LATRA: Mfumo wa ukataji tiketi kwa njia za kielektroniki haulengi kuumiza yeyote

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali imesema iko tayari kukaa pamoja na wamiliki wa mabasi kujadili mambo mbalimbali ya kuboresha sekta hiyo huku ikiwatoa hofu kutokana na kutangaza mabadiliko ya mfumo wa kawaida wa kukata tiketi kwa njia za kielektroniki.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usafiri ardhini (LATRA), Gilliard Ngewe alisema hayo jana na kubainisha kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza mapato ya serikali.

Alisema serikali iko tayari kukaa pamoja na wamiliki wa mabasi kujadili changamoto zao ili kuhakikisha wanaboresha sekta hiyo muhimu.

"Hatujafanya uamuzi huu kuumiza yeyote tunalenga kusaidia kila upande kwa nafasi yake tuone tija ya sekta hii, sasa unakuta tukiwaita wamiliki wanatuma wawakilishi sasa kwa namna hii hatuwezi kufika tunaendelea kuwaelimisha, tumeshafanya mikoa mingi ikiwemo Arusha, Tanga, Dar es Salaam tukagundua tatizo ni uelewa na uoga hawataki kuwa wazi,"alieleza Ngewe.

Akizungumzia mfumo wa kukata tiketi kwa njia za kielektroniki, alisema uamuzi huo utawezesha kukuza sekta ya uchukuzi na kuondoa usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza kwa abiria wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali kwani baadhi yao wamekuwa wakikatiwa tiketi isiyo halali.

Alisema tiketi ya kawaida inapokatwa fedha inapitia kwenye mikono ya watu wengi na kiasi kinachomfikia msafirishaji ni kidogo na mwisho wa mwaka wanashindwa kulipa Kodi na hata kupata hasara.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Kampuni ya Shabiby, Mabkhet Omary aliipongeza serikali akisema mfumo huo utakuwa msaada mkubwa kwao kama wamiliki kwani utadhibiti wapiga debe hali iliyokuwa ikisababisha kutopata mapato waliyokusudia.

"Kuna vitu sisi wamiliki tulikuwa tukikosa hasa ikisababishwa na hawa wapiga debe wanapunguza sana faida maana na yeye anategemea hapo kwa hiyo katika huu mfumo tutapata kiasi cha fedha kikichopangwa na niombe tu elimu itolewe,"alipongeza Omary.

Issa Mrwata ambaye ni Mkurugenzi wa Basi la Shukrani alieleza kwamba mfumo huo kwao ni changamoto kwani zipo baadhi ya huduma ambazo wamekuwa wakilipa kwa fedha taslimu na bado hawana elimu ya kutosha kuhusu mfumo wa tiketi mtandao.

Akitoa maoni yake Moses Julio ambaye ni mkazi wa Mpunguzi alisema mfumo huo utapunguza usumbufu ambao wamekuwa wakiupata kituoni ikiwemo kudanganywa, kupewa tiketi feki na kung'ang'aniwa na mawakala wa mabasi ambapo wengine hupoteza mizigo yao .

Pia Husna Juma mkazi wa Veyula alisema "Kwa mjini wenye elimu zao itawasaidia lakini siyo vijijini wawape elimu tutapunguza gharama za usafiri maana tunatofautiana uwezo, nimefurahi sana sasa naweza kupata tiketi yangu nikiwa nyumbani,".

Mfumo wa tiketi mtandao ulizinduliwa Mei mwaka jana na aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe kwa lengo la kuleta tija kwa serikali, abiria na wamiliki wa mabasi.
 
Halaf una miaka kedekede humu, ila unachangia ushuzi tu, kama reply zimekuish kichwani soma thread hamia nyingine! Mnafanya Jf kuonekana jalala
Acha dharau. Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake hapa JF. Usituletee upumbavu wako wa kutaka kunyamazisha watu wengine. Ukiona vp, ww ndio ondoka jf
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom