LATRA wafafanua madereva wa taksi za mtandaoni walioandamana kwenda ofisini hapo

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Baada ya Madereva wa taksi za mitandao wameandamana mpaka makao makuu ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Jijini Dar es Salaam kudai kupandishwa kwa bei elekezi ambazo licha ya kupandishwa bado kuna wahusika awazifanyii kazi hali hiyo inatokana na kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta, LATRA imetoa ufafanuzi.

Madereva hao ambao ni wanachama wa Chama cha Madereva wa Mtandaoni (Tanzania Online Drivers Association - TODA) waliandamana Aprili 12, 2022 wakidai wamiliki wa huduma ya Uber na Bolt ndiyo ambao hawataki kupandisha bei ya nauli kitu ambacho kinawaumiza wao.

LATRA wametoa ufafanuzi huu hapa…

Latra madereva.jpg
 
Huo sio ufafanuzi ni muhtasari tu na pia hii nchi wengi waliopo kwenye nafasi za kutolea majibu ya Mamlaka hawana elimu wala uelewa wa Mamlaka husika na Changamoto zake. Hivyo, kupelekea majibu ya hovyo kama haya.

Mimi binafsi sijaona jibu wala ufafanuzi wowote katika hili zaidi ya hofu na uoga kwa hizo kampuni za wazungu/wageni kwa kuhofia kutopata kodi.

Au itakua Kiongozi anasubiria Mama arudi kutoka Marekani ili amuulize afanyeje, ajibuje ndiyo atoe majibu. Anahofia kukosea na kupelekea wawekezaji kuondoka na Mama kumkasirikia hata kupelekea Kibarua chake kuota nyasi.

Chunguza elimu ya Mkurugenzi wa Latra kisha utajua kwanini kuna utaratibu n uendeshaji wa hovyo pale ofisini.

Naomba kuwasilisha.
 
Eti nauli iongezwe Kwa 100% ?

Kwa nini?

Yani kama mahala ulikuwa unaenda kwa 10,000 sasa uende kwa shilingi 20,000

Nani ataitaka hiyo huduma?!
 
Halafu Kwanini nguvu ya demand na supply isiachwe ipange bei?

Afadhali mnge intervene in favor of wananchi badala yake mnataka kuumiza wananchi na kwa sababu kuna mbadala ya huduma za usafiri kama vile daladala wananchi wata shift in demand na biashara ya hao jamaa kuanguka kama siyo kufa kabisa !
Ndio maana wana raise concern.
 
Baada ya Madereva wa taksi za mitandao wameandamana mpaka makao makuu ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Jijini Dar es Salaam kudai kupandishwa kwa bei elekezi ambazo licha ya kupandishwa bado kuna wahusika awazifanyii kazi hali hiyo inatokana na kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta, LATRA imetoa ufafanuzi.

Madereva hao ambao ni wanachama wa Chama cha Madereva wa Mtandaoni (Tanzania Online Drivers Association - TODA) waliandamana Aprili 12, 2022 wakidai wamiliki wa huduma ya Uber na Bolt ndiyo ambao hawataki kupandisha bei ya nauli kitu ambacho kinawaumiza wao.

LATRA wametoa ufafanuzi huu hapa…

Kuna App za wazawa kama TANTAXI ambazo ziko vizuri sana na zingeleta mabadiliko ila watu wamekariri uber na Bolt. Uwekezaji pia lazima utazame wawekezaji wa ndani ambao gharama zao za uendeshaji sio kubwa kivile kiasi haitowalazimu kuweka kamisheni kubwa kama ilivyo kwa Bolt na Uber: TanTaxi Passenger - Apps on Google Play. Hii TanTaxi haikati kamisheni kwa sasa na wamedhamiria kutovuka asilimia 10%. Abiria anafaidika na dereva anafaidika na kupata moyo wa kutoka huduma nzuri.
 
Naona unapigia upatu app yako.

Sent from my CPH2349 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom