LAW GRADUATE SCHOOL - Ni kwa watoto wa mawaziri, majaji na wafanyabiashara?

mwewe

Senior Member
Jul 17, 2007
124
5
Moja ya masharti ya kujiunga na fani ya uanasheria ilikuwa ni kumaliza mafunzo ya internship kwa mwaka mmoja. Utaratibu huu umebadilishwa, hivyo kuanzia mwaka huu wahitimu wote wa Laws wanatakiwa kupitia kwenye Graduate School pale Mlimani (yalipo maskani ya muda)kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Tatizo lililopo ni masharti ya kujiunga. Kila mwombaji anatakiwa kulipa IN FULL kiasi cha Shs.1,570,000. Tangazo hili limetoka tarehe 10.03.2008 na tarehe ya mwisho ni 25.03.2008.

Hivi kweli pana mkulima au mlalahoi wa nchi hii anayeweza ku-raise kiasi hicho kwa muda mfupi kiasi hicho? Ikumbukwe kuwa wengi wa waombaji wamesoma kwa mikopo ya Bodi na wengi wanatoka mikoani na wanapaswa wajitegemee wakiwa hapa DSM.

a) Hii sio njia ya kuwaondoa walalahoi kwenye profession ya U-Lawyer?
b) Serikali - kupitia kwa Waziri Nagu aliyelianzisha hili - haikuweza kuandaa utaratibu mzuri tu wa kuwawezesha vijana hao ama kupata mikopo au kuwagharamia?
c)Kiasi cha hela hizo, hakiwezi kulipwa kwa awamu 3 au 4 kuwawezesha vijana hao kujiunga na masomo.

Kwa hili, naomba serikali - and especially Dr. NAGU, iwajibike kwa mipangilio hii mibovu.
 
c)Kiasi cha hela hizo, hakiwezi kulipwa kwa awamu 3 au 4 kuwawezesha vijana hao kujiunga na masomo.Hivi watanzania mbona ni wavivu kufikiria!!! Haya siyo maswali ya kuiuliza serikali ya CCM!

Mlishaambiwa siku nyingi Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe. Na miaka ya karibuni tumewaambia maisha bora kwa kila MTANZANIA. Sasa wewe unakaa mkoani au kijijini umekuwa mtanzania toka lini? Nani kakuambia kuwa mtu wa kijijini ana haki ya kusoma elimu ya juu kwa kodi za watanzania. Ukae ukijua kuwa si elimu tu, hata matibabu ya uhakika wanaostahili ni WATANZANIA. Nyumba na makazi bora ni kwa ajili ya WATANZANIA. By the way usije ukafikiri na huko vijijini na nyinyi ni WATANZANIA. Nyinyi yenu benderea tu.

Ila kwa kuwa mna nguvu msijali sababu mtakuwa msaada mkubwa sana wakati WATANZANIA wakihitaji ma-house girl, vibarua, na nguvu kazi nyingine isiyoelimika. WATANZNIA wana pesa ya kutosha hivyo watawalipa mshahara mzuri tu unaweza kubahatika ukapata 50,000 kwa mwezi kwa kazi ya kuwaogesha watoto wa KITANZANIA na kuwapikia wengine wanaosoma LAW GRADUATE SCHOOL ili wakirudi toka shule wakute chakula tayari.

Kimsingi hata zile loan za undergraduates ilishawekwa wazi kuwa ni DIVISIONS ONE tu ndio watasomeshwa kwa pesa ya uma. Hii ni wazi kuwa hizi nafasi ni za WATANZANIA. Sasa huko kijijini toka lini mnapata DIvision one!!!?? MSitake kuleta kichekesho!!! Utapate Division one wakati hata walimu hamna huko Kilindi, Kilwa, Ujiji, Ileje, Chanika, na kwingine. Division ONE inapatikanaje kwenye hizo nyumba za matope, zisizo na umeme,zilizojaa mbu, magonjwa, na wakati hata mlo wa jioni hamuujui!! Hao form six leavers mmeletewa wawafundishe ili kuwagelesha tu na atleast mjue kuna kitu kinaitwa elimu ambacho WATANZANIA ndio wanakifurahia huko Dar es salaam na kwingine.

Siku za karibuni mmekuwa mkiwapigia kelele sana watoto wa WATANZANIA. Mara sijui wanapendelewa BOT, mara sijui scholarships za upendeleao, mara sijui baba zao ni mafisadi. Sasa mkae mkjiua kuwa hii LAW GRADUATE SCHOOL ndio inakuja kuwamaliza zaidi sababu wakishaelemika hawa ndio watasaidia kuwapeleka lupango huko segerea, Keko, na kwingine kunakowafaa.
 
Moja ya masharti ya kujiunga na fani ya uanasheria ilikuwa ni kumaliza mafunzo ya internship kwa mwaka mmoja. Utaratibu huu umebadilishwa, hivyo kuanzia mwaka huu wahitimu wote wa Laws wanatakiwa kupitia kwenye Graduate School pale Mlimani (yalipo maskani ya muda)kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Tatizo lililopo ni masharti ya kujiunga. Kila mwombaji anatakiwa kulipa IN FULL kiasi cha Shs.1,570,000. Tangazo hili limetoka tarehe 10.03.2008 na tarehe ya mwisho ni 25.03.2008.

Hivi kweli pana mkulima au mlalahoi wa nchi hii anayeweza ku-raise kiasi hicho kwa muda mfupi kiasi hicho? Ikumbukwe kuwa wengi wa waombaji wamesoma kwa mikopo ya Bodi na wengi wanatoka mikoani na wanapaswa wajitegemee wakiwa hapa DSM.

a) Hii sio njia ya kuwaondoa walalahoi kwenye profession ya U-Lawyer?
b) Serikali - kupitia kwa Waziri Nagu aliyelianzisha hili - haikuweza kuandaa utaratibu mzuri tu wa kuwawezesha vijana hao ama kupata mikopo au kuwagharamia?
c)Kiasi cha hela hizo, hakiwezi kulipwa kwa awamu 3 au 4 kuwawezesha vijana hao kujiunga na masomo.

Kwa hili, naomba serikali - and especially Dr. NAGU, iwajibike kwa mipangilio hii mibovu.

kama huko dsm, i expect you to be lawyers, who know how to demand your right. and the right is always obtained by all means. organize yourselves and require it to handle your rights, either by or without will.

i wish you all the best.
 
Moja ya masharti ya kujiunga na fani ya uanasheria ilikuwa ni kumaliza mafunzo ya internship kwa mwaka mmoja. Utaratibu huu umebadilishwa, hivyo kuanzia mwaka huu wahitimu wote wa Laws wanatakiwa kupitia kwenye Graduate School pale Mlimani (yalipo maskani ya muda)kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Tatizo lililopo ni masharti ya kujiunga. Kila mwombaji anatakiwa kulipa IN FULL kiasi cha Shs.1,570,000. Tangazo hili limetoka tarehe 10.03.2008 na tarehe ya mwisho ni 25.03.2008.

Hivi kweli pana mkulima au mlalahoi wa nchi hii anayeweza ku-raise kiasi hicho kwa muda mfupi kiasi hicho? Ikumbukwe kuwa wengi wa waombaji wamesoma kwa mikopo ya Bodi na wengi wanatoka mikoani na wanapaswa wajitegemee wakiwa hapa DSM.

a) Hii sio njia ya kuwaondoa walalahoi kwenye profession ya U-Lawyer?
b) Serikali - kupitia kwa Waziri Nagu aliyelianzisha hili - haikuweza kuandaa utaratibu mzuri tu wa kuwawezesha vijana hao ama kupata mikopo au kuwagharamia?
c)Kiasi cha hela hizo, hakiwezi kulipwa kwa awamu 3 au 4 kuwawezesha vijana hao kujiunga na masomo.

Kwa hili, naomba serikali - and especially Dr. NAGU, iwajibike kwa mipangilio hii mibovu.

pole sana lakini huyu Nagu sio dokta muongo kasoma wapi?
 
Pole sana ndugu yangu,lakini omba mungu atakusaidia usome hiyo law school.Problem ya viongozi wetu wa kibongo wamejengeka ktk tabia za kukurupuka,akibahatika kwenda nje basi shughuli imeanza,atakachokiona huko anataka leo kiwe TZ.

Yaaani hawa viongozi wetu ukiwatazama kwa harakaharaka unaamini kwamba kisomo chao ni duni NA KAMA WALIKWENDA SHULE BASI WAS JUST KUDESA.Kwanini usifanye utafiti katika nchi yako kabla ya KUFANYA implementation?Matokeo yake ndio hayo mnaanza kuwabana UDSM ambao wanapumulia mashine kutokaNA na uhaba wa vyumba vya madarasa,leo mnaipeleka Law School UDSM,hivi viongozi hamuoni kama mnafanya mzaha na nchi yetu.NASEMA HIVI ONE DAY YES.VILIO TUNAVYOVITOA VINASIKIKA KWA MUNGU,IPO SIKU BUBU ATASEMA NA VIZIWI WATASIKIA.HAKUNA MAREFU YASIYOKUA NA NCHA.
 
Its very sad pia nasikia kuna kikwazo kingine kwamba mtu anahitaji kuwa amefanya 16 modules kabla ya kukubalika ku join the law school and those modules should include International Private Law and Altenative Dispute Resolution..kwa kweli imenishangaza sana...watu waliopanga hii system si kama wamejisahau kwamba wanafunzi wakiwa kama Undergraduate au postgrad huwa wanachagua wenyewe areas to specialise in...sasa hiki kimekuwa kikwazo kikubwa kwa wengi...na sasa nasikia huwezi kupata certificate mwisho wa mwaka kama hukufanya masomo hayo!!
 
Attachments

  • Law School of Tanzania Act 2007.pdf
    641.1 KB · Views: 129
Unajua tatizo la viongozi wetu wamelewa fedha kiasi kwamba wanajifanya kusahau hali halisi ya watanzania wengi.Waziri anapewa nyumba,gari na mafuta kibao,analipiwa umeme,maji,simu n.k .Nyumba yake inawekewa kila kitu mpaka kijiko,ana 'allowance' nyingine kibao acha za ubunge.Kwa kweli mshahara wake hauguswi benki,saa ngapi akukumbuke wewe uluyempigia kura? hajui na hajali kama kuna watu wana njaa na kujikwamua kwao ni kupata elimu.Nawaambieni Tamzania hii ni tajiri tena tajiri sana na kama rasilimali tulizonazo na tunazoweza kuziendeleza tungezitumia vizuri,walahi serikali isingeshindwa kumlipia kila aliyeomba hiyo LAW SCHOOL, na si hivyo tu ungekutu huko Kilindi,Ileje na Kasulu kuna umeme mpaka kwa bibi zetu,huduma za afya zingekua nzuri na za bure.Yaani inauma sana,fedha zetu tunazozilipia kodi zinawaneemesha wachache na ndiyo hao watakaokwenda huko kwenye Law School,Mungu mkubwa atasikia kilio cha waTZ na Mungu akikisikia hujibu kwa mashambulizi.
 
Back
Top Bottom