Law school of Tanzania Mwaka huu ya tia fora | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Law school of Tanzania Mwaka huu ya tia fora

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by chumvichumvi, Mar 17, 2012.

 1. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Law school ya Tanzania ya tia fora mwaka huu baada ya kuchagua wanafunzi wengi zaidi kuliko miaka iliyopita kama ilivyokuwa ada huko miaka ya nyuma. Ni leo jioni majina ya wanafunzia waliochaguliwa na chuo hicho yametolewa katika mfululizo wa batch 3, ya kwanza ikiwa inaingia mwezi april ambayo hiyo ni batch ya kumi na moja(11)na nyingine ikiwa inaingia mwezi wa 6 batch ya kumi na mbili(12) na kumi na tatu(13) kwa ufafanuzi zaidi tembelea website ya chuo hicho ambayo ni www.lst.ac.tz
   
 2. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  ni vizuri: huitaji bado ni mkubwa.
   
 3. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Doing some PR sir?
   
 4. mka

  mka JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nendeni mkasome taifa bado lina uhitaji wa mawakili.
   
 5. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  lw scul uchupiiiii tu mradi wa watu
   
 6. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  from my heart bado cjaona umuhimu wa wanasheria nchi hii. Mikataba kibao mibovu inasainiwa na ina vifungu kibao vya kisheria na kila ofisi ina mwanasheria, mswada wa sheria ya katiba umepitishwa kishabiki na mabadiliko mengine ya sheria hufanywa kisiasa na wao wapo. Katiba ya nchi inaendeshwa na mtu anavyotaka mfano suala la uraia wa sioi, uraia wa nchi mbili watu wanao na ni viongozi na katiba haitambui hilo. Watu wanabambikiwa kesi wakiwa mahakamani na wanafungwa. Hayo yote hawayaoni,mpaka sie tuliosoma bachelor of mathematics tupige kelele majukwaani ndo washtuke. Kuna wengine wamesoma na wanategemewa na jamii lakini ukiwasikiliza argument zao kwenye mambo ya kisheria hata mtoto wa first year medicine anamshinda. Wanatetea matumbo yao tu na hawasimamii ukweli mfano werema, tendwa,lubuva, kabudi nk.
   
 7. mka

  mka JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu salam, naomba nitofauti nawe kidogo. Japo ni kweli kuwa taifa lina wanasheria wasio kuwa na dhamira safi na maadili ila bado twahitaji wanasheria. Nina sema hivi kwa sababu, mfano kumbuka suala la uvunjwaji wa haki za binadamu nyamuma ni wanasheria(LHRC na wengineo) waliolivalia njuga hadi likafahamika na kuipeleka serikali mahakamani. Pia kuhusu katiba Chama cha Wanasheria Tanzania Bara (TLS) kwa miaka mingi kimekuwa kikidai mabadiliko ya katiba hii ya sasa. Pia kabla na baada ya muswada wa mabadiliko ya katiba TLS kilitoa waraka kupinga muswada ule 'mbovu', pia walifungua kesi mahakamani kuupinga muswada huo

  Kuhusu kupitishwa kwa saheria mbovu mkuu waweza laumu wanasheria lakini nadhani watambua kuwa muswada huwa wapitishwa bungeni na kusainiwa na Rais(hiyo mihimili miwili sio wanasheria) ni wanasiasa mara nyingi hawana elimu ya sheria. Umeshajiuliza ni kwanini sheria mbovu zinapitishwa bungeni? Je ni sababu ya wanasheria? Kwangu mimi sababu kubwa ni wananchi, sisi wananchi ndio tunaowachagua viongozi wabovu na walio walarushwa, wao wanatuletea sheria mbovu. Wadhani tukichagua wabunge safi tutapata sheria mbovu? Kumbuka kuwa jamii isiyofikiria vizuri, jamii inayokumbatia viongozi wabovu na kuchagua walarushwa itatoa viongozi wabovu watao tunga sheria mbovu. Kinyume chake kama jamii yetu ikiwa na maadili itachagua viongozi safi watakao tunga sheria nzuri wanasheria watalazimika kutumia sheria nzuri.

  Ninakubali kuwa kuna wanasheria wasio na maadili, ila nao ni zao la jamii isiyo na maadili inayowakumbatia. Je hatuna walimu, wahandisi, madaktari n.k wasio na maadili? Kuhusu matumizi ya sheria katika mikataba, japo ni kweli kuwa wanasheria ndio wanaandaa hiyo mikataba, kumbuka kuwa wanaandaa kwa kufuata dondoo za mwajili wao serikali na kuangalia sheria inasemaje, inasikitisha kuona kuwa mikataba mingi 'mibovu' haijavunja sheria za nchi japo kimaadili si mizuri, lakini kisheria, sheria yeyote ni halali mpaka pale itakapofutwa. Mfano Sheria zetu hazisemi mikataba ya biashara kati ya serikali na mwekezaji iingiwaje na hazitoi uwazi katika hilo.

  Wanasheria wanahitajika kuwa wengi maana hii itawafanya wasambae sehemu nyingi na huenda ikashusha hata gharama. Ni ukweli usiopingika kuwa wananchi wengi wanaonewa kwa sababu ya kukosa mawakili, umesema kuhusu watu kubambikiwa kesi, kumbuka ukiwa na mwanasheria ni rahisi kushinda kesi uliyobambikiwa kuliko mtu asiye na wakili.

  Kiujumla kwangu mimi japo ni kweli wanasheria (baadhi) hawana uzalendo na maadili, nao ni zao la jamii iliyokosa maadili na iliyokosa uzalendo.
   
 8. k

  kelvinkipeta Senior Member

  #8
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  wewe UNAWEZA KUNAMBIA N KITENGO GANI KIMEKAMILIKA/hao madaktari au.naona umekurupuka jombaa
   
 9. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  vipi kuhus majengo yanayodondoka kama lile la kisutu na chang'ombe house, hii nchi kila kona mbovu. wabunge wenu mnaowapitisha wanafanya mambo kishabiki, hata wanasheria wakiwaambia muswada huo unatatizo wao wapo kishabiki.
  Jua kutofautisha kati proffessionalism na breach of code of conduct.
   
 10. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  hata kama ni mradi wa m2 hamna means nyingine zaidi ya kwenda kama kweli unataka uadvocate otherwise utaendelea kuteseka mtaani as kila ofisi ukiingia wanakuuliza kuhusu law xul otherwise underpayment itakuhusu
   
 11. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  unajua kuna swala moja naic tunachanganya au tunashindwa kutofautisha kati ya siasa na sheria nikiwa namaana ya kwamba m2 anaweza akawa mwanasiasa aliyebahatika ku-practice sheria sasa anapokuwa mwana siasa anasahau nini sheria inataka au mwanasheria ni nani na ikatokea akafanya vyote viwili kwa wakati m1 vyote huwa vinamshinda ndio mambo hayo unayoyasema kutokuwepo kwa uadilifu as its well know u cant serve 2 masters @ a time mmoja lazima aende mfano hai ni Tindu Lissu yule jamaa ana-practice uwanasheria bungeni na si siasa ndio maana kwenye miswada ya sheria huwa yuko moto na straight
  ni hayo 2
   
 12. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  sasa swala la magorofa na nyumba kudondoka ni swala la wakandarasi ndugu yangu
   
 13. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Tanzania ina wanasheria wengine wamesoma Havard lakini bure. Mikataba kwenye madini ovyo, wameruhusu mpaka wanasiasa wawe kwenye kamati za maadili za mahakama. Tena wengine washawahi kuwa majaji,sasa kama huku hivije kwenye ujaji ilikuwaje
   
 14. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  ingewezekana kila raia wa TZ angekuwa na mwanasheria wake lakini mawakili ni wachache na uhitaji ni mkubwa wangetoa hata batch 5 ni sawa tu
   
 15. k

  kanganyoro Senior Member

  #15
  Mar 27, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kasomeni muijenge nchi yenu.
   
 16. n

  nyariamani Member

  #16
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  No research no right talk. Kaa chini fanya uchunguzi kwanza ukishaelewa/ukishapata ufahamu wa suala unalotaka kulizungumzia ndiyo ulizungumzie kwa jamii.
   
 17. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  mkuu nimeshindwa kukugongea like kama mia tano hivi mka
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. kimpango

  kimpango JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 515
  Likes Received: 382
  Trophy Points: 80
  ni sawa lakini kuiweka dar peke yake inaumiza watanzania wengine especially wale waliomaliza llb kutoka mikoani pia inawabagua watanzania kwani bodi ya mkopo haihusiki huko na wengi hatuna uwezo wa kujisomesha
   
 19. vigilia

  vigilia Member

  #19
  Jan 23, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kasahau hata madaktari wanakata kichwa badala ya mguu, na engineers wanabomoa gorofa kwa kuanza chini badala ya juu. Hizo ni challenges ambazo ziko katika kila fani. Lakini huwezi sema yaani huoni kabisa umuhimu wa wanasheria. Uhukumiwe kifo halafu mwanasheria akusemee mahakamani ndio utatambua umuhimu wake.
   
 20. D

  Dingi mchafu Member

  #20
  Jan 25, 2013
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo sio wingi wa watu je watafaulu na kuwa mawakili?ukweli ni kuwa input na output hazishabiani ata kidg..mfano cohort ya 10 waliingia watu zaidi ya 240 waliofaulu first sitting ni 30 tu.Ushauri wangu ni kuwa dnt go there unless una mda vizuri wa kusoma otherwise watakula kichwa cjawai ona shule ngumu km ile
   
Loading...