Law School of Tanzania: Ubabaishaji, uonevu na ubinafsi wa wanataaluma wa sheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Law School of Tanzania: Ubabaishaji, uonevu na ubinafsi wa wanataaluma wa sheria

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Daudi Maginga, Jul 10, 2009.

 1. D

  Daudi Maginga New Member

  #1
  Jul 10, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tarehe 30 mwezi wa sita, Waziri wa katiba na Sheria aliwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2009/2010 bungeni mjini Dodoma. Pamoja na mambo mbalimbali aliyoyaeleza kutoka katika hotuba yake, ilikuwa ni pamoja na kuahidi kuifanyia marekebisho ya sheria inayoanzisha shule ya sheria ya mafunzo kwa vitendo yaani Law School of Tanzania.

  Sheria ya Tanzania Law School Act ya mwaka 2007 ndio iliyoanzisha shule ya sheria kwa vitendo. Madhumuni ya kuanzishwa kwa shule hiyo ilikuwa pamoja na mambo mengine kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya Sheria nchini na hii inajumuisha wale waliosoma nje ya nchi ambao wanatakiwa kwa utaratibu wa sasa kipitia mafunzo kwa vitendo katika shule hiyo ya sheria kabla ya kuingia katika ajira rasmi ya utumishi wa umma na nyanja tofauti tofauti.

  Sheria hiyo ambayo ilianzisha shule ya mafunzo kwa vitendo imekuwa ikilaumiwa na wadau wengi wa sheria kutokana na mfumo wake mbovu tena usioeleweka hata kidogo. Baadhi ya lawama ambazo wadau wengi wa sheria nchini wamekuwa wakitaka kujua ni ubora halisi wa elimu inayotolewa na shule hiyo, mantiki ya elimu yenyewe na ubovu wa sheria inayosimamia shule hiyo.

  Serikali kwa kipindi kirefu sasa imekuwa ikipitisha sheria nyingi zinazowagusa wananchi moja kwa moja pasipo hata kupata maoni ama ushauri wa wadau ili kuboresha sheria husika. Mojawapo ya sheria ambazo zimepitishwa bila kujali maoni ya wadau basi ni hii ya Law School of Tanzania ya mwaka 2007.

  Ukiitazama sheria husika, utakubaliana nami kuwa sheria hiyo ilipitishwa kwa kufuata matakwa ama maoni ya kundi flani la watu waliokubaliana kwa maslahi yao binafsi. Imekuwa ni tabia kwa serikali kuanzisha baadhi ya mifumo katika nchi hii pasipo hata kuwa na maandalizi ya kutosha ama kutokufanya utafiti wa kutosha kutoka kwa wenzetu waliopiga hatua katika nyanja husika.

  Kwa upeo wangu nilionao nilidhani sheria hii ya shule ya mafunzo ya sheria kwa vitendo ingekuwa ni bora zaidi kuliko ya nchi yeyote ile inayotoa mafunzo ya namna hiyo. Kwa mfano kitivo cha sheria cha chuo kikuu cha Dar es Salaam, ndicho kongwe hapa Afrika Mashariki, kilianzishwa mwaka 1954. Hebu tazama ni takribani miaka 45 tangu mafunzo ya sheria yaanze kutolewa nchini, haiingii akilini eti mpaka mwaka 2007 ndipo ilipoanzishwa shule ya sheria kwa vitendo. Hapo unaweza kuona kuwa kulikuwa na muda mrefu wa kuanzisha mfumo huo kwani kulikuwa na maandalizi ya kutosha na si ubabaishaji unaoekana sasa.

  Kwa upande wa Kenya, wao mfumo shule ya sheria kwa vitendo wameanza tangu mwaka 1963. Hivyo basi kwa kuwa wao walikwishaanza muda mrefu, kwetu ingelikuwa sehemu nzuri sana ya kwenda kujifunza wenzetu wamewezaje kufika hapo walipo leo hii. Kwa jambo hili haihitaji hata kuwa profesa ama daktari wa sheria kuweza kulitambua jambo hili. Unaweza kudhani ni utani lakini ndio hali halisi, yapata mwezi wa nne mwaka huu baadhi ya wakufunzi na kaimu mkuu wa shule hiyo walikwenda katika nchi za Kenya na Ghana kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ziara ya mafunzo. Hapa unaweza kuona ubabaishaji iweje wapitishe mfumo ambao unagharimu maisha ya wanafunzi pasipo hata kufanya utafiti kabla ya kutunga sheria husika.

  Hebu tutazame baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza mpaka sasa:

  Mosi, Kwa sasa chini ya sheria hiyo ni lazima (mandatory) kwa kila mhitimu wa shahada ya kwanza ya sheria kupita kwanza katika shule ya sheria kwa vitendo ili aweze kuwa na sifa ya kuajiriwa na mashirika ya umma na yale binafsi. Haiwezekani kwa nchi iliyo na uhaba wa wanasheria kama yetu kuweza kuwa na mfumo kama huu kwa sababu kwa utafiti uliofanyika kwa nchi za Kenya na Uganda wao mfumo wa shule ya sheria kwa vitendo si kwa wahitimu wote bali ni kwa wale wanaotaka kuwa mawakili wa kujitegemea pekee na si kama hapa kwetu.


  Pili, ubora wa mafunzo. Hapa ndipo kichekesho kinapokuja, mafunzo yanayotolewa katika shule hii ya mafunzo hayana ubora na hayana tija kwa wanafunzi kwani hayana tofauti na yale ambayo wamejifunza walipokuwa wanayasoma katika shahada ya kwanza. Tunaamini ya kwamba tunaposema mafunzo kwa vitendo (Practical training) ni vitendo kweli katika eneo husika na sio kuendeleza dhana ile ile ya mafunzo kwa nadharia (Theory). Ninachokiona katika mafunzo haya na mwendelezo ule ule usio na mantiki wa kufanya masomo kuwa magumu na kuweka mizengwe na fitina zisizo na maana. Wakufunzi wamekuwa wakijali maslahi yao binafsi na siyo yale yanayowaweka pale.

  Kwa upande mwingine wakufunzi wa semina wamekuwa ni mzigo usiobebeka na wasio na sifa husika. Walio wengi ni wale ambao ni wanafunzi wanaosomea shahada ya uzamili, wamekuwa hawajui kile wanachokifanya na kuendeleza dhana ya nadharia na ubabe kuliko uwezo halisi wa kisomi.

  Mpaka sasa ni aibu kwa serikali na viongozi wanaosimamia shule hii kiasi kwamba hadi hii leo mafunzo haya yamekuwa hayana tija na kukosa mantiki ya uanzishwaji wake. Mafunzo yamekuwa mzigo kwa serikali. Mzigo kwa maana kwamba mfumo wa utoaji mikopo umekuwa ni tatizo na kulalamikiwa na wanafunzi husika huku viongozi wakishindwa kuwasaidia na kutatua tatizo hilo. Kwa mfano wanafunzi wa awamu ya tatu (third Cohort) wamesimamishwa masomo kutokana na matatizo ya mikopo. Kuna habari kuwa watahamishiwa katika kampasi ya Mlimani pindi watakaporejea, hivi hawa viongozi hawatambui wala kuthamini utu wa wanafunzi? Walio wengi wanatoka mikoani na kabla hawajasimamishwa walikuwa tayari wamekwisha kulipia kodi za pango mahala wanapoishi, je kwa huu mkanganyiko nani anawajibika kwa hasara hii wanayopata wanafunzi hawa? Ni ukweli usiopingika kwamba uanzishwaji wa mafunzo haya ulikuwa ni wa kukurupuka.

  Utaratibu wa kutahini wanafunzi umekuwa ni ule ule wa mitihani, tena ikiwa imeongezewa ugumu wa makusudi kwa lengo la kufelisha wanafunzi. Kwa mfano matokeo ya wanafunzi wa awamu ya kwanza(first cohort) yaliyotoka hivi majuzi yanaonesha zaidi ya asilimia 73 wamefeli masomo yao. Hapa utashangaa ni wanafunzi hao hao waliomaliza shahada zao za kwanza tena kwa alama za juu, leo hii anaonekana si kitu katika shule hii, hilo kwa mwenye akili timamu halimuingii akilini.

  Mgongano wa maslahi ni jambo la tatu linalotia doa mfumo mzima wa mafunzo ya sheria kwa vitendo. Watu wanaounda bodi ya shule hii wamekuwa na mgongano wa maslahi na kazi zao wanazozifanya. Kwa mfano mtu hawezi kuwa mkufunzi wa mafunzo hapo hapo ni mjumbe wa bodi na wakati huo huo ni raisi wa chama cha mawakili Tanzania. Hapo hakuna haki yoyote itakayotolewa kwa misingi ya namna hiyo. Ndio maana bodi hiyo imekuwa ikitoa maamuzi ya ajabu na ubabe usio na weredi hata kidogo na kuendeleza mfumo wa kubeza kila hoja inayotolewa kwa lengo la kufanya maboresho katika shule hiyo.

  Pia haiwezekani Dean wa kitivo cha Sheria cha chuo kikuu cha Dar es Salaam kuwa mjumbe wa kudumu wa shule hiyo ya mafunzo ya sheria kwa vitendo. Iweje awe Dean wa chuo hicho pekee kama hakuna ajenda ya siri iliyojificha? Kwa kuwa wanafunzi wa shule hiyo wanatoka katika vyuo mbalimbali nchini, kwanini Dean wa vyuo vyao wasiwe wajumbe wa bodi ama wao hawahusiki? Pia mbona wakufunzi ni hao hao wa chuo kikuu cha dar es salaam na sio wa vyuo vingine? Hapa kuna tatizo, tena si dogo bali ni kubwa na nimeanza kuamini kuwa wakufunzi wa chuo kikuu cha dar es salaam wamefanya mafunzo hayo kuwa mali yao.

  Ama kwa hakika ni jambo la kushangaza sana kwa shule hii ya mafunzo ya sheria kwa vitendo ambayo imekuwa ikiongozwa kwa ubinafsi na ubabaishaji wa hali ya juu sana na kaimu mkuu wa shule hiyo. Kaimu huyo hashauriki na pia hajawahi kuongea na wanafunzi wake tangu waingie katika shule hiyo na wamekuwa wanashindwa kutoa maoni yao na dukuduku zao kuhusiana na mfumo mzima wa mafunzo wanayopata.

  Ni ukweli usiopingika kuwa kati ya kozi zilizowekewa ugumu, ubinafsi, mizengwe, na umimi wa hali ya juu hapa nchini, basi kozi ya sheria inatia fora. Kwa ujumla kwa yeyote yule ambaye anajitahidi kusoma ili angalau aingie kwenye fani hii anajua jinsi anavyokumbana na vitisho, manyanyaso, uonevu wa waziwazi toka kwa wataaluma wanaofundisha fani hii.

  Kwa kumalizia napenda kutoa ushauri kwa viongozi husika na serikali kwa ujumla. Kwanza wanatakiwa kuelewa kuwa wanaharibu mifumo kwa kukosa ushauri mzuri na kutotaka kufuata maoni ya wadau, hivyo basi ni rai yangu kwamba katika mabadiliko ya sheria hiyo wanapaswa kuileta kwa wadau ili watoe maoni yao kwa ajili ya maboresho yenye tija kwa taifa.

  Kitu cha pili ni kwamba serikali iwe sikivu na iache kuchezea tena kwa makusudi nguvu kazi ya vijana wenye kiu ya kuitumikia nchi yao kwa moyo wote lakini wanakwamishwa kwa mifumo mibovu inayowekwa. Hivyo basi hakuna haja ya kuendelea kung’ang’aniza wahitimu wote wa shahada ya kwanza ya sheria kusoma mafunzo hayo bali iwe kwa wale wachache tu wanaopenda kuwa mawakili wa kujitegemea pekee.

  Jambo la tatu ni kwamba si lazima mafunzo hayo yatolewe Dar es Salaam pekee, naamini ya kwamba mafunzo haya haya kwa nchi za wenzetu kama Australia, wao kila chuo kinakuwa na mafunzo kwa vitendo (Law School). Hivyo basi hapa nchini ingekuwa ni jambo rahisi kuwa na mafunzo haya kwa kila chuo. Hebe tazama vyuo vyote vivavyotoa shahada ya kwanza ya Sheria mahala vilipo kuna mahakama kuu ya Tanzania. Kwa mfano SAUT- Mwanza, RUCO na TUMAINI-Iringa, MZUMBE-Mbeya, Makumira-Arusha, UDSM na TUMAINI tawi la Dar es Salaam. Kwa hakika wanafunzi hao wangepata wasaa mzuri wa kujifunza kwa vitendo.

  Masomo hayaeleweki na yamekuwa ya nadharia mno hivyo kukosa mantiki na kushindwa kukidhi matakwa ya kuanzishwa kwake. Tulitegemea wanafunzi wangekuwa wanafanya mazoezi ya vitendo kwa kufanya kesi za kutengenezwa ili mafunzo yawe ya uhalisia zaidi kuliko hali ya sasa ambapo ni nadharia pekee. Kwa sasa mafunzo hayo hayana tofauti na mfumo wa zamani wa internship. Hivyo basi mfumo wote wa mafunzo utazamwe upya ili mafunzo yaweze kuleta mantiki ya uanzishwaji wake.

  Nikija katika utaratibu wa kutahini wanafunzi, hapa watanzania hasa wakufunzi inabidi kubadilika, tuondokane na utaratibu wa kutahini wanafunzi kwa kutumia kigezo cha mitihani pekee. Katika sheria mwanafunzi anafundishwa jinsi ya kutafuta sheria na si vinginevyo. Kupitia mitihani huwezi kutambua uwezo binafsi wa mwanafunzi husika ila ni kuendeleza mfumo wa kuwakaririsha wanafunzi.

  Kitu kingine cha msingi kuwekwa wazi hapa ni kwamba, wanafunzi wa sheria nchini kwa sasa wamekuwa wakinyanyasika na kukosa mtu wa kuwasemea machungu yao wanayoyapata. Kwa mfano mpaka sasa wanafunzi wa awamu ta tano(fifth Cohort) wamekuwa wakipigwa danadana na hawajui ni lini hasa watajiunga na masomo yao hayo. Kwa kawaida walitakiwa kuingia mwezi wa sita mwanzoni. Kiukweli wamechoka kukaa nyumbani kwani kwa sasa ni mwaka mmoja tangu wamalize shahada yao ya kwanza lakini mpaka sasa hawajui hatima ya maisha yao.

  Ushauri wa bure kwa kaimu mkuu wa shule hii ni kwamba upotoshaji wa taarifa ama tabia ya kukimbia matatizo si suruhisho na ni kinyume cha maadili ya utumishi wa umma. Hivyo basi akae na wanafunzi wake ili kwa pamoja waweze kutatua baadhi ya matatizo yanayojitokeza mara kwa mara.

  Mwisho napenda kumpongeza waziri wa katiba na sheria kwa kuliona tatizo hili na kuahidi kufanya mabadiliko katika sheria ya shule ya mafunzo ya sheria kwa vitendo, naamini huu ni mwanzo tu wa mabadiliko makubwa yanayotarajiwa na wadau wa sheria. Pia napenda kuwaasa wanafunzi wa sheria kote nchini kuamka na kudai haki zao na si kunung’unika moyoni na kujaa woga kwamba wakikosoa watafeli, hiyo ni nidhamu ya woga.

  Haya ni mawazo binafsi tu, naamini ujumbe umefika kwa wahusika.

  Ahsanteni.
   
 2. Mtabiri

  Mtabiri Senior Member

  #2
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Law School students poleni sana.
   
 3. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #3
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Pole sana Maginga,

  Nasikitika kuwa wenzako walikuwa hawakuelewi, walau maelezo yako yamenipa hali halisi ya mambo.

  Inasikitisha, walau ujumbe umefika!
   
 4. m

  macinkus JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2009
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mwaka wa 1963 mwishoni ndio Kenya ilipata uhuru. Mwaka huo ndio chuo kikuu cha Afrika ya Mashariki kilianzishwa kikiwa na vyuo vya Makerere {udaktari} Nairobi {uhandisi} na Dar es Salaam {sheria}. Kwa hiyo isingwezekana Kenya kuwa na mfumo wa shule ya sheria wakati sheria ilikua haifundishwii Nairobi. Chuo kikuu cha Nairobi na vyuo vikuu vingine nchini Kenya vilianza baada ya kuvunjika kwa Shirikisho la Afrika ya Mashariki 1977. Kwa hiyo mfumo wa shule ya sheria labda ulianza baada ya 1977.

  macinkus
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  tatizo la nchi hii ni CUT-AND-PASTE!NA mbaya mbaya mbaya kuliko ni kwamba they copy it without preparations

  poleni sana wanasheria
  INAUMA SANA
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  by the way maginga hongera kwa post yako nzuri sana!

  COUNTING ONE...................
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jul 10, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sina hakika na mfumo wa Kenya kuhusu Law School ila Law School ya Tanzania mambo yake hayaeleweki. Nasikia huyo Acting Principal huwa hataki simu yake ya mkononi wapatiwe wanafunzi. Ukimpigia ya mezani anakujibu kwa mkato. Huyu nako anaonekana ni sehemu ya matatizo ya Law School!
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  sister wangu kapiga hiyo,anakwambia miyeyusho tu!tupo nae kijiweni
   
 9. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #9
  Jul 11, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Daudi Maginga, uliyeleta hii mada,

  Kwanza, umepotosha ulipodai kwamba wahitimu wote watatakiwa kwenda law school, si kweli, na sheria unaijua. Inasema hivi:

  Section 12 ( 3 )
  The Post-graduate Diploma in Legal Practice issued by the School shall, upon the clearance by the Chief Justice, qualify and entitle the holder to practice as an advocate of the High Court and courts subordinate thereto or employment in the public service.


  Kuna vurugu nyingine nyingi tu umeandika hapo. Unalalamikia serikali isivyo sikivu kwa matatizo ulotaja lakini mwishoni unammwagia sifa Waziri wa Sheria kwa kukubali kubadili sheria husika. Kama wameshawasikia, wanabadili sheria, unalalama nini sasa? Hueleweki, unaandika madudu.

  Umesema kwamba inabidi wakufunzi wabadili jinsi ya kutahini wanafunzi kwa vile unadai "...katika sheria mwanafunzi anafundishwa jinsi ya kutafuta sheria na si vinginevyo." La hasha, umepotoka na hujaelewa hata unywele wa maana ya mafunzo ya sheria. Sheria zipo wazi vitabuni, kuweza kuzitafuta sio ufundi wenye umuhimu pekee. Mwanasheria anatakiwa kuchukuliwa anajua sheria, changamoto kubwa ni jinsi ya ku apply hiyo sheria kwenye vithibiti vilivyo mbele yake. Zingatia hilo.

  Umedai walimu wa shule hii ni mzigo kwa serikali. Na shule yenyewe ni mzigo kwa serikali, kwa nini, kwa sababu mfumo wa mikopo yake unalalamikiwa na wanafunzi. Ndugu, kama nyinyi ndio mnalalamika, huo ni mzigo wenu nyinyi, sio wao! Unapo raise grievance weka uzito kwenye kuonyesha kwamba wewe ndio muathirika,
  sio wao serikali, hususan kama hujui wao wameathirika vipi. Au kama pande zote mbili zinaathirika na hawa wanafunzi wa shahada ya uzamili, onyesha ni kwa vipi, how? Inawezekana hawa walimu-wanafunzi ndio cheap labor kwa serikali. I mean, unasema ni mzigo kwa serikali, mzigo, how?

  Unawaambia wakufunzi wenu "nawapa ushauri wa bure..." Kijana, wewe ndio una shida, nyinyi ndio mna msiba na hilo li Law School lenu hilo, inabidi muwashawishi hao wakuu kwa maelezo yenye fikra, yenye heshima, mantiki, wao wameshamaliza shule, hawatakosa usingizi na huo "ushauri wa bure," jenga hoja nyoofu.

  Na ujifunze kiswahili. Angalia unavyoandika:
  Siri iliyojificha? Mfumo umegharimu maisha ya wanafunzi, nani kafa? Utajiwekaje kama mwanasheria hata Kiswahili cha kawaida, cha barabarani tu, hujui, umekulia Bulawayo? Mhitimu wa sheria unasema "suruhisho"?
   
  Last edited: Jul 11, 2009
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Jul 11, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Elezea umeelewaje kifungu cha 12(3) cha Law School of Tanzania Act, 2007!
   
 11. Mpandafarasi

  Mpandafarasi Member

  #11
  Jul 12, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba kutambua mchango wa Bwana Daudi Maginga na hasa kuwa hapo ametumia haki yake ya Kikatiba kutoa maoni binafsi juu ya Law School Tanzania na hivyo basi Siungani na Bwana Dilunga hasa jinsi unavyomshambulia mtoa mada. Lakini pia naheshimu haki yako ya freedom of expression katika hilo. Bwana Dilunga unaposema , kwa mfano"Kama wameshawasikia, wanabadili sheria, unalalama nini sasa? Hueleweki, unaandika madudu."Hapo naona unakosa uzalendo na utu wa kuheshimu maoni ya mtoa mada

  Mkuu Dilunga, Bwana Daudi Maginga hajapotosha anaposema kwamba
  Hiyo Section 12 of the Law School Act, unatoisema hapo ni lazima isomwe pamoja na Section 2 of the Act ambayo inasema, pamoja na mambo mengine kuwa, sheria hiyo itawahusu wale wote waliohitimu shahada za sheria katika vyuo vikuuu nchini na pia nje ya nchi

  Section 2 of the Law School of Tanzania Act 2007 provides that;
  Sasa kwa mujibiu wa Kifungu hiki cha sheria, ni dhahiri kuwa huwezi kufanya kazi Tanzania kama Mwanasheria pasipo kupitia Law School. Hapa naomba kuclarify hilo, Bwana Dilunga wewe ndiye unayepotosha mambo,isome vizuri hiyo Act No 18 of 2007.

  Wanaokuwa exempted from the Law kwa mujibu wa Section 28 of the Act ni wale wote waliohitimu sheria na kupitia mafunzo ya nje kwa vitendo (extenship) at the University hawatatakiwa kujiunga na Law School tena. Na pia wale waliohitimu LLB zao kabla ya tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria hiyo ya Law School. Nje ya hapo huwezi fanya kazi kama mwanasheria pasipo kupitia Law School ni kinyume na sheria.

  Kuhusu ni namna gani maisha ya hao wahitimu wa Sheria nchini yanagharimika, inategemea na mtizamo wa mtu. Lakini kimantiki ni dhahiri kuwa kumuharibia mtu maisha si lazima umkate kichwa na kufanya actual killing, hata kumuharibia mazingira ya kuishi au kumuharibia mtu pale ambapo angeweza kujipatia riziki nalo pia lichukuliwe na kutambulika kuwa linagharimu maisha ya mtu huyo. Nitoe tu mfano hapa; Kuna LLB graduates waliohitimu masomo yao mwaka 2007 June hao ndio walioingia Law School first cohort na hao hivi tunavyoongea hawaja maliza mchakato wa Law shool mpaka sasa. Matokeo yao yametoka mwezi ulipoita, pamoja na kuwa wengi wao hawakupass vema, hata hao wachache, less than 30 waliopita hawajawa confirmed yet mpaka hapo Law School itakapo amua kufanya hivyo, when?No body knows! Hivyo fikiria mtu aliyehitimu Shahada yake June 2007 mpaka lend of 2009 yupo mtaani na haruhusiwi kuajiriwa kama Lawyer nchini na hajui ni lini exactly atakamilisha.

  So generally, kuhusu Ubabaishaji Law School, hilo halina upinzani, ni dhahiri na ni kweli kuwa serikali yetu haikufanya preliminary preparations kabla ya kuanzisha Tanzania Law School. Kwa mfano hadi sasa Law School haina majengo yake na imeishia kujiegesha pale UDSM Faculty of Law. Ikumbukwe kuwa Faculty of Law UDSM yenyewe pekee na wanafunzi wa undergraduate tu hapatoshi, hawana enough rooms hasa lecture theatres now how come wanahost Law School?

  Kuna ubabaishaji mwingi, upon a ni wakutosha kukithiri. Hakuna haja ya kuitetea Serikali hapo.

  Lakini jambo la msingi hapo niungane na Mr Dilunga kuwa hao wanafunzi wa hiyo Law School hawajasimama imara kudai what they want the way they want it.
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Nampongeza Daudi sana kwa kuliweka wazi suala zima sasa kama kuna uozo,ujinga ujinga,mafunzo hayaeleweki watu wame binafsisha kitengo na mafunzo hiyo haikubaliki....inakuwa haina maana tena.....lengo zuri utekelezaji usanii kibao....hongera uliemsha wengi usingizi wa uoga.....
   
 13. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ha ha ha Dilunga nimekusoma mkuu... ila umekaa kaa kama ndio hao (waalimu) ambao bwana Daudi analalamikia.. though umesaidia kuweka mambo sawa.
   
 14. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana. lakini naona njia sahihi ni kufungua kesi na kudai haki zenu badala ya kupita mkilalama.

  Tunafahamu kuwa kupita kwenu hapo Law sch ni kwa mujibu wa sheria. Na lazima tujue kuwa kila sheria ni lazima iwe na mipaka yake.

  sasa mna haki kabisa kudai ukomo wa mwanafunzi ndani ya Law sch. Mfano hata JKT iliundwa kwa mujibu wa sheria kwa wanafunzi wote wa diploma, form six na certificate . lakini sheria ilibainisha wazi kuwa kwa wanafunzi hawa kukaa JKT ni kwa siku 365 tu kama hatakuwa ana matatizo yoyote ya utovu wa nidhamu.
  Poleni sana


  Nasriyah
   
 15. A

  ASSEY New Member

  #15
  Feb 27, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamania mbona hatubadiliki na kuachana na hii tabia ya kulaumu na kulalamika bila kutoa jawabu au ufumbuzi? mimi nilitarajia watu wa JF kwakua nimkusanyiko wa "great thinkers" wangekua watoa masuluisho ya mambo yanayoisumbua jamii,lahasha huku kumekua ni malalamiko na lawama tu. mtu anadai Law school of Tanzania imejaa ubabaishaji, uonevu na ubinafsi nikweli kabisa laikini mimi nashindwa kuelewa huo u-great thinker wako upo wapi hashwa? labda ni kwenye kukosoa na kulalamika! acha ujinga na uvivu wa kufikiri toa suluisho hayo matatizo wote tunayajua vipi bwana ubongo umeganda?
  You need to become an option-thinker a creative and a possibilty thinker. A creative and a possibilty thinker are people who constantly search for options and new ways to get things done. if one way doesnt work they try another until they win. You also need to open up your own way of thinkin b'se you limit yourself by the way you think you must learn to think outside of your limitations
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Unataka suluhisho? Kill that "Law School" bs and either incorporate it in the University curriculum, or emphasize a bar system.

  Law is not Chemistry kusema utataka practical, na si kila mtu anayesoma law anataka ku practise law, kuna watu wana degree za journalism na washaji establish katika profession hiyo na wanataka soma law kujimarisha katika uelewa wao wa sheria tu, sasa mtu kama huyu akitaka kwenda kufanya kazi Daily News kwa credential zake za lawyer lakini katika profession ya Journalism mtataka aende hicho ki "Law School" kama anataka ku practise law?
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,546
  Trophy Points: 280
  Daudi Maginga, anastahili pongezi na encouragement, haswa ukizingatia ndio posti yake ya kwanza, na amezama that deep.

  Ni kweli hii sheria ya law school ni kitanzi, infact ni msumeno unaokata mbele na nyuma ama upanga wa makali kuwili.

  Nijuavyo mimi, hii law school inaendeshewa pale UDSM kama mradi tuu wa ulaji mpaka majengo yao yaliyoko mabibo external yakamilike.

  Sheria inalazimisha kupitia law school kwa kila mhitimu wa LLB. Tuna vyuo vitatu vya LLB Tanzania, UD, Mzumbe na Tumaini, kila mwaka tunazalisha LLB 1000. Uwezo wa law school ni less than half. Hivyo kuwanyima haki hawa wengine wote wanaokosa nafasi law school.

  Msumari ni kwa sisi wengine wote tuliosoma sheria zamani kabla ya sheria ya law school, hatukupetition kuwa mawakili eti nasi haturuhusiwi kupractise uwakili mpaka nasi tupite law school!. Majaji wengi wakishastaafu ndio wana petition na kuwa mawakili, hebu tusubiri Jaji Agostino Ramadhani anastaafu Desemba hii, tuone akija darasana kusoma ili awe wakili!.

  Ilipoanza walisema wahitimu wa law school wanakuwa mawakili moja kwa moja, leo wako cohot ya 3 na hakuna hata mmoja wao aliyepata huo uwakili!. Nakubaliana na Maginga, something is seriously wrong somewhere here!.

  Naamini, wanasheria wakiichalenge hii sheria mahakamani, inakuwa scripped off there and then, outright!.

  Asante Maginga, karibu JF.
   
 18. Yohana Kilimba

  Yohana Kilimba JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2016
  Joined: Dec 25, 2012
  Messages: 8,132
  Likes Received: 5,211
  Trophy Points: 280
  Hivi hii kadhia iliishia wapi?
   
Loading...