article
Senior Member
- Sep 10, 2016
- 184
- 344
Laptops ni komputa zinazobebeka kirahisi kwenye mkoba wa mgongoni au mkononi zinazopenda kutumiwa na wasomi wengi kurahisisha utatayarishaji wa kazi za kiofisi na zile zisiyo za kiofisi.
Laptops silionyesha uwezo mkubwa na Ufanisi na kuzipiku PDA kirahisi ambazo zilkuwa zimeshika soko la komputa zinazozohamishika duniani.
Baadhi ya aina fulani za laptops kama vile Apple zimekuwa zikitumiwa na watu wachache wenye uwezo wa kifedha kutokana na bei yake kuwa ghali sana ukilinganisha na komputa nyingine na kuonyesha ufahari fulani.
Mageuzi ya haraka kwenye teknologia ya smatifoni yanapelekea maisha ya laptop kuwa hatarini kwa sasa kutokana na watumiaji wengi wa laptop kutumia zaidi smatifoni kutokana na smatifoni kuwa na uwezo mkubwa unaokaribia laptop.
Kampuni inayoongoza kwa kutengeneza na kusambaza smatifoni ulimwenguni ya Samsung imezindua simu ya kwanza ulimwenguni Samsung galaxy S8 itakayokuwa na uwezo kwa kutumika kama "desktop computer" na hii itaongeza moto mkali kwenye maisha ya laptop.
Vijana wengi wamekuwa wakitumia zaidi smatifoni kwa sasa ukilinganisha na utumiaji wa laptop hivyo ununuaji wa laptop unategemewa kupungua sana katika miaka ijayo na kuifanya laptop kufutwa kwenye sura ya dunia.
Ijapokuwa Smatifoni zinaonyesha dalili zilizo wazi kupiku laptops lakini bado itakuwa ni ngumu kuifuta kabisa kwenye uso wa dunia kwani bado zipo kazi ambazo smatifoni haitaweza kufanya ikiwa peke yake bila ya msaada wa "peripherals" husika.
Nawasilisha ,
Article.