Laughter series: Tricky mummy!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Laughter series: Tricky mummy!!

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Kwetunikwetu, Apr 23, 2009.

 1. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kuna jamaa mmoja aitwae Williams alikuwa akisoma chuo huko California, ambapo alikuwa aki-share hostel pamoja na dada mmoja aitwae Jane. Katika apartment waliyopanga pale hostel ilikuwa na vyumba vitatu vya kulala, sebule ndogo, jiko nk.
  Siku moja Williams alitembelewa na mama yake mzazi pale chuoni (ie hostel). Williams akatoa utambulisho kuhusu Jane kuwa ni msichana tu wanayesoma nae, wala kukaa nae kwenye nyumba hiyo hakumaanishi lolote zaidi ya classmate tu. Mama alikubali utambulisho huo ingawa akawa na dukuduku kuona inawezekana vipi mwanae akae na totoz bila kuwa na uhusiano zaidi ya masomo. Hata hivyo wasiwasi huo ulionekana kuwa hauna nguvu kwa vile Williams alijitahidi kumwelewesha mama yake na pia mama mwenyewe kuthibitisha baada ya kuona kweli kila mtu analala chumba chake.
  After two weeks mama akaamua kuondoka zake kurudi kwake. Huku nyuma, baada ya siku mbili kupita tangu mama aondoke, Jane akagundua kuwa kiroba kilichokuwa na mchele almost 20 kg hakipo. Baada ya kutafuta sana aliamua kumweleza Williams juu ya upotevu wa chakula hicho, hata hivyo alimsihi Williams asijisikie vibaya kwa vile hamaanishi kuwa anamhisi mama kuwa ni mwizi.
  Williams akashauri wampigie simu mama ili kujua imekuwaje lakini Jane alikataa. Baada ya mabishano ya almost siku saba hatimaye Jane alikubali Williams amuulize mama yake kuhusu upotevu wa kile chakula. Basi Williams akanyanyua simu na kuamua kumpigia mama yake, ambapo baada ya salamu ujumbe mahsusi ukatolewa.
  Williams: Mama tangu siku ile ulipoondoka, kile kiroba cha mchele hakionekani jikoni. Sisemi kwamba mama umeiba, ila ukweli ni kwamba kiroba hakipo jikoni!!!
  Mama Williams: Mwanangu nashukuru sana kwa kunihisi vibaya, na mimi pia sisemi kuwa Jane ni girlfriend wako, ila ni ukweli kuwa Jane halali chumbani kwake!!!!!!!! Kwa vile kiroba cha mchele kipo chini ya pillow kwenye kitanda chumbani kwake tangu siku nilipoondoka………………………….!
   
  Last edited: Apr 23, 2009
Loading...