Law school, Kitivo cha sheria (UDSM) na ubinafsi wa wanataaluma wa sheria

masungan

New Member
Mar 28, 2008
1
4
Law school, Kitivo cha sheria (UDSM) na ubinafsi wa wanataaluma wa sheria


Kati ya fani zilizowekewa ugumu, ubinafsi, mizengwe, na umimi wa hali ya juu Tanzania, basi fani ya sheria inatia fora na pengine imefanywa kuwa ni mali ya wale walioko kwenye soko kwa sasa pekee. Wanaojiita wanasheria kwa sasa wanahakikisha wanaweka masharti magumu ambayo yatawahakikishia wanaendeleza umangimeza na Umgabe wa kumiliki fani hii kana kwamba imekuawa mali yao.

Nasema hivyo kwa sababu kwa yeyote yule ambaye anajitahidi kusoma ili angalau aingie kwenye fani hii anajua jinsi anavyokumbana na vitisho, manyanyaso, uonevu wa waziwazi toka kwa wataaluma wanaofundisha fani hii katika vyuo vikuu hapa nchini na hili kwa wanafunzi wa fani hii kwa chuo kikuu cha Dar es salaam kitivo cha sheria wanalijua kwani kwao hayo ni haki yao ya msingi kukutana nayo.

Tulitarajia wanataaluma wanaofundisha fani hii katika kitivo hiki wangekuwa wa kwanza kujali, kusimamia, kuendesha na kufanya mambo kufuata taratibu na kuwa mfano kwa vitivo vingine lakini imekuwa kinyume kabisa na matazamio na matamanio ya jamii.

Taaluma hii hutolewa kwa vitisho, manyanyaso, uonevu na kwa kiwango cha dhahania tu maana hakuna mafunzo kwa vitendo kwa miaka minne. Ni vigumu kuamini hili na haingii akilini kwa mtu yeyote yule mwenye uelewa mdogo japo wa elimu ya msingi kuwa mwanafunzi wa fani hii toka chuo kikuu cha Dar es salaam hafanyi mafunzo kwa vitendo kwa muda wote wa miaka minne.

Wengi tunajuta kuchukua fani hii kwenye kitivo hiki kwani tumejikuta kwenye wakati mgumu wa kuingia kwenye soko la ajira lenye ushindani wa hali ya juu.Mathalani tungelijua ubabe huu tungesomea fani zingine ili tupate elimu stahili, yenye kujengwa kwenye uhalisia wa mambo (theory and practical trainings) vitu ambavyo vinatofautisha elimu ya vyuo vikuu na elimu ya shule za upili, tupata kile kitakiwacho katika soko siyo majivuno ya ukongwe wa kitivo na pengine tukamilishe ndoto zetu za kuwa wataalamu na kuona matunda ya mlolongo wa kusotea elimu ambayo hapa nyumbani ni bahati kuipata.

Ni uwazi usiopingika kuwa uanzishaji wa LAW SCHOOL Tanzania umetokana na juhudi za makusudi za kitivo hiki ili azma yake itimie, na kweli hili limefanikiwa japo kwa kinadharia zaidi. Sheria ya uanzishaji wa LAW SCHOOL ni moja kati ya sheria mbovu, kandamizi, baguzi, onevu na kwakuwa waasisi wa wazo hili ni kitivo cha sheria cha chuo kikuu cha Dar es salaam, ilikuwa ni lazima iakisi yale yale ambayo wanafunzi wa kitivo cha sheria wanaumizwa nayo siku zote.

Sheria hii inatamka wazi kuwa Dean wa kitivo hiki atakuwa mjumbe wa kudumu katika bodi ya LAW SCHOOL, kwanini asiwe Dean wa Mzumbe, SAUT, RUCO n.k?.Sheria hii inatutaka tujilipie ada, (shilingi milioni 1.6), tujitegemee malazi na chakula pamoja na mambo mengineyo. Hivi waliotunga sheria hii ni watu wanaofikiri vizuri kweli au ni umimi na kutaka kubaki wao na wenye uwezo wa kifedha tu katika fani hii? Ni lini wanafunzi hao hao waliokuwa wanagharamiwa masomo na BODI YA MKONO ya nadharia katika kitivo hiki wamekuwa na uwezo wa kulipia na kugharamia gharama za LAW SCHOOL? Je fani ya sheria ni kwa watoto wa matajiri tu? Kama ni hivyo tangazeni basi ili watoto wa wafinyanzi tusije mbaki peke yenu. Je fani hii ni kwa ajli ya watokao Dar es salaam tu kwani wao malazi hayawagusi? Tutangazieni basi mapema ili sisi wa LONGIDO, OLDONYO LENGAI, NKUNDI, MAKETE, MGANDU, NKASI n.k tusije ili wabaki wateule wa jijini na wenye nazo.

Ili kuendeleza uonevu, sheria hii inaendelea kusema kwamba yeyote ambaye hajapitia shule hii (ambayo itakuwa chini ya kitivo cha sheria UDSM, kitivo kikongwe,kizee kuliko vyote Tanzania) hawezi kuajiriwa au kufanya kazi katika ASASI ZA SERIKALI, je mtoto wa wenzangu na mimi tuliojitumbukiza katika fani hii ya wateule tutaenda wapi?kulima?------hapana hatujasomea kilimo kwani fani hiyo iko SUA, kufinyanga?-----hapana hatukusoma FPA, kufundisha?----------hapana labda Prof. Mkandala atuonee huruma tufanye mafunzo ya muda mfupi (Crush program). Jibu ni rahisi masikini na mwanae na wateule na mali zao.

Tunajua wazi kuwa kitivo hiki kwa kawaida hakiko tayari kusikiliza, hakuna uhuru wa kusema, au ukisema unakuwa muhuni na lazima ukubali kufeli na hakuna anayepewa uhru ya kujitetea.Labda nitoe mifano michache ya mambo yalivyo katika kitivo hiki kikongwe kuliko vyote Tanzania,

Mosi, kutokuwepo kwa haki ya kusikilizwa kwa wanafunzi. DEAN hayupo tayari kuongea na wanafunzi moja kwa moja, hata kwenye vikao vilivyowekwa kisheria na chuo( Faculty baraza) kama wafanyavyo DEANS wa vitivo vingine.
Kama utasikilizwa aidha hutapewa nafasi ya kutosha au utaitwa muhuni unayetaka kuchochea vurugu au unafanywa mfano kwa kuhakikishiwa nafasi ya kufeli mara moja.Mara zote mawazo ya wanafunzi yanachukuliwa kamw uchochezi na au yasiyo na tija na pengine hayana msingi mpaka yaandikiwe propasal eti ndiyo yafikiriwe.

Pili, haki ya kupata kozi weksi kabla ya kufanya U.E. Prospectus inatamka wazi kuwa kila mwannafunzi ni lazima apate matokeo ya kazi zake za tests kabla hajafanya mtihani lakini hili halifinyi kazi na halipo kwa kitivo hiki. Sababu kubwa ya kutokufanya hivyo inasadikika ni kuwa na waalimu WACHACHE hivyo ni vigumu kusaisha kazi na kutoa matokeo kwa muda stahiki. Lakini ni waalimu haohao ndiyo walioandika propasal ya kuanzisha, kuiendesha na kuisimamia LAW SCHOOL. Je idadi ya waalimu ya kitivo hiki ambao hata matokeo ya U.E kuyatoa inahitaji wanafunzi watishie kugoma ndipo yatolewe idadi imeongezeka? Au tuandike propasal za kuomba matokeo kama ilivyo ada yenu ya kutaka kila kitu tukiombe kwa staili hii?

Tunashukuru kwa kufanikiwa kuandaa PROPASAL ya kuanzisha LAW SCHOOL, kwani ni wazi mmepata AJIRA na mtakuwa mnapata mishahara minono tena bila kusotea sana maana mtafanya kazi mbili kwa pamoja katika mazingira yalayale,yaani utatoka YOMBO 1 kwa ajili ya LW? Alafu mara moja unaingia kwenye mradi wenu wa kuingiza pesa kwa njia yenu ya KIVULI cha LAW SCHOOL

Swali hapa inakuwaje watu ambao hawaendeshi hata semina katika kitivo hiki kwa kisingizio cha uchache wao wanakuwa na uwezo wa kuwa na vipindi SEHEMU NYINGINE na ndiyo MADINI wa LAW SCHOOL? Huu ni UFISADI tena mbovu kuliko ule wa EPA na RICHMOND.Kitu gani kinazuia matokeo kutoka kama si kuyapika? Ni wangapi wamerudia au wamefukuzwa kinyama kwa kukosa kozi weks ambazo kama zingekuwa zinatolewa mapema tatizo la kukosekana lingetatuliwa? Ni wangapi wameondoka kwa makosa ya kawaida ambayo kama matokeo na kozi weksi zingekuwa zinatolewa mapema wangekuwepo? Angalia kama kosa hili la mwanafunzi kuandika namba yake ya mtihani 162 badala ya 152 amefukuzwa kwa kisingizio cha kutokufanya mitihani mitatu? Ni kweli hili ni kosa lakini kwakuwa mwenye namba 162 alionekana kufanya mitihani mingi lakini mwandiko wa huyu dada ailyestahili kuandika namba yake 152 si zilionekana na mwenye namba ya mtihani 162 alipatikana kwa urahisi kipi kilichosababisha dada huyu atimuliwe kinyama tena miezi sita baada ya tatizo hili kama si uonevu, unyanyasaji na umimi?

Nafikiri ni wakati muafaka kwa makamu mkuu wa UDSM kutumia staili ya Rais na awatake Waalimu wake walioandaa PROPASAL na kufanikiwa kujiajiri LAW SCHOOL wachague moja kati ya kutumikia chuo au waende kwenye AJIRA WALIOJIANDALIA ya LAW SCHOOL kwani kuendelea na AJIRA hizi mbil ni ukiukwaji wa maadili. Iweje mwalimu huyu ashindwe kutoa semina kwa kisingizio cha uwingi wa wanafunzi alafu aweze kufundisha sehumu nyingine? UFISADI HUU ni wizi wa mali ya umma.

Tuna kila sababu ya kuamini kuwa law school ni mradi wa baadhi ya waaalimu wa FOL na ndiyo maana wao wamejiweka katika nafasi ya kuwa WAJUMBE wa kudumu katika LAW SCHHOOL,wameandaa silabus, wamejiwekea iwe katika majengo ya udsm, ofisi za kiyivo ziwe ndiyo ofisi za LAW SHOOL, wao ndiyo waalimu hapo, ndiyo viongozi wakuu na ndiyo hao hao waliohusika kudrafti sheria hii mbovu,ovu, kandamizi na ya kujitafutia ajira kwa njia ya kuwaumiza wanafunzi wanaohitaji SOCIAL ASSISTANCE? Kwa nini si DEAN wa Mzumbe, kwanini Mzumbe wasiwe HOST INSTITUTION, kwanini Mzumbe, Tumaini, SAUT n.k PROSPECTUS zao hazitamki uwepo wa hii LAW SCHOOL?

Inaendelea wiki ijayo-----------------------------------------------


Mwandishi ni mwanafunzi wa FOL na Mpinga Ufisadi kama huu.



 
I feel your pain..nina ndugu yangu hapo amelalamika sana kuusu law school...pia kuna issue nyingine ya kuwa umefanya 16 different modules (including Arbitration na Private international law) ili uweze kukubalika ku join lasi ivyo wanakunyima certificate mwisho wa mwaka...naomba info if this is true or not!

Im planning on joining the law next yr...je kwasisi wenye Law Degree kutoka nje ya nchi...kuna vikwazo vyoyote??

Ntashukuru msaada wako...
 
Pole sana ndg yangu masungani,that is the faculty of law at UDSM.ambacho naweza kukushauri ni uvumilivu maana hapo kuna vichwa vibovu na tena vinakatisha tamaa eg Kabu',luog,mchom,jes,msha,yupo na muhaya mmoja nimemsahau yaani hivi vichwa vinaweza vikakuletea frustration mpaka ukaamua kuacha chuo kwa ajili ya hawa wajinga wachache.

wewe komaa nao mpaka uondoke na degree yako ili waisome namba.Mimi nilipita hapo miaka ya nyuma hivyo ulichokisema huo ndio ukweli.He nilimsahau frustrator mwingine Mr.Mvung'yaaaaaani ni problem mwanawane.
 
Pole sana ndg yangu masungani,that is the faculty of law at UDSM.ambacho naweza kukushauri ni uvumilivu maana hapo kuna vichwa vibovu na tena vinakatisha tamaa eg Kabu',luog,mchom,jes,msha,yupo na muhaya mmoja nimemsahau yaani hivi vichwa vinaweza vikakuletea frustration mpaka ukaamua kuacha chuo kwa ajili ya hawa wajinga wachache.

wewe komaa nao mpaka uondoke na degree yako ili waisome namba.Mimi nilipita hapo miaka ya nyuma hivyo ulichokisema huo ndio ukweli.He nilimsahau frustrator mwingine Mr.Mvung'yaaaaaani ni problem mwanawane.


HATA MIMI NILIPITA MIAKA YA NYUMA, NDIYO MAANA KILA NIONGEAPO WATU HUONA HUWA NINAKIPONDA, ILA HALI NDIVYO ILIVYO.

KWA TAARIFA , HIYO LAW SCHOOL ILIKUWA IWE MONOPOLIZED NA HAO WASHENZI ILA SASA ANGALAU KUNA VIPENGELE VIMEKUWA RELEASED. NA INASEMEKANA SOME OF THE QUALIFICATIONS ZA COURSE MTU INABIDI AWE AMECHUKUA.

ILA MZUMBE INAONAONEKANA QUALIFICATIONS ZOTE ZIPO, SASA SIJUI WA SISI UDSM ITAKUWAJE.

TUENDELEE KUPIGA KELELE TU LABDA WATASIKIA
 
mchango wangu na mawazo yangu ktk hii thread ni huu.......SOMENI VIZURI THREAD YA...."UDSM CHANZO CHA MFUBAO WA ELIMU TANZANIA......"
 
I feel your pain..nina ndugu yangu hapo amelalamika sana kuusu law school...pia kuna issue nyingine ya kuwa umefanya 16 different modules (including Arbitration na Private international law) ili uweze kukubalika ku join lasi ivyo wanakunyima certificate mwisho wa mwaka...naomba info if this is true or not!

Im planning on joining the law next yr...je kwasisi wenye Law Degree kutoka nje ya nchi...kuna vikwazo vyoyote??

Ntashukuru msaada wako...

HIVI VIPINDI ULIVYOVITAJA NI KUWA KWA INTAKE ZA MWAKA HUU WATAHARMONIZE ILA MIAKA INAYOKUJA ITAKUWA NI NGUMU.
 
I feel your pain..nina ndugu yangu hapo amelalamika sana kuusu law school...pia kuna issue nyingine ya kuwa umefanya 16 different modules (including Arbitration na Private international law) ili uweze kukubalika ku join lasi ivyo wanakunyima certificate mwisho wa mwaka...naomba info if this is true or not!

Im planning on joining the law next yr...je kwasisi wenye Law Degree kutoka nje ya nchi...kuna vikwazo vyoyote??

Ntashukuru msaada wako...


KWA MWAKA HUU WATAHARMONIZE ILA MIAKA IJAYO ITAKUWA COMPULSORY. ILA KUNA ULAZIMA WA VYUO VYOTE KUWA NA MITAALA INAYOFANANA.

VYUO VILIVYOKUTWA KUWA NA MTAALA UNAOENDANA NA REQUIREMENTS ZA SCHOOL OF LAW NI MZUMBE TU.
 
KWA MWAKA HUU WATAHARMONIZE ILA MIAKA IJAYO ITAKUWA COMPULSORY. ILA KUNA ULAZIMA WA VYUO VYOTE KUWA NA MITAALA INAYOFANANA.

VYUO VILIVYOKUTWA KUWA NA MTAALA UNAOENDANA NA REQUIREMENTS ZA SCHOOL OF LAW NI MZUMBE TU.

Samahani Mtaala ndo? kiswahili changu sio fasaha sana
Syllabus??

Anywho all i knw huku UK 2nd and 3rd yr mwanafunzi hunakuwa free kuchagua 4 modules of your choice...sasa kama wanaweka system hii ndo maana yake watu walio changua modules zao hawataweza ruhusiwa kupita law school?
 
Samahani Mtaala ndo? kiswahili changu sio fasaha sana
Syllabus??

Anywho all i knw huku UK 2nd and 3rd yr mwanafunzi hunakuwa free kuchagua 4 modules of your choice...sasa kama wanaweka system hii ndo maana yake watu walio changua modules zao hawataweza ruhusiwa kupita law school?

asante kaka,

vipindi 16 vimefanywa compulsory kwa yeyote kuingia school of law kwa tanzania.

sasa ikaja kasheshe kuwa baadhi ya vipindi kama private international law ilikuwa ni optional kwa UDSM, wakati Mzumbe na Tumaini ilikuwa compulsory, i mean UDSM mtu angeweza kugraduate bila kuisoma.

school of law entrance ikahitaji kila mtu atakayejiunga na law school lazima awe amechukua vipindi vyote ambako unakuta UDSM graduate for example hakusoma kwa sababu ilikuwa ni option. kwa mwaka huu labda na mwaka kesho imesemwa kuwa masharti hayo yatakuwa released ila vyuo vya TZ inabidi viharmonize mitaala yao yes 'sylabus' ili kuwepo na uwiano. sasa kwa wale wa nchi za nje labda inabidi kuwepo na ufuatiliaji wa karibu ili kama unafanya option basi uwe kwenye ambit ya school of law requirements.

vyuo vyote tz vilikuwa kavina qualifications kwa wanafunzi wao isipokuwa Mzumbe. ndio maana ikawepo ulazima wa kutokuwa strict kwa mwaka huo as far as
courses is concerned.
 
ni kweli kabisa mimi binafsi ninasikitishwa na kitivo hiki wanafunzi hatutendewi haki kila kitu mizengwe tofauti na vitivo vingine hapa UDSM,mikwara kila kukicha.
 
Naombeni muanike hiyo ratiba,ili wadau wailelewe kabisa wasujekutana na hayo majanga tafadhali
 
Tukisema UDSM ni chanzo cha kuanguka kwa elimi hapa nchini watu huwa hawaelewi kabisa.
Post graduate diploma in legal practice vyuo kama SAUT, MZUMBE na BAGAMOYO kwa sasa vinaweza kutoa vizuri kabisa.

Lazima tukubali kama hii shule ya Sheria ya Mlimani ni matatizo makubwa,
Haiwezekani kuwe na wanasheria zaidi ya 2000 wanaomaliza degree halafu 100 tu ndiyo wanamaliza hao wengine wasubiri miaka mingine. Hii si sawa hata kidogo.

Mosi, hili linaharibia watu soko la ajira.
Watoto wanasubiri mtaani mafisadi wachache ndiyo wawaamulie waendelee na fani yao au lah.

Huwezi kusema kila anayeingia Law School ni competent na kila anayeshindwa ni Incompetent.
Hapa lazima vyuo vyenye uwezo viruhusiwe kutoa Law School.

Pili, kama hilo la kwanza litakuwa ni gumu basi BODI ya LAW SCHOOL ni lazima ipanguliwe.

Chuo kikuu cha Mlimani kisiwe na monopoly kabisa over the LAW SCHOOL OF TANZANIA.
Hapa nashauri JUDICIARY ihusishwe moja kwa moja; majaji wastaafu au hata Jaji Kiongozi wa Mahakama kuu ndiye awe mkuu wa BODI.
Nasema hivi kwasababu, zamani kabla ya mtu kuruhusiwa kuwa wakili wa kujitegemea ilikuwa ni lazima uombe ruhusu kwa Jaji mkuu.

Tatu, kama la pili litashidikana basi hata OFISI YA MWANASHERIA mkuu wa serikali ihusishwe na hii BODI. Nasema hili kwasababu State Attorneys ambao nao ni mawakili wa serikali wako chini ya hii ofisi.
Mwajiri wao Mkuu ni naibu mwanasheria mkuu, ambaye kwa namna moja au nyingine anajua nini kinaendelea kwenye hizi mahakama.

Nne, BODI YA LAW SCHOOL ni lazima ihusishe wadau wakuu wa elimu Tanzania; na huu ndiyo utaratibu wa dunia nzima. Tanzania wadau wakuu wa elimu hawahishwi kwenye maamuzi, hapa inatufanya tuamini kwamba LAW SHOOL ni pango la wanyanganyi.

Mwarobaini wa hili na kuzuia rishwa na malalamiko ya wanafunzi nchi nzima ni lazima wadau wakuu wa Sheria wahusishwe:

  1. Mahakama Kuu.
  2. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu.
  3. Vyuo vikuu vyote vya sheria vya Tanzania.
CC: Tomahawk , Advocate J , EJay , Mushobozi , Mahesabu
 
OMBA SANA MUNGU AND SOMA SANA....utachomoka tu law school.....

asante Mungu kwa kunivusha!
 
Back
Top Bottom