Latino na harakati za kuzamia ughaibuni mpaka kutoswa baharini

Sasa unabisha kwamba hakuwepo?
Au alikuwepo lakini ni mzungu tu?
Ama alikuwa CIA?

Kuhusu hilo tusi sioni sababu ya kukutukana zaidi ya kudhihirisha ushamba wako kushindwa kujua hii ni story tu
We ni mshamba sana. Hiyo comment uliyo quote ni ya pili kumjibu mleta mada, ungesoma na comment ya kwanza uone nilisemaje na mleta mada alijibu vipi hadi kufikia kujibu hivo tena.
Uspende kudandia dandia comments za watu Ipo siku utadandia kichwa cha mb@0.
Kuwa makini.
 
We ni mshamba sana. Hiyo comment uliyo quote ni ya pili kumjibu mleta mada, ungesoma na comment ya kwanza uone nilisemaje na mleta mada alijibu vipi hadi kufikia kujibu hivo tena.
Uspende kudandia dandia comments za watu Ipo siku utadandia kichwa cha mb@0.
Kuwa makini
Nimeziona anzia juu nikawa navumilia nipate burudani, Ila kwa sehemu ya CIA asee jamaa amevuka mipaka
emoji1787.png
emoji23.png


Naona unazidi kudhihirisha ulemavu wako wa akili mkuu reply yenyewe ndo hiyo👆👆👆
😀😀😀😀😀 kukutukana ni matumizi mabaya ya matusi
 
Nimeziona anzia juu nikawa navumilia nipate burudani, Ila kwa sehemu ya CIA asee jamaa amevuka mipaka
emoji1787.png
emoji23.png


Naona unazidi kudhihirisha ulemavu wako wa akili mkuu reply yenyewe ndo hiyo
kukutukana ni matumizi mabaya ya matusi
Aya
 
Tuendelee
Yule joakim alichoamua niku kanyaga kile chakula tukose wote ila tulicho amua kufanya ule ugali tukageuza juu chini alafu tukaendelea kula joakimu akumuamini kama tumekula safi kile chakula nia yake ikawa imefeli.
Basi tukaendelea na harkati zetu kama kawida sasa kuna siku tulitoka pale tulipo tukaenda kijijini kwa jamaa yetu ambae tulikua nae pale anakaa chaka uko tumefika pale tumesalimia fresh tukaandaliwa chakula vizuri mboga ilikua panya tulikula maisha yakasonga,

Wakati tunarudi njiani tukakutana na waasi hawa wanatabia kumbe wanafika pale kijijini wanakamata watu wanaondoka nao kwenda kwao uko kuwafanyisha kazi kilazima bila malipo na uko inasemekana watu walikua wanakufa sana sababu ya kukosa huduma muhimu.
Basi tumeshtukia hawa hapa wakatuweka chini ya ulinzi pale tulikua wa nne na wale jamaa walikua na silaa atukua na ujanja wakatufunga kamba ni kama vile watumwa yani kamba imeunganishwa alifungwa mwenzangu na Mimi nimefungwa iyo iyo kama mnyororo ivi na wengne iyo kamba inaitwa kurubuku ngumu sana ikikauka ndio inakua nyepesi.

kumbe walikua na migodi ndio walitupeleka uko nikawakuta baazi ya wasichana ambao tulikua kwenye kjiji tulichopita kule wanako acha matiti wazi nao wapo pale na vijana wengine ina maana wale waasi walipita kule wakashika watu na kuwaleta pale wale wa Dada walikua wanafanya usafi pale basi tukafikishwa apo.
Mi sikuonesha kama nawajua nilikauka tu apo tukaanza kufanya kazi kinguvu bila malipo na hata chakula kwa siku ni mlo mmoja tu ikifika usiku wanaweka mziki walikua na betri za gari kwajili ya umeme na jenereta na hata wanawake walikua wanawachukua kinguvu tu akuna maelewano wanaenda kubaka wakati wa usiku wakiwa na mizuka yao kwenye mziki pale wanapiga risasi juu mzuka umepanda apo na hata wazungu wale nao wakawa wanakuja pale wanashirikiana nao wale waasi sasa katika kuangaza nikamuona yule mzungu alie tusaidia kule porini yupo pale.

Ila sikutaka anitambue mapema laikini niliona uyu anaweza kua msaada, siku iyo tukiwa kwenye kazi yule mzungu alikuja karibu yangu akanikumbuka alikuja kwangu tukaongea aliniulizia wale wenzangu nikaumueleza akaniambia ana jambo na Mimi ivyo nitulie nikawa nipo pale nasikilizia .
Katika wale wasichana mmoja. Baadae tulizoeana aliitwa suzana nilikua napiga nae sana story akaniambia pale sio salama sababu serikali huwa wanavamia sasa kutambua kama uyu raia au sio raia awajui ilo ivyo huwaga wanauwawa watu pale,
Tuliendelea kuwepo pale kabla ya yule mzungu kunipa msada kikosi cha serikali kilivamia pale ilikua mida kama ya saa 11 ivi alfajiri nimelala nikashtushwa na risasi kutoka nje nakuta tayari vurugu vibanda vina ungua moto milipuko watu wanakimbia kujiokoa pale
mi nilikua na lala na yule suzana tulitoka na jamaa wengnine tukaenda kama kwenye pango ivi tukajificha hapo ni eneo la mgodi.
Baadae ivi hali ikatulia sababu kikosi cha serikali kilizidiwa ivyo waliondoka watu walikufa wengne waliumia ivyo mi nikoana hapa sasa ndio kukimbia na tupo na yule msichana anazijua njia japo ni msituni.
Ivyo tulirudi tena mana kwa muda ule ilikua ni ngumu sababu ya uangalizi ulizidi na jamaa walikua na hasira na kuna mkubwa wao alikufa na hata.zile sherehe za usiku zilikoma na ulinzi uliimarishwa ila sisi mpango wetu ulikua pale pale kutoroka.

Siku iyo usiku sana mida ka ya saa nane Giza Nene ndio tukaona Leo tuondoke ila kule ni mbali jamaa walikua wanakaa kati kati ya misitu uko ni mikubwa sana na hata pale ukiondoka basi ujiandae kutembea kitambo kirefu sana na pia kuna wanyama wakali mule.
Ilibidi tuondoke lakini tulikuta zile njia ambako zinapita gari tukawa tunapita pembezoni ya njia sasa humo tumetembea wakati kama kuna kucha ivi inaonekana jamaa walishtuka sisi awakutuona pale ivyo kwa mbali tulisikia milio ya risasi tukaona tuache ile njia tuingie msituni kabisa sababu lazima wangejua tunapita kule ujanaja wakupita porini usingekuepo alafu walikua na mishale ya sumu na nyavu flani za kushikia wanyama.
Tukazama msituni sasa ile njia tukaacha tumekwenda mbali zile risasi atukusikia tena kuna sehemu tulifika tukapumzika jama yetu mmoja alikua na kiberiti na kisu tu atukua na cha zaidi ya ivyo tukakoka moto tukatulia apo nilikua peku wenzangu walivaa viatu sasa miba ilinichoma sana alafu upupu tulimopita mwili ulikua una washa sana tukawa tunajipaka majivu.
pale palikua na matunda yule Dada ndio alikua ana yajua tukala baadae safari iliendelea mbele tulikuta matunda ya mabungo ila ni makubwa sana tukala lakini yale mbegu hua aziliwi jamaa mmoja ye alikula na mbegu nyingi tu tumekwenda sehemu flani akaenda jisaidia aja iligoma kutoka tulisikia ana lia tulifikiri labda nyoka ka mgonga ikabidi tuamsaidie pale akajisaidia ila kwa maumivu na hata tulipo toka na kutembea jamaa alipungua spidi kutokana na maumivu Yale ilikua tunakwenda ikifika sehemu
mmoja wetu anapanda mtini juu kuangalia uelekeo maana msitu ni mkubwa sana.
Tuliendelea kutembea mpaka sehemu flani tukaona kama mji kwa mbali tukaenda tukaja kukuta kijiji usiku sana palikua na ufugaji pale tukapewa msaada na chakula ndio ilikua shida kubwa maji tulikua tunakuta miti ya kutoa maji tunakata tunakunywa aikua shida ya maji.
Jamaa alichinja bata mzinga tukamtengeneza pale tukala na chakula tukalala pale mi Niliwaza sasa hapa niitafute Maputo pale tuliachana yule dada alikwenda kwake na jamaa wengne mi nilibaki na mshikaji mmoja tukaondoka pale tukaanza safari kuitafuta Maputo yule jamaa ni mwenyeji na njia tumekwenda sana usiku wakati tupo njiani tukaingia sehemu moja ivi pana muziki kuingia humo nikakutana na Mangushi bana.
alikua mtu wa tungi sana alafu yupo na mademu wawili pale nikampa mkasa mzima yeye alipata ishu pale alikua anaenda Eswatin anachukua bangi anakuja kuuza pale alikua na bosi mmoja ivi.

yeye fikra zake kwamba tayari Mimi nipo south Africa basi usiku tukatoka mpaka geto kwake alikua na bastola black metal M9 akanitolea bangi pale akanipa kuvuta nikawa mtumiaji mzuri sana wa bangi kuliko pombe.
Asubuhi mi na Mangushi tukaenda kutana na bosi wake kule mi nikamwambia mi pia nahitaji kuingia mzigoni yule bosi akaniambia unajua kutumia bunduki nikamwambia Nina utaalamu wa bunduki kubwa sio izi ndogo hasa kwenye kuibalance basi jamaa akapanga nikutane na jamaa wengne tufanye mambo kumbe walikua na genge kubwa sana la ujambazi na genge jingine lipo kusini mwa Afrika ivyo tukapanga pale tuchomoke na ishu za passport uko boda chini yao mi ntasafiri fresh.
Basi tulienda afrika kusini Johannesburg tukiwa uko jamaa wanavyofanya mfano kuvamia sehemu wanaanza upelelezi kama ni nyumba wana angalia wanaishi wangapi na vitu kama ivyo.
Ila raia wa kule swala la mtu kumiliki silaa ni kawaida sababu ya ulinzi sasa ukijichanganya kuvamia ovyo kwisha habari yako,
Ila sasa katika izi kazi za ujambazi nikaja gundua ishu moja ukiwa mgeni unakua kama chambo sasa wao wanakutanguliza mbele wanakupa maelezo tu ukifika basi nao ndio wanakuja ukinasa wameondoka wewe umekamatwa.
Siku iyo katika kuingia maeneo kuvamia mi nilitangulizwa eneo la tukio wenzangu wapo nyuma ...................
Tutateajea wakuu
 
Tuendelee
Tulifika pale mi nikaingia sehemu moja ivi ya nyumba kama chambo ila sehemu ile nilikuja gundua ilikua na mbwa ila walifungwa kwa muda huo ilikua bado awajafunguliwa nikaingia ndan ya ile nyumba mpaka getini nilikua na koleo nikakata nyororo ilikua pale getini wale jamaa wakaingia tukavamia mule ndani.
Tukawatuliza tukachukua pesa simu laptop na zaga nyingne tukaondoka,
sasa baada ya kufanya vamizi nyingi ndio nikagundua ukiwa mgeni ndio unakua chambo sababu kuna wengne walio jiunga ndio walikua wanafanywa chambo ndio nilijua apo.
Siku iyo tukapanga na mshikaji tuende eswatini tukachukue mzigo wa bangi tukawa wanne tulikuia na Mangush tumeenda tukabeba ule mzigo ilikua ni oda maaalumu ile tunarudi tukavamiwa na jamaa wengne wakautunyang'anya ule mzigo wote mangushi alikimbia na Mimi nilikimbia jamaa wawili waliobaki walipigwa risasi niliingia porini nikatokea shamba moja kuna mzee alikua analima bangi na ma Apple katikat ya shamba nikafiki pale alinhoji nikampa mkasa nikabaki pale alafu niliumia mguu alinisaidi
Pale nilikaa kama wiki siku iyo walikuja watu pale wakachukua ma Apple na bangi nikaingia kwenye iyo gari nilipata lifti mpaka sehemu moja ivi club nikamkuta mangushi anakunywa pombe ila kaumia bega alijeruhuwa alikua na bandeji tulitoka pale mpaka nyumbani kwake mangushi.
Sasa wale waliotupa oda ya mzigo mangushi ilibidi awalipe ili kujenga uminifu sababu uwezi aminika kam mzigo umepotea kweli kwaiyo alikua anawalipa mdogo mdogo pesa yao .
Lakini mim kukaa kutokana na mikutuo ile
nikapata wazo niende Malawi nikamwambia mangushi nikamuelekeza kule kuna ndugu zangu wanafanya kazi ya ufundi magari lakini pia nataka niende kule nikaendelee na shughuli zangu za uvuvi jamaa akanipa go ahead.
Nilitulia siku chache pale kumbe sasa wale jamaa wenye mzigo awakuamini kama jamaa kaibiwa ivyo wakapanga kumvamia, siku iyo tuanatoka klabu usiku jamaa yupo na mademu wawili tumefika pale home tumeingia ndani tumekaa usiku ivi jamaa alikua ana mbwa tukasikia ana bweka sana mangushi akachungulia akaowaona jamaa wamezingira na ana wafahamu wapo na bunduki kumbe jamaa ile nyumba chumbani kwake kulikua na kiandaki siku ile ndio nikajua juu kipo kikapeti huwezi jua unaingia unakifunga ndio tukaingia humo tukajificha jamaa waliingia mpka mle ndani amna mtu tukasikia wana mgombeza jamaa walio mtuma atufatilie kwamba kadanganya jamaa anasema mi nimewaona wameingia humu waka msema alafu inaonekana jamaa ni mtu wa unga kwaiyo wakaona tu kwamba unga mwingi kapiga ivyo kawazngua.

Tulikaa pale mpaka asubuhi ndio tukatoka mangushi akaona pale sio salama akasema tufanye mpango tuludi south Africa tuelekee richdbay na kuna jamaa tukaungana nao walikua wanatoka msumbiji wanaenda south awa walikua wanaiba magari south africa wanakuja kuuza Msumbiji tukaondoka nao mpaka south kule mangush akatafuta geto tukapanga apo na alikua ana vijisent aikua shida ila sasa mangushi alikua mtu wa pombe sana hapa ndio nilishindwana nae siku iyo katoka kwenye tungi kaja na jamaa akawa tunakaa nae pale kumbe jamaa alikua snich alikua anachek mazngira akatuchomesha siku iyo walikuja kutuvamia ila mangushi alishtuka mapema tukajificha wale wamekuja kwenye chumba chetu wametukosa wakaona jamaa kawadanganya walimpiga visu vya shingo akafariki pale pale tulimkuta getini sasa kutokana na aya matukio nikaona hii sehemu ni hatarishi kwangu nikaona nifanye ile safari yangu ya kuelekea malawai .

Niliondoka south nikaenda Malawi brentaya nilikutana na yule ndugu yangu aliekua ana piga ishu za magari lakini mi nilijiunga na ishu za uvuvi eneo linaitwa nkata bei nikawa nafanya pale.

kuna kipindi nikawa naenda chukua mahitaji mzuzu apo kuna sehemu inaitwa mataifa market watu ndio huenda kufanya shopping baadae nilienda sehemu moja ivi inaitwa mikendeni ndio palikua kwa ndugu zangu wengne ambao walikua kule Malawi baadae nikapnga niludi nyumbani tz tena baada ya iyo mizunguko ila niliendelea kuwepo kule Malawi nikaja nikapata tenda jamaa mmoja alikua anahitaji injini ya boti na Tanzania zilikuepo maeneo ya msasani pale zilikua zinapatikana alihitaji injini alikua ana million 2 mi nilifanya mpango ikapatikana ya miliom moja na laki tano kwaiyo nilipga udalali cha juu changu .
Tuliondoka na jamaa kutoka Malawi kuja dar tulipita boda ila ile njia kuu atukupita kutokana na ualali wa vitambulisho na ishu ka izo tulipita njia za mkato mkato kwenye vijiji tukavuka na kuitafuta stend kuu ya mbeya kwa vile tuliingia usiku apakua na gari na muda huo ilikua kipindi cha likizo wanafunzi wengi ivyo gari zilikua adimu.
pale stendi kuna konda akatukatia tiketi ila ilikua ya kuondoka siku ya pili asubuhi na alitupa eneo la kulala pale stend mpaka asubuhi jamaa yangu yule alichukua pombe kali kuondoa baridi mi sikua mtu wa pombe nilimcheki yule konda akanitafutia mshikaji mmoja akanifanyia mpango wa bangi
ilikua bangi kavu ile aina mchanganyo nikavuta ila ilikua kali sana mpaka nikaisi jamaa kanichanganyia na kitu kingne nilimuuliza akaniambia hii kitu ya Malawi bangi za ukanda ule zinakua kali sana .

Asubuhi gari zilifika stendi kwenye ile kampuni zilifika tatu namba tatu ndio ilikua yetu tukapanda na kuondoka Mbeya saa tatu usiku ivi tuliingia ubungo na kutafuta sehemu ya kupumzika asubhi tulienda msasani kufata ule mzigo wakati nisha mpanga jamaa ela yangu ya udalali ile ya juu uyu wa injini nilimwambia million 2 ila mzgo ni million 1.5 na wa dukani nilimshusha million 1.3 ivyo kwote nilikua napiga na nina kama laki 7 apo.
Mzigo ukawa fresh tukapata injini ya Honda used imesimama fresh na hata jamaa akuamini sababu kule Malawi ni ishu kuzipata jamaa ilibid aludi ila sasa ilibidi nimsindikize tena mpaka boda ya Malawi kule mbeya akaenda mi nikapata gari ya mizigo nikarudi tena dar siku ya pili yake nikatafuta chumba kupitia dalali kule home niliona siwezi kukaa home kwa muda huo ivyo nikapata chumba maeneo ya karibu na bahari ndio nilimwambia anitafutie uko,
na vile vijisenti nilikua navyo nikanunua vitu vidogo dogo vya kuanzia pale geto ............,...........
tutarejea wakuu
 
Tumerejea
Pale nilipokua nahamia watu walinishangaa sikujali sana,, Nilihamia rasmi usiku mida kama ya saa mbili hivi laikini kwa maelezo ya dalali ile nyumba ilkua na wapangaji wengne wawili na Mimi nikawa wa tatu akanipa fungo fresh Ila mpaka muda huo sikuona mtu pale na sikujua kama wanaokaa pale ni wanawake au wanaume siku ile nikalala sijaona mtu asubuhi mi nikatoka nikaenda kwenye mishe zangu uko bichi mbweni nikaonane na wanangu ambao walikua kule wanapiga ishu za uvuvi kina salumu kibambe pia Fred mbuna ila sio yule mchezaji wa yanga.
Nilifika pale mbweni nipate samaki wa kutafuna na nilikua najulikana na washkaji aikua ishu nikapiga story na wana baadae nikarudi kule geto sasa nikawa nacheki mazingira ya pale na ishu ka izo pembeni tu hapo palikua na kibanda cha chips jamaa ana choma nikaona niende pale na ukicheki jamaa ni mweneyeji atanipa ABC za pale nikaenda pale kwanza nikaagiza chips na soda peps akanitengenezea fresh wakati nakula tukawa tunapiga story kumbe wakat nahamia aliniona basi nikamwambia toka nimehamia sijaona wapangaji wenzangu na dalali aliniambia pale wapo yule muuza chips akasema amna we ndio wa kwanza apakua na mtu pale mhmmm nikashangaa alafu akasema ile nyumba ile akaishia hapo nikamuuliza vipi akasema ndio ivyo we ndo wa kwanza alitaka kusema kitu akaishia hapo mi pale baada ya kumaliza nikarudi geto pale kulala nilikua na redio ile usiku nikawasha nasikiliza mziki ngoma kwa ngoma Mara nikasikia watu wanaongea chumba cha pili sauti ni ya kike na ya kiume nikajiuliza ina mana wakati nipo pale kwenye chips wamefika lakini jamaa kasema akai mtu nikaona poa nikatulia baadae nikasikia sauti ya kike akisema ili joto feni aifai ni heri AC mwanaume akasema nenda kaoge mimi sasa nika amka fasta kuwai pale kwenye kitasa kuchungulia anae toka milango ilikua inaangaliana cha ajabu sikuona mtu ila nikasikia bafuni maji yanamwagika ina maana pale alishatoka na baadae akarudi ila sikumuona ilibidi nitoke niende bafuni kuhakikisha kweli nikakuta maji yamemwagika na mtu katoka kuoga.
ila kile kitendo walishakiona nikasikia sauti ya kike inatoa kejeli alafu kasonya nikarudi chumbani kwangu nikatulia kwa vile natumia bangi nikawasha nivute baada ya kuwasha na ile nyumba aina sling bodi inaonekana harufu kule waliiskia wakaanza kuongea maneno tena
Na ile bangi nilifanya kusudi tu mi nikalala mpaka asubuhi nimetoka nikaenda tena kwenye mishe zangu niliporudi nikapita kwa muuza chips nikaona nimuhoji kwanza kwamba alisema pale amna watu mbona Jana nimesikia watu mule na wanatoa kejeli Kwangu jamaa alicheka alafu akasema mi Jana nilishindwa kukwambia pale watu hua awakai akifika mtu siku mbili tatu anaondoka kutokana na mambo ya mauza uza na hata mwenye nyumba hapa afiki wanakuja madalali tu na inaonekana madalali vituko vya mule wanavijua.

Ikabidi nimpigie yule dalali simu na kumueleza lile swala japo alikazia kwamba pale wapo watu ila wako bize na mishe zao ndio mana kila mtu ana funguo yake mi nikamwambia kama vipi niludishie nusu hasara nihame hapa akasema pesa kashampa bosi nisubiri apate mtu mwingne amlete ndio pesa ya uyo anipe kumbe yule dalali ndio michezo yake nikajua sasa wanafanya kusudi.

pale kwenye chips nikaona nitulie nione wale wanarudi mda gani nilikaa mpaka muuza chipsi anaanza funga nikatoka nikaenda karibu na pale nikatulia nichore wanaingia mida gani nilikaa muda mrefu sana sikuona mtu ikabidi niende tu geto kwangu nimefika pale nimeingia ndani nimewasha taa na redio nasikia wanaongea tena ina maana walishapita muda tu.
Ikabidi niwe mpole nilichofanya sasa nikawa navuta bangi kwa wingi na sauti ya redio naweka juu wale kwenye kufanya mapenz walikua wanapiga sana kelele nikaendelea kuishi kibishi maisha hayo hayo.
Kuna Siku tena narudi kabla ya kwenda pale geto nikabana tena mahali akapita bibi mmoja anatoka dukan alikua na kopo katoka nunua mafuta ya taa nikamsalimu nikamuulizia kuhusu pale nilipohamia maana niliona pale ye ni mwenyeji
yule bibi akashtuka alafu akasema pale sio pazuri nikamuuliza kwanni nilitaka anipe maelezo ya kina akaguna wakati anataka kunielezea kuna mdada alitokea yupo vizuri mrembo kweli ananukia utuli vizuri kabeba mkoba na zaga nyingne yule bibi alishtuka alafu yule Dada akapita na akasema acha kufatilia maisha ya watu akasonya yule bibi alianguka kwa mshtuko alafu yule Dada sasa kwa Mara ya kwanza ndio nikamuona anakwenda kwenye ile nyumba na kuingia ndani kiroho ngumu nilienda na nikalala pale ila sasa usiku huo sikulala.

zile sauti kuongea zinakuaga mbili iyo siku walizidi nikama walikua wanakaribishana walikua wengi.
Siku ya pili asubuhi nilikubali hasara pale nilihama na ile kodi kwa dalali nilisamehe siku shughulika nayo.
Yule dalali ikawa tukikutana ana nikwepa hizi ishu za nyumba kama hizi zinatokana na mazingira ya nyumba labda aliejenga alizurumu mtu au migogoro ya familia au kuvamia maeneo labda palikua na makaburi zamani na mambo mengine kama ayo.

Tutarejea...............
 
Tendelee Eid imepita sasa japo wapo wanao malizia

Basi pale mi nilihama kutokana na mauza uza Yale akuna ambae angeweza kuvumilia niliwaza kwanza awa watu naishi nao hapa ni majini na majini chakula Kikuu ni binadamu sasa ikitokea siku wakakosa uko mi ntageuka kua chakula nikaondoka pale.

Nikatafuta eneo jngne nikaanza maisha tena ila kwa vile sikua na mishe nikawa nasaka hapa na pale sasa kuna rafik angu mmoja Robati alikuja kunishtua palikua na ishu ya ulinzi kampuni ipo hapa Dar jina kapuni ilihitaji watu na wanawapa mafunzo kisha wanangia kazini mi niliona najiweza tayri nishatumia bunduki sio ishu kwangu tulifanya mpango barua za wazamini na paspot saiz tukapeleka maombi aikua tabu walihitaji watu si tukaingia moja kwa moja kwenye mafunzo na tukapata kazi ya ulinzi.

Sasa ulinzi ule ulikua unafanyika sehemu tofautu tofaut makampuni au shule au nyumba binafsi wanapohitaji walinzi kampuni ikipewa tenda inapeleka, mi nilipangwa na mwenzangu mmoja sio yule robati uyu ni mwngne robati alipangwa sehemu nyigne sisi tulipelekwa nyumba ya mtu binafsi alikua ni mama mmoja ivi mfanya biashara tukawa tunalinda pale.
Siku iyo saa 11 alafajiri yule mama anatoka mwenzangu yule akamfungulia geti akaondoka alikua na gari mi nipo pale ndio nilikua na bunduki yule akua na bunduki mim sikua mtu wa kujionesha sababu nipo na bunduki nilikua Mara nyingi najificha lakini kila kinachoendelea naona sababu ukiwa mlinzi upo na silaha majambazi wakivamia popote pale cha kwanza wao tageti yao ni mwenye silaha maana wanaona yule ndio ata waletea shida wanaanza na uyo kwaiyo lazima uwe makini unapokua mlinzi na upo na silaha wewe ndio inabidi uanze kumuona adui na sio adui aanze kukuona wewe.

Iyo mida baada ya yule mama kutoka na palikua na mbwa pale jamaa akawafungia wale mbwa bandani, baada ya dakika chache mbele ile gari ya yule mama ikarudi na kupiga honi pale getini ila honi azikua zile za kawaida jamaa akafungua mi nacheki tu ile gari ikaingia ndani ilipopita pale getini yule jamaa aliona watu wamemteka yule mama wamo ndani ya gari jamaa akashtuka akatoka mbio kuelekea bandani ili afungulie mbwa ile anashika komeo alipigwa risasi tatu mgongoni pale pale akafariki na mbwa wale akufungua mi nikaona hapa nipo na watu wenye silaha nzito ukicheki ya kwangu ni ya kukoki upige alafu useti wao wanazo za kuachia mfululizo ina maana nikiludisha shambulizi sichukui muda na uwawa fasta ikabidi ni bane tu ukicheki nisha survive maeneo kibao uko alafu nife kizembe tu hapa hapana .

Kuna jamaa mwingne nae alikua mlinzi iyo siku wanavamiwa alikua yupo kizembe tu yupo eneo la wazi alafu na kirungu tu jamaa walimpiga tofali kichwani akazimia aliposhtuka akakuta kashapigwa kamba wakampiga virungu vya kichwa vya kutosha alilazwa muhimbili miez mitatu kichwa kina manundu mpaka Leo na ile kazi aliacha na akarudi kwao Dodoma.

Uamuzi nilioamua ni kufanya mawasiliano nikampigia kiongozi wetu ili waje kuongeza nguvu msaada ulikuja kama nusu saa mbele na ile kampuni kubwa ina ambulance za wagonjwa wakaja wakambeba mshikaji wale majambazi walichukua kwa yule mama milioni 30 alafu yule mama wakamfunga kamba, inaonekana mama alikua nazo izo pesa ndani na kuna mtu alichoresha sababu jambazi akurupuki kuvamia kama kibaka
Kibaka ana mvamia mtu ajui labda ana ndizi na pilipli tu lakini jambazi anakua na ramani kabisa kwaiyo anaenda akijua kuna nini.
Walimchukua jamaa akiwa kafariki tayari apakua na la zaidi Mimi niliomba pale nihamishwe na wakanihamishia sehemu nyingne.
Hapa nilikua na jamaa mwngne nae sio mjuzi sana kwenye ulinzi isipokua ni ujanja ujanja tu sehemu nilio amishiwa ilikua karibu na bahari, siku iyo usiku mnene sana ghafla getini nikamuona bibi kasimama sijui katokea wapi sikumfata kumuuliza nilikaa kumtazama tu pale alikaa karibu masaa manne badae akaondoka mwenyewe kwanni sikumfata uwezi jua labda katumwa chambo ukijitokeza ovyo na kuleta shobo kwake unastukia umepigwa wewe ivyo sikumfata akaondoka mwenyewe
Siku nyingne tena nipo lindo hapo na yule mwenzangu tupo ndani tukasikia mtu anapita taratibu nje kuchungulia alikua na mavaz ya kike anapita anaenda ila alikua na marashi makali ananukia juu kichwani aonekani vizur ila chini unamuona akapotea zake yule mtu.
Siku nyingne ilitokea zarulala yule mwenzangu akaenda sehemu nyingne pale nikabaki peke angu wakati nipo lindo ukanipitia usingizi bana mida kama ya saa Tisa au sa kumi hii tunaita asubuhi ya uongo sababu panakua na muangaza flani ivi kama asubhi kumbe ni usiku hapa ukijichanganya unajua asubuhi kumekucha mi mudawangu ukifika naondoka mi nikaondoka bana mdogo mdogo nimefika sehemu kuna viwanja viwili vya mpira cha kiwanja cha kwanza nikasikia kelele za watu ndio nikajiaminisha kabisa kwamba kumekucha nikawa napita nakaribia ule uwanja ghafla nywele na mwili vikanisisimka sana sasa napita pale uwanjani nikakuta paka wengi sio watu nikajua hawa sio paka ni wanga nikanyosha sikuegeuka .
Nimefika mbele nikakutana na mtu akaniangalia sana sasa nimevaa gwanda zile za ulinzi akutilia Shaka mi nikaenda mpaka nyumbani kitandani nimetulia naona kiza kinazidi kila nikichungulia nje mhm badae nikasikia swalaha swalaha ile alfajir nikajua nimebugi siku ikapita.

Sasa yule jamaa niliepangiwa nae alikua na simu ya smartphone kubwa mi nilkiua nayo ndogo ambayo ina uwezo tu wa kuingia Facebook basi jamaa aliniambia nijiunge Facebook mi nikamwambia fb sitoiweza kutokana na lugha ya mule na Mimi sijasoma akaniambia aina mambo mengi na kipindi icho watu wengi fb ndio wanajiunga kwa wingi akasema unaposhindwa nta kuelekeza kweli akaniunganisha fb fresh akanipiga picha akaweka kwene profile akanielekeza vipengele vichache mi nikaanza kuchati alikua bi mkubwa flani ivi nikaanza chati nae ni mmama mtu mzima mtanzania lakini alikua anaishi Denmark akasema ye yupo kule miaka mingi anafanya shughuli zake na kaolewa uko.
Nika mwambia nahitaji mchumba uko vipi siwezi pata msichana uko akaniambia ngoja, basi nikawa nikipata mb naingia namsalimia fresh siku iyo akanitumia picha ya msichana akaniuliza uyo vipi nikamwambia yupo vizuri akasema ila ana watoto lakini anaishi mwenyewe tu hana mtu mi nikamwambia sawa akuna tatizo mama.
Akaniambia uyo siku za wikiendi anakuaga hapa kwangu kwaiyo nta kuunganisha akaniambia nitumie picha zako ili nimuoneshe du nikalipokea ilo nika mshilikisha yule mshkaji wakati tunatoka lindo akasema mi nakujua kwenye kuvaa sio mzembe cha msingi ukiwa home chagua pamba za maana vaa fresh nikupige picha tutume.
Tukafanikisha lile jambao zile picha nikamtumia yule bi mkubwa akaenda kumuonesha yule Dada zile picha akazikubali alafu yule mama akasema nimpe namba ya simu tulituma na yule jamaa yangu akasema tutume na code namba sababu ni nje ya nchi inahitaji ianze na code namba hii 255 jamaa alikua anani elekeza vitu vingi .
Kweli kwa Mara ya kwanza simu yangu ikapokea simu kutoka nje ya nchi ndio alikua yule binti akaniambia uyu mama kanipa namba zako alafu nimeona na picha zako mi pia nikamsifia pale ndio tukawa sasa tunawasiliana ila uyu dada alikua katokea kwenye kambi za wakimbizi uko burundi au Congo aliondika pale kwa msaada wa UN kwaiyo kiswahili alikua ana kiongea vizuri na tayari yeye alikua anatambulika raia wa kule ikawa sasa mida ya usiku wakati katulia akawa anapiga simu kwangu tunaongea.
Baadae akaniuliza utumii Skype au Viber nikamwambia simu yangu ina uwezo mdogo sana aiwezi Fanya ivyo vitu na kipindi kile wasap ilikua bado akasema kupiga simu kwangu anatumia gharama kubwa sana nikamwambia mi nafanya kazi ya ulinzi na hata uwezo wa kununua izo simu sina akaniambia uku kazi za ulinzi zina hela akasema basi ngoja nikufanyie mpango upate simu kubwa nikaona hapa natengenezewa mazingira basi nikasubiri.
Siku kazaa akaniambia nataka nikutumie pesa sasa nikajiuliza uyu pesa anatumaje na tuko mbali ivi mi bana sikua mtaalamu wa aya mambo ya mtandao ye akasema ata nitumia kwa njia ya western Union au money gramu mi ivo sivijui akaniulizia kitambulisho nnacho akasema nitatuma pesa alafu ntaweka majina yako yaliyo kwenye kitambulisho usikosee ata moja maana wata kusumbua kweli siku ya jumatano ilikua pesa iliingia nilipata ujumbe kwenye simu sababu aliweka namba yangu na aliniambia isizdi siku tatu sijachukua pesa inarudi kwa mwenyewe japo siku izi naisi wameongeza siku sjui ni siku saba akanipa namba za siri za kuonesha pale na majina yake fresh pale nikapata muangaza sasa na kutambua .
Nilienda bank nikafanya taratibu zote na kutoa copy kitambulisho na ishu zingine hatimae nikapata ile pesa kutoka nje ya nchi.
Tukawasiliana akaniambia yule bi mkubwa anakuja Tanzania ivyo atampa mzigo wangu aniletee Mimi na yule bi mkubwa siku kazaa akaniambia anakuja Tanzania kapewa mzigo ila akusema kuna nini ,
yule mama alisafiri mpaka uku Tanzania alifika ila sasa nikawa simpati kwenye simu kila nikimtafuta kumbe alikua yupo kweye ishu za kubadilisha laini kupata laini za kwetu uku.
Siku iyo mida ya saa kumi na moja jioni akanicheki tukaongea akasema tuonane mida ya saa mbili usiku maeneo ya Makumbusho ukawa mtihani mida iyo inabidi niwe kibaruani lindo sasa hapa nikapanga nikaombe ruhusa kwamba nimepata zarula lakini nikawaza nikaona watanizingua sababu kule wana ntegemea sikwenda siku iyo nilichofanya nikaenda saloon nikajiweka fresh ili niwe na muonekano wa utanashati alafu nikaenda mpaka pale makunbusho palikua na kama mgahawa pale ndani mi niliwai ili akija anikute nishafika nimekaa pale nikaona sio walau nijibust kuondoa noma akija nichangamke nikapata kinywaji kipo kama zanzi ivi nikapigilia nikapiga na pipi kifua kukata harufu.
Mida nikaona tax inakuja pale mbele yangu alafu ikanimulika taa flani ivi za kunishtua nikajua hapa keshaniona kweli alishuka yule bi mkubwa kwa shangwe nyingi tu yupo na wanawe rangi nyeupe ye aliolewa na mzungu ................................

Tutarejea
 
Back
Top Bottom