,899,587,282.44.

ImageUploadedByJamiiForums1444706939.634026.jpg
 
ufanya chochote kile kwa kutumia mapungufu ya katiba tuliyonayo,
Suluhisho la haya yote ni katiba mpya. Ndio maana viongozi wa CCM waliipinga kwa nguvu zote ili waweze kupiga
 
Kipindi hiki ndio zinapgwa za mwisho...baadhi ya watumishi wamekuwa wezi nao watasingizia ni mfumo.
 
Hizi pesa zitakuwa zinapelekwa kusaidia kampeni za CCM tu. Maana maji kwa sasa yamewafika shingoni na pumzi Inaelekea kukata.
 
So sad miaka yote ..Miezi Sita ya mwisho Hasa baada ya bunge kuvunjwa zinaibwa sana hela na watendaji safari hii wamehama BOT wameenda kwa MSAJILI WA HAZINA .....
 
Hii sheria ya kuruhusu MAWAZIRI na MANAIBU wao kuendelea kukaa ofisini na kutumia rasilimali za nchi kwa faida zao wakati bunge limeshavunjwa na wao wenyewe wako kwenye kampeni za ubunge kwenye majimbo yao inabidi liangaliwe kwa makini sana. Kuna mambo mengi yanafanywa na mawaziri hao kwa kushinikiza ilhal bunge halipo tena.

Wanasheria na wataalam wengine inabidi waliangalie jambo hili kwa undani na ikibidi lipigiwe kelele kwa nguvu zote ili kuepusha mambo ya kifisadi kufanywa wakati watu wengi wako kwenye fukuto la uchaguzi
 
ufanya chochote kile kwa kutumia mapungufu ya katiba tuliyonayo,
Suluhisho la haya yote ni katiba mpya. Ndio maana viongozi wa CCM waliipinga kwa nguvu zote ili waweze kupiga

Ukiwa na mfumo wa hovyo uliojaa magoigoi yasiyoweza kuwadhibiti wezi wachache, katiba na sheria nzuri hazisaidii sana.
Tunahitaji viongozi safi wenye maadili na nia njema kwa taifa.
Kama watawala waovu wana nguvu na ikiwa wananchi ni magoigoi, katiba na sheria zinazowabana watawala zitabaki kwenye makaratasi tu!
Mara ngapi katiba iliyopo imevunjwa na hakuna wa kuhoji?
Hili suala la hisa ni muhimu sana kuhojiwa lakini watu wako kimya. Hii ni dharau kwa wananchi!
 
Kodi imeanza inaitwa RAILWAY DEVELOPMENT LEVY ............TAZAMENI KILA MIZIGO INAYOINGIA BANDARI ,AIRPORT ,AU MIPAKANI WANAPIGA 1.5 % ..Kodi ya kuchangia RELI ....!!!!!!!!!!

Mkuu nimeshtuka sana! Hii kodi itakua imeidhinisha na mamlaka gani?!
 
Chungurumbira kuna kodi gani mpya ndugu maana nataka kufanya mchakato wa kuvuta KLUGER yangu?

Kuna mtu wa clearing aliniambia kuwa kodi za reli! lakini hakufafanua zaidi though nimeangalia kwenye calculator ya TRA sijaona! Labda zimechomekwa na huku kwenye calculator tunaona jumla jumla tu!!
 
Back
Top Bottom