Laptop ya kununua kwa bajeti isiyozidi 950k

FUTURE HUNTER

JF-Expert Member
Apr 30, 2018
2,022
2,591
Salaam wana jamii tech,

Naombeni ushauri ni laptop gani Brandnew naweza pata kwa bei isiyozidi 950k ambayo ina vigezo hivi
RAM 4GB
PROCESSOR COi 3 walau kuanzia generation ya 6
HDD kuanzia 500gb
Nimejaribu kupita mitandaoni bei zimechangamka sana alafu nyingi ni refurbished.
Matumizi yangu ni ya kawaida sana sina heavy duty work.Nitashukuru nikiweza elekezwa na maduka yenye bei nzuri kwa kariakoo maana nina mpango kuja kununua huko baada ya kukosa hapa dodoma.

Nashukuru kwa ushirikiano wenu pia niko tayari kupokea ushauri mbadala ilimradi niweze kupata kitu kizuri.
Chief-Mkwawa na wengine wote ushauri wenu ni muhimu hapa
 
Tunachokosea kwenye PC ni kuweka vitu vingi ambavyo ni unneccessary kwa purpose ya PC yako na kutokuondoa vitu tusivyovihitaji kwenye PC au vilivyopitwa na wakati. PC nyingi tunazotumia ni above our purpose kwa wengi wetu.

Unakuta mtu ana application kama 4 zote za purpose moja. Mfano unakuta mtu ana google chrome, Mozila Firefox, Opera Mini, safari na Microsoft edge kwenye PC moja. PC hiyo hiyo ana pdf reader kibao, foxit, adobe, nitro na microsoft pdfkwa w10, unakuta ana window media player, Image viewer, Videos and Movies na VLAN vyote ndani ya PC moja! Yaani!
 
Salaam wana jamii tech
Naombeni ushauri ni laptop gani Brandnew naweza pata kwa bei isiyozidi 950k ambayo ina vigezo hivi
RAM 4GB
PROCESSOR COi 3 walau kuanzia generation ya 6
HDD kuanzia 500gb
Nimejaribu kupita mitandaoni bei zimechangamka sana alafu nyingi ni refurbished.
Matumizi yangu ni ya kawaida sana sina heavy duty work.Nitashukuru nikiweza elekezwa na maduka yenye bei nzuri kwa kariakoo maana nina mpango kuja kununua huko baada ya kukosa hapa dodoma.
Nashukuru kwa ushirikiano wenu pia niko tayari kupokea ushauri mbadala ilimradi niweze kupata kitu kizuri.
Chief-Mkwawa na wengine wote ushauri wenu ni muhimu hapa
Piga simu 0718 372 227 utapata
 
Sasa huna heavy duty, unapeleka wapi 4GB, 500GB na Co i3, 6th generation? Hiyo ni heavy duty tayari. Na umesema kuanzia. Of course kwa 950k utapata. Nenda Kariakoo utapata.
Ndio nimesema niko tayari kwa ushauri mbadala mkuu
 
Jaribu kuchek computer gallery, wapo mtaa wa jamhuri karibu na petrol station ya Puma au computer vision morogoro road karibu na kisutu BRT station, wanauza bei rafiki na warranty ni 1 year
asante kwa hint.nitawatafuta
 
Tafuta i3 gen ya 10 ama 11 zina nguvu kushinda i7 gen ya 7.

Zinaishiwa na G1 ama G4 kwa mbele, mfano

I3 1005G1
I3 1115G4

Nimeona nyingi hizo gen ya 10 mtaani mpya around 900k.
Asante sana chief.Hamna maduka unayajua ili nipitie kwa urahisi
 
Ingia instagram wacheki computer bei poa.
Hao naona niwakweli na zao bei ni halisi kutokana na kitu. Ukiwapata wape spacification alizokupa chief mkwawa hapo. Waambia unataka pc design hiyo mpya.
Asante mkuu.nimewacheki sema naoana nyingi bei zake ni milioni na chenji juu aisee
 
Asante mkuu.nimewacheki sema naoana nyingi bei zake ni milioni na chenji juu aisee
Za milioni nyingi ni zile zenye gpu ndani ya nvidia.
Hizi za kawaida zinacheza humo humo. Kama kuna namba pale watumie hizo spacification za chief. Waweza kuta wanazo.

Au ongea na Chief-Mkwawa siku akiwa free akupige tafu uende nae kutafuta town waweza mpoza ya kumpotezea siku ila ukapata kitu kizuri (wazo tu)
 
Back
Top Bottom