Laura Pettie: Hivi karibuni, matukio ya kikatili dhidi ya wanaume yanaibuka kwa kasi

Igande

Member
Jun 10, 2021
19
75
PETROLI TENA...

Msichana aliyejulikana kwa jina la Tina mkazi wa eneo la Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kuchoma nyumba ya anayedaiwa kuwa mpenzi wake aitwaye kwa jina moja la Kelvin mkazi wa Mbezi Bondeni.
-------------------------

Hili ni tukio lingine tena. Huyu jamaa angekuwa ndani au hili tukio lingetendeka usiku, saa hizi tungekuwa tunaandika mengine juu ya Kelvin.

Mara zote wanawake wanapotendewa ukatili kuna kauli nyingi za kukemea na kuna kauli fulani huwa zinaudhi sana. Kauli zinazohalalisha matukio kama hayo. Kauli kama, wanawake punguzeni midomo. Alikula hela yake. Wanawake msipoacha usaliti dawa yenu ndiyo hii. nk nk.

Hivi karibuni, matukio ya kikatili dhidi ya wanaume yanaibuka kwa kasi. Kauli za kukemea ni chache na hali kadhalika kauli zile zile za maudhi zinachomoza tena. Kauli za kuhalalisha mtu kutendewa jambo baya kwa sababu hii au ile. Tunaingiza masihara na kauli za kuchochea haya mambo kuendelea. Utasikia, Nyie gunia mbili za mkaa, sisi petroli. Tutawachoma mpaka mkome. Hii ndiyo dawa yenu sasa.

Wakati tunapofanya mizaha kama hii.
Wakati tunaposhindwa kupambana kukemea.
Wakati tunapotiana hamasa ya visasi kwa lugha za utani.
Kuna watu afya zao za akili zimeshayumba kitambo wanahamasika kweli.

Tunasahau tuna watoto, ndugu, jamaa na marafiki wa kike wenye wenza.
Tunasahau tuna watoto, ndugu, jamaa na marafiki wa kiume wenye wenza.
Wanaoweza kukumbana na ukatili kama huu wakati wowote, popote.

Tunafanya mzaha mtu akijiua.
Tunafanya mzaha mtu akiua.
Tunafanya mzaha mtu akifunguka kuelezea maumivu yake kisaikolojia.
Daaaah!!

Kuna athari kubwa kushadadia na kutoa kauli zenye kulea matukio kama haya. Kuna athari kubwa kukaa kimya pasi kuelimishana na kuzungumza na jamii kuwa hii si njia sahihi ya kupambana na msongo au maumivu ya kutendwa. Haileti nafuu. Haileti nafuu hata kidogo. Unawaumiza na wengine wasiohusika.

Afya yako ya akili ndiyo inayoendesha maamuzi, mawazo na hulka zako. Haijalishi unapitia au umepitia nini hebu jiulize, unaposhadadia matukio ya kikatili hata kwa kofia ya utani, unajisikiaje nafsini? uko sawa kichwani?
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
57,228
2,000
Siyo kwa wanaume tu, haya mambo yanaenda zamu kwa zamu.

Juzi tu chamazi mwanaume alifanya yake ikaja Tina, kabla ya Tina Neema

Issue inakwenda zam kwa zam

Ova
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom