gasto genaro
JF-Expert Member
- Oct 15, 2014
- 780
- 554
Salaam wakuu,
Kumekuwa na uhaba wa ajira nchini kwa miaka kadhaa sasa. Kwa miaka ya hivi karibuni, badala ya tatizo hili kuisha, linazidi kuongezeka mara dufu hasa kwa vijana waliomaliza vyuo vikuu, stashahada na cheti.
Ukitaka kujua uhaba wa ajira nchini ni wa kiwango cha dunia, utakuta kampuni inatangaza nafasi moja au mbili tu za kazi, lakini applications zitakazotumwa, ni zaidi ya 500.
Katika kulidadavua hili, yapo makundi matatu yanayohusika katika cycle hii nzima ya ajira, katika makundi hayo matatu (ambayo nitayataja hapo chini) , ni nani wa kulaumiwa kwa kufanya suala la ajira nchini kuwa gumu?
Makundi hayo ni haya yafuatayo.
1. Shule/Vyuo/wizara ya elimu/taasisi mbalimbali za elimu.
Kundi hili ndilo linalohusika kuusuka mfumo wa elimu nchini, kufanya delivery ya huo mfumo ikiwa ni pamoja na mitaala shuleni.
Kundi hili ndilo limeusuka na kuung'ang'ania mfumo wa kusoma kwa nadharia zaidi na kukariri.
2. Serikali
Kundi hili ndilo linatengeneza mfumo wa ajira, mazingira ya wafanyakazi kufanya kazi, fursa za ajira pamoja na kulipa wafanyakazi mishahara.
Kundi hili pia ndilo lililo na mamlaka ya kusitisha ajira kutokana na sababu mbali mbali kama alivyofanya Mheshimiwa Rais JPM
3. Wahitimu/ wasaka ajira
Hawa ndiyo wale waliosoma kwa bidii zote kwa kufuata mfumo uliowekwa na kundi namba moja, na hatimaye wamehitimu na wapo mtaani kusaka ajira.
Hawana mtaji wa kujiajiri, wanazitajirisha stationery kwa copy na print za vyeti, barua na CV za ku apply kazi. Wengi wanawaza kuomba kazi maana mitaji ya kujiajiri hawana.
Je, hapa nani mzembe anayelifanya suala la ukosefu wa ajira lizidi kuwa sugu na anayefaa kulaumiwa kwa hili? Ni nani hasaa?
Nauliza..