Law school of Tanzania yapandisha ada na gharama nyingine, kutoka 1,570,000/= mpaka 2,950,000/=

Junior counsel

Senior Member
May 17, 2022
190
503
Taasisi ya mafunzo ya uanasheria Kwa vitendo (LST) imepandisha gharama za mafunzo ya uanasheria kwa vitendo kutoka 1,570,000/= mpaka 2,950,000/=. Ikumbukwe kuwa malipo hayo hufanyika Kwa mkupuo mmoja.

Maswali ya kujiuliza;

~ Je, lengo la kupandisha gharama kwa kiwango kikubwa kiasi hiki ni nini?

~ Je LST inatoa huduma au inafanya biashara?

~ Je, watoto wa maskini ambao tayari wameanza kusoma sheria watumudu kiwango hiki, ukizingatia kazi nyingi za kisheria ili mtu aweze kuzifanya lazima awe anatambulika kama Wakili?

Je, LST walichukia kukosolewa na hivyo kupandisha gharama ili kuwakomoa wananchi?

Mwisho
Kwa sisi ambao bado hatujapata fedha za kutosha, usimshauri mwanao kusoma sheria, ni kozi fulani inahitaji uwe unajiweza kiuchumi.

IMG-20221126-WA0006.jpg
IMG-20221126-WA0007.jpg
 
Naona LST wameamua kuzua balaa jingine wamepandisha ada kwa takribani 88% (135000 shs estimate). Hii umeiona wapi? Sidhani kama inakubalika labda iwe mkopo. Ngoja tuone.
 
Sasa mtoto wa maskini unatafuta nini huko? Fanya mambo mengine
 
Taasisi ya mafunzo ya uanasheria Kwa vitendo (LST) imepandisha gharama za mafunzo ya uanasheria Kwa vitendo kutoka 1,570,000/= mpaka 2,950,000/...
Tayari kumeonekana kuna wimbi kubwa la watu kuchukua course ya sheria Sasa wanataka wawapunguze ili kubalance mambo na kurudisha heshima ya kozi husika.
 
Doh ichi chuo kina endeshwa na wasomi kweli.iyo ya kulipa tu ada full ni ujingaa
 
Uzuri si ya lazima sana
Nani aliyekudanganya kuwa kwa sasa sio ya lazima?kwa sasa mtu yoyote aliyemaliza shahada ya sheria lazima asomee uwakili kama ana mategemeo ya kuajiliwa kwani karibu kazi zote zinazo husiana na kada ya sheria wanataka lazima uwe umehitimu shule ya sheria.

Ndio maana sasa wanafunzi wamekuwa ni wengi sana kwani lazima ,Nadhani sheria ingebadirishwa ikawa wale wanotaka kuwa mawakili ndio lazima wapitie shule ya sheria lakini kwa wale wanaoenda kufanya kazi nyingine tu zisizohusiana na kwenda mahakamani isiwe kuwa ni lazima kupitia shule hiyo.
 
Shangaz.JPG

Ameandika Fatma Karume "Shangazi"

Failure rate ya Law School ni 95%…. 😂😂😂
Halafu eti wanapandisha ADA!!
Monopolies zisizokuwa REGULATED EFFECTIVELY ni WIZI tu!
Council of Legal Education mko wapi? Hii si kazi ya Serikali.
Mnatakiwa kuwa REGULATE hawa watu. Wanachukuwa pesa za watu and they don’t DELIVER!
 
Kama vile kupandisha ada ilikuwa ni mojawapo ya mapendekezo ya ile tume ya Dr. Mwakyembe, imekuwa haraka sana.

Hawa jamaa ni kama vile wameamua kuwamaliza kijanja wanafunzi kwa kupandisha ada, wakijua wengi itawashinda kulipa hivyo wasiende kujifunza.

Matokeo yake, idadi ndogo itakayobaki, itakuwa rahisi kuichinjia baharini kwenye matokeo, na pasiwepo na malalamiko ya wanafunzi wengi kufeli kama ilivyo sasa.

Sijawahi kuona taasisi iliyopewa uhuru mkubwa wa kujiamulia mambo kama FIFA, hii Law School itakuwa ni FIFA yetu Tanzania.
 
Ama kweli staajabu ya Mussa.

IMG_20221128_083257_507.jpg

Inatia kichefuchefu kuwa ada ya mwaka LST imepandishwa maradufu bila sababu.

Haya ni matokeo ya kuwaacha mabaradhuli kutamalaki na kauli zao kama hizi:

1. Sheria si kwa Kila mtu.
2. Pass mark sheria zipandishwe.

Kwani Kila mtu anaweza kuwa mhandisi, dereva, nurse, mhasibu, rubani, mwalimu nk?

Kwamba pass mark kusoma law zipandishwe? Kwanini pass mark za awaye yote ziwe chini? Kwanini tusizungumzie pass marks za kada zote kupanda?

Kwani sheria ina impact au umuhimu gani wapi chini au juu ya jua?

Ni upumbavu uliopitiliza kuwaacha watu wenye mawazo duni ya kujidhania kuwa wana umuhimu mno katika jamii kuendelea kutukosea adabu kiasi hiki hadharani.

Kwa gharama zipi za uendeshaji ada Law school ya Tanzania kuwa juu kuliko za kusomea hata kada nyingine muhimu zaidi kwa maisha ya binadamu?

Ushahidi wa wazi kuwa tume za maana ni zilizo huru ama za kimataifa kama za Ile ndege ya precision.

Pia ushahidi wa wazi kuwa ya Mwakyembe ni upigaji kama upigaji mwingine.
 
Back
Top Bottom