LAWAMA: Hasa toka kwa wanawake

Nyakwaratony

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
573
140
Habari za jumapili mabibi na mabwana.....
Ningependa leo tujadiliane kuhusu LAWAMA hasa kutoka kwa wanawake. Kwa mfano, mmeo/boyfriend wako anapenda uwe unamjulisha ratiba zako. Ukitoka kazini au kwenye biashara zako utapitia wapi mpaka unapofika nyumbani lakini kwake yeye ni kinyume haweki wazi ratiba zake. Unaweza ukampigia simu kumuuliza yu wapi kwa wakati huo yeye akakujibu nipo kwenye kikao cha harusi (achilia mbali vikao vya kikazi au kibiashara hapa havihuasini) lakini hakukujulisha. Wewe mwanamke unaanza kulaumu ooh mbona hukuniambia kitambo mbona mimi hutoa ratiba zangu hata za salon?

Wanaume mnawachukuliaje wanawake wenye kulaumu kila wakati? Je ni sawa?

Wanawake je mnahandle vipi situation kama hii ya kulaumu laumu?

Karibuni kwa mjadala.
 
mie bwana ninapenda uwazi na taarifa...mambo yakuwekana roho juu juu mie sipendi. hivyo mie naona sawa tuu mke gf wangu kujua mizunguko yangu itakuwaje.
 
Haya mambo ya ratiba ndio hufikia watu wanapangia kupeana tunda...bao moja kwa siku kwa wiki mara moja
 
Hili ni tatizo la mapenzi ya kutarajia urudishiwe kitu
"
Unapokuwa na mwenza wako wewe penda tu bila kujali kama unarudishiwa upendo ama la!
 
Hili ni tatizo la mapenzi ya kutarajia urudishiwe kitu
"
Unapokuwa na mwenza wako wewe penda tu bila kujali kama unarudishiwa upendo ama la!

ubaya ni kwamba mtu huwezi kujiingiza ambapo unajua kabisa hapa hapafai
 
mie bwana ninapenda uwazi na taarifa...mambo yakuwekana roho juu juu mie sipendi. hivyo mie naona sawa tuu mke gf wangu kujua mizunguko yangu itakuwaje.

Ni wanaume wachache wenye positive perception kama wewe. Keep it up.
 
Haya mambo ya ratiba ndio hufikia watu wanapangia kupeana tunda...bao moja kwa siku kwa wiki mara moja

Mkuu ratiba humfanya mwenzi wako kuwa na amani hasa nyakati za usiku na uwapo safarini. Just imagine umesafiri umefika huko unapokwenda ukaishiwa charge, kumbuka wakati huo mwenzi wako hana taarifa kuwa umeishiwa charge. Je atakuwa na amani?

Ni vyema ukatumia simu ya mtu mwingine kutoa taarifa ya kuiashiwa charge ili mwenzi wako awe na amani. Au wewe una maoni gani? Tupe uzoefu
 
Hili ni tatizo la mapenzi ya kutarajia urudishiwe kitu
"
Unapokuwa na mwenza wako wewe penda tu bila kujali kama unarudishiwa upendo ama la!

Mkuu simaanishi mapenzi ya kutarajia urudishiwe bali mawasiliano kama mojawapo ya nguzo katika mahusiano ni vyema kupeana taarifa za ratiba zisizo rasmi.
 
Ni katika hali ya kutaka kufahamu usalama wa mwenzi wako.

hilo tu basi! usalama kwamba asichukuliwe/asichukuwe mwengine au usalama wa maisha?

Hizi ratiba ndiyo chanzo cha matatizo ikitokea kwa bahati mbaya tu hupatikani teyari kidonda, mashaka na wasiwasi kwa mpezi!

Babu zetu hawakuwa na ratiba za aina hii, wanahistoria nzuri sana ya kudumu katika ndoa zao, nyinyi na ratiba zenu ni ndoa za voda fast na kutengana hivyo hivyo.

Kinachotakiwa ni uvumilivu, uaminifu na upendo wa dhati kwa mwenzi wako. Ratiba inaokoa nini jamani kuliwakula kupo palepale.
 
mbona wengine mnayafanya maisha kuwa magumu? Yaani mnapeana ratiba ya siku? Huyo ni jumatatu hadi jumapili? Siku 7 za wiki, siku 30 za mwezi na siku 365 za mwaka? Khaaaaa
 
Mkuu simaanishi mapenzi ya kutarajia urudishiwe bali mawasiliano kama mojawapo ya nguzo katika mahusiano ni vyema kupeana taarifa za ratiba zisizo rasmi.

Uko sawa,hili ni muhimu.Tatizo unapoanza kupima kama nawe huambiwi hilo ni tatizo!
 
mbona wengine mnayafanya maisha kuwa magumu? Yaani mnapeana ratiba ya siku? Huyo ni jumatatu hadi jumapili? Siku 7 za wiki, siku 30 za mwezi na siku 365 za mwaka? Khaaaaa

Sio hivyo madame; nina maanisha ratiba zisizo rasmi. Let say mmeo amekwenda kazini kama kawaida ghafla akaambiwa na boss wake aende kibaha. Akaenda bila kukwambia, mara unampigia anakwambia yupo kibaha. We unalionaje hilo?
 
Uko sawa,hili ni muhimu.Tatizo unapoanza kupima kama nawe huambiwi hilo ni tatizo!

Lakini mkuu, Kuna usemi unasema "Unachopenda kufanyiwa nawe mfanyie mwenzio" kwanini yeye apende kupewa taarifa ila yeye asipende kutoa taarifa?
 
hilo tu basi! usalama kwamba asichukuliwe/asichukuwe mwengine au usalama wa maisha?

Hizi ratiba ndiyo chanzo cha matatizo ikitokea kwa bahati mbaya tu hupatikani teyari kidonda, mashaka na wasiwasi kwa mpezi!

Babu zetu hawakuwa na ratiba za aina hii, wanahistoria nzuri sana ya kudumu katika ndoa zao, nyinyi na ratiba zenu ni ndoa za voda fast na kutengana hivyo hivyo.

Kinachotakiwa ni uvumilivu, uaminifu na upendo wa dhati kwa mwenzi wako. Ratiba inaokoa nini jamani kuliwakula kupo palepale.

Naamaanisha usalama wa maisha, hiki ni kizazi kingine kabisaa tofauti na kizazi cha mababu zetu. Leo hii ukisema mimi sitaki kutumia simu ili nifanane na enzi za mababu zetu jamii itakushangaa. Tunapaswa kuendana na mabadiliko hasa katika teknolojia.
 
Back
Top Bottom