LATRA Kibaha na wahusika simamieni magari yafike mwisho wa safari kama mlivyoyasajiri

eSIM

Senior Member
Sep 27, 2018
167
135
Kuna magari mengi sana ya Mbezi - Mwanalugali, Mbezi Boko Mnemela na sasa Mbezi Sofu yamesajiriwa kupeleka abiria huko lakini yanaishia Njuweni - Kibaha hii ni kikwazo kwa wakazi wa maeneo hayo maana gari zipo lakini hakuna hata moja inayoenda huko.

Sasa hii ruti mpya ya sofu magari ni mengi sana lakini hakuna linaloenda sofu. Tunaomba mamlaka husika kusimamia jambo hili ikiwa ni pamoja na kuzingatia nauli kama ilivyopangwa.

20210820_075710.jpg
 
Huko ulikotaja abiria ni wa kutegeshea muda fulani ndio wanakuwa wengi. Lakini muda mwingi hakuna, gari inapiga debe mpaka abiria waliopo ndani ya gari wanakereka.

Lakini Njuweni (Maili Moja) gari inasubiriwa na kundi la abiria na ikisimama tu wamejaa. Kuna siku hapo Mbezi ziliondoka gari kama 6 za Njuweni zote zimejaza.

Kwa mwenye gari kushusha Njuweni na kugeuza kuja Mbezi mwisho ni rahisi na inalipa kibiashara kuliko kwenda Mwanalugali, Boko Mnemela au Sofu.

Labda ianzishwe ruti mpya ya Njuweni-Mwnalugali,Njuweni-Boko Mnemela.
 
Sasa kama tatizo ni hilo la kutokuwa na abiria si mambo yatakuwa yaleyale hata yakianzia Njuweni - Sofu?

Ilitakiwa iwe hivi, gari iite Kibaha> Njuweni> Picha ya ndege>Sofu alafu ikifika Njuweni itapakia wengine wa Sofu, ikifika Loliondo hvyohvyo na ikifika Picha ya ndege itaendelea kupakia mpaka mwisho wa safari yake.

Sasa mnakuta abilia mpo wengi ila gari haliendi kisa eti Mwanalugali au Sofu 800 afu Njuweni 500 wanaona bora wachukue hizo 500 ageuke chapchap kwakuwa Njuweni kuna abiria wengi. Hili ni tatizo la usimanizi maana Sofu barabara ni nzuri sana.
 
Duh kweli maendeleo huko mwanalugali na Boko siku hizi kuna watu? Nilifanikiwa kukaa kidogo hapo kibaha mwaka 1979
Mzee wangu kama ulifanikiwa kununua Mashamba miaka hiyo sasa hivi wewe ni Milionea maana Kibaha kumekucha haswa hayo maeneo ya Kwa Mathias, Mkoani, Filibert Bay/Mkuza, Sofu, Picha ya ndege, Gill(Pangani), Lulanzi.
 
Duh pangani nako kuna mji😮 na mwanalugali, boko mnemela asee
 
Mzee wangu kama ulifanikiwa kununua Mashamba miaka hiyo sasa hivi wewe ni Milionea maana Kibaha kumekucha haswa hayo maeneo ya Kwa Mathias, Mkoani, Filibert Bay/Mkuza, Sofu, Picha ya ndege, Gill(Pangani), Lulanzi.

Nilinunuaga kiluvya enzi hizo hekari Kama 200…. Nilikaa kibaha sisi ndo tuliendesha mchakato wa kuufanya Pwani kuwa mkoa those days
 
Back
Top Bottom