Lawama nimpe Nani?

MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,470
6,562
Wapendwa hamjambo?

Ninaomba mnisaidie kufikiri maana sasa naiona dunia ya mapenzi kama uwanja wa fujo tu ambao natamani kama ningeweza kujiepusha nao niuepuke.

Nimesoma na kusikia visa vingi sana vya mapenzi ila ambacho ninashindwa kukielewa lawama nimtupie nani ni hiki cha mtu na shemeji yake!! Yaani iwe
1. mke kutembea na shemeji yake i.e. kaka/mdogo/binamu wa mume wake
2. Mume kutembea na shemejiye i.e. dada/mdogo/binamu wa mkewe.

(Nimewaexclude marafiki kwa kuwa nahisi wao hawaangukii kwenye huu mshangao wangu).

Je kosa ni la nani kati ya hawa?
 
Lawama kwa wote na wanastahili kutengwa na Jamii
 
MJ1 ..umemsahau mtu wa tatu. ambaye yupo kati yao..anaitwa Sheeeetani!

Ukiwa rafiki na huyu jamaa anakubadili akili na kuwa punguani au Juha hadi unaweza kutembea na mtoto wako au mama yako mzazi..
 
Wapendwa hamjambo?

Ninaomba mnisaidie kufikiri maana sasa naiona dunia ya mapenzi kama uwanja wa fujo tu ambao natamani kama ningeweza kujiepusha nao niuepuke.

Nimesoma na kusikia visa vingi sana vya mapenzi ila ambacho ninashindwa kukielewa lawama nimtupie nani ni hiki cha mtu na shemeji yake!! Yaani iwe
1. mke kutembea na shemeji yake i.e. kaka/mdogo/binamu wa mume wake
2. Mume kutembea na shemejiye i.e. dada/mdogo/binamu wa mkewe.

(Nimewaexclude marafiki kwa kuwa nahisi wao hawaangukii kwenye huu mshangao wangu).

Je kosa ni la nani kati ya hawa?

kusema wote wanamakosa inategemea na situation yenyewe, maana kuna sometimes mtu unafanyiwa visa mpaka unashindwa kupata suluhu, maana kusema kwa shemeji yako inakua ngumu ukiogopa kuvunja ndoa ya kaka au dada yako. ndo maana sa ingine mtu unasema "kubali yaishe"
 
Wote ni wakulaumiwa, adhabu kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu ni kuwatenga na jamii kama inawezekana.
 
Hata mahakamani kuna sheria ya "kuua bila kukusudia" kwa hiyo lazima tuangalie situation ilikuwaje mpaka ikapelekea hayo!
 
kusema wote wanamakosa inategemea na situation yenyewe, maana kuna sometimes mtu unafanyiwa visa mpaka unashindwa kupata suluhu, maana kusema kwa shemeji yako inakua ngumu ukiogopa kuvunja ndoa ya kaka au dada yako. ndo maana sa ingine mtu unasema "kubali yaishe"

hapo labda iwe amebakwa otherwise wote wana makosa makubwa sana! alikutongoza ungeniambia/nijulisha...visa kama vipi hapo vya kufanya utembee na shem wako?...ukiona watu wana mahusiano kama haya ujue wameamua kufanya, hakuna cha shetani wala ibilisi...cjui kama ntaweza wasamehe wote wawili.
 
MJ1 yote haya yanategemea na mazingira.Kuna couple moja naifahamu (tena ni wanene serikalini) mama aliolewa mimba ikawa haishiki,kupima akaambiwa hali si hali,all she did alikwenda kijijini akamleta mdogo wake wa kuzaliwa,tunavyoongea mme keshamzalisha watoto wawili na mahari ishatolewa.Mke mkubwa ana nyumba yake na mdogo ana nyumba yake.MJ1 hapa siongelei 1947 naongelea 2011.
 
Lakini ukumbuke kua kufanya mapenzi na mtoto chini ya miaka kumi nane ni kubaka hata kama walikubaliana si ndio?
 
hapa hatuongelei under age, 2fanye ni wa2 wazima na akili zao, amebakwa, na wa2 wazima nao c wanaweza kubakwa? hiyo ya kubakwa ntaielewa but sio wameshafanyaa weee nije nijue, hapo hakutakuwa na msamaha kwa wote wawili!...tabia mbaya sana sana hiyo!
 
Ni ngumu kutoa hukumu moja kwa moja, ktk hili inategemea v2 vingi mfano mazingira na ukaribu kwa kuhusisha hiv vichahche ndo waweza kuhukumu
 
Wote ndio mashetani wenyewe adhabu yao kufungwa jiwe la kusagia shingon na kutupwa baharin, kama atakuwa amebakwa basi mbakaji adhabu yake ni kuchemshwa kwenye pipa la mafuta mpaka aishie huko.
 
MJ1 yote haya yanategemea na mazingira.Kuna couple moja naifahamu (tena ni wanene serikalini) mama aliolewa mimba ikawa haishiki,kupima akaambiwa hali si hali,all she did alikwenda kijijini akamleta mdogo wake wa kuzaliwa,tunavyoongea mme keshamzalisha watoto wawili na mahari ishatolewa.Mke mkubwa ana nyumba yake na mdogo ana nyumba yake.MJ1 hapa siongelei 1947 naongelea 2011.

haya nadhani yalikuwa makubaliano.....
 
Zinaa ni uchafu haijalishi unazini na nani?
Mwanandoa kuzini ni kosa haijalish kazini na nan?
Wote wanamakosa!!
 
Lawama kwa wote na wanastahili kutengwa na Jamii

Wote ni wakulaumiwa, adhabu kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu ni kuwatenga na jamii kama inawezekana.

Wote ndio mashetani wenyewe adhabu yao kufungwa jiwe la kusagia shingon na kutupwa baharin, kama atakuwa amebakwa basi mbakaji adhabu yake ni kuchemshwa kwenye pipa la mafuta mpaka aishie huko.

Aksanteni nimewaelewa ni kweli hata mie ninavyoelewa ni kuwa wote wana makosa na hili ni fundisho kubwa nililolisoma hapa hapa JF. Zamani nilikuwa natupa lawama kwa wanawake. Kwa nini walikubali ilhali wanajua kuwa ni shemeji zao! sijui ndo nilikuwa najikubalisha kuwa victim is the one to be blamed kila siku?! Mwe aksanteni wana JF.

Hapo kwenye adhabu hapo, kwa trend hii tuliyo nayo sijui tutawatenga wangapi? Au ndo tuamue wengi waangamie ili kusafisha jamii??!
 
Makosa yatakuwa ya mwenza wa aliyemega au kumegwa.............kama humpi kitu ambayo akikaa ofisini anacheka mwenyewe unategemea nini???!!!
haijalishi kala/kaliwa na nani..........issue inabaki pale pale.......kaliwa/kala!!
 
Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom