LATRA na Askari wa Usalama Barabarani, mlichokifanya hapo Bomang'ombe si sahihi kwa utalii

Semahengere

JF-Expert Member
Nov 29, 2020
1,186
1,955
Habari wadau.

Mimi sio muongeaji sana ila kwa Leo kilichofanyika Bomang'ombe Moshi ni kuuchafua utalii.

Latra Leo walizuia magari yote ya Transfer yaliyokuwa yamebeba watalii wanaotoka Airport na yanayokwenda na Yale yanayotoka mlima Kilimanjaro kwa wageni waliomaliza trekking na wanaoenda kuanza trekking kisa wanahitaji Latra.

Na ni wao waliokuja tukakaa nao kikao wakitaka maoni ya wadau Ili wakate geneze sheria then wakasema watarudi tena kutuletea mrejesho

Leo tunashangaa wamezuia magari wengi wao waliokuwa wageni wao wamelipa vibali vyao ya Tanapa vya kuanza trekking Leo hawakuweza Tena pesa zimeenda Bure na siku imepotea
Wacha tuone wageni wataandika Nini huko Duniani.

USHAURI WANGU
Latra tafuteni namna Bora ya kufwatilia leseni zenu. Na mkumbuke utalii ulikuwa hoi ndio unafufuka vibali vingi viliisha ndio watu wanadunduliza wakate.

Si lazima Hadi wageni wapewe usumbufu kwa dhambi isiyowahusu.
Tangazieni wadau wapeni muda wakate hicho kileseni chenu Watu wametoka kwenye Hali ngumu jamani
Kuaibishana kwa wageni sio ustaarabu.
 
Permit huwa zinakatwa magetini, kilichofanyika sio sahihi maana kama wageni wamerudi mahotelini ni kuwa plan yake imeharibiwa. Upande wa Tour company nao umepata hasara ya kuwalaza hao walioona bora wabaki na kuanza tena safari leo
 
Habari wadau.

Mimi sio muongeaji sana ila kwa Leo kilichofanyika Bomang'ombe Moshi ni kuuchafua utalii.

Latra Leo walizuia magari yote ya Transfer yaliyokuwa yamebeba watalii wanaotoka Airport na yanayokwenda na Yale yanayotoka mlima Kilimanjaro kwa wageni waliomaliza trekking na wanaoenda kuanza trekking kisa wanahitaji Latra.

Na ni wao waliokuja tukakaa nao kikao wakitaka maoni ya wadau Ili wakate geneze sheria then wakasema watarudi tena kutuletea mrejesho

Leo tunashangaa wamezuia magari wengi wao waliokuwa wageni wao wamelipa vibali vyao ya Tanapa vya kuanza trekking Leo hawakuweza Tena pesa zimeenda Bure na siku imepotea
Wacha tuone wageni wataandika Nini huko Duniani.

USHAURI WANGU
Latra tafuteni namna Bora ya kufwatilia leseni zenu. Na mkumbuke utalii ulikuwa hoi ndio unafufuka vibali vingi viliisha ndio watu wanadunduliza wakate.

Si lazima Hadi wageni wapewe usumbufu kwa dhambi isiyowahusu.
Tangazieni wadau wapeni muda wakate hicho kileseni chenu Watu wametoka kwenye Hali ngumu jamani
Kuaibishana kwa wageni sio ustaarabu.
Mama anajenga kwa bidii zote watu wake hao hao wanamwaribia, kwanini hao latra wasi # NOTE hayo magari hasa yenye wageni yakaendelea na safari zao,
#NOTA_BENE, watalii muda kwao ni kitu kikubwa mno, na huja kwa budget maalum. Hawana wajomba hapa wa kwenda kulala kwao bure..!
 
Siku moja Pale Kongowe ya Mbagala wakatupanga foleni kama gari 10 hivi nyakati za jioni zikiwemo school bus zenye watoto wadogo waliochoka..
Tuliwacharukia mno lakini wale jamaa akili zao wanazijua wenyewe walikomaa
Gari yangu cc ilikuwa 750 haipaswi kulipiwa LATRA kwakuwa sheria inasema kuanzia cc 1000 lakini ukijaribu kuwaelewesha wanakuwa wakali
 
Mama anajenga kwa bidii zote watu wake hao hao wanamwaribia, kwanini hao latra wasi # NOTE hayo magari hasa yenye wageni yakaendelea na safari zao,
#NOTA_BENE, watalii muda kwao ni kitu kikubwa mno, na huja kwa budget maalum. Hawana wajomba hapa wa kwenda kulala kwao bure..!
Hiko anachojenga ni kipi?
 
Tatizo lenu hamtaki kufanya biashara kihalali, mna noah na Alphard za private, hamjakatia TALA wala LATRA, Mnataka mfanye kazi kwa uhuru.. Hamuoni kuwa hamuwatendei hakibwale wanaofuata vigezo vyote?
Hao wazungu mkienda kwao wanaheshimu sana sheria, wakifika huku mnavunja sheria kisingizio eti mmebeba wazungu, acheni ubabaishaji katieni vibali
 
TRA, POLISI, LATRA na Wizara ya maliasili na utalii endeleeni kukaza hivyohivyo mpaka wote wakatie vibali.. Haiwezekani nilipe dola 500 TALA, Dola 50 LATRA, na hela kibao TRA, Alafu nyie hamjalipia kote huko na mnataka mfanye biashara bila vibali, eti kisa mnabeba wazungu.. Hiyo haiwezekani wazee, punguzeni kulalamika katieni vibali
 
Back
Top Bottom