peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 12,793
- 21,367
Kumekuwepo na usiri mkubwa , kwenye sakata la wizi wa laptop computers 10 uliofanyika shule ya Moshi Technical kule kilimanjaro, ambapo shule hii Ina kitengo maalumu cha wanafunzi wenye matatizo ya kutokusikia vizuri. Hii ni mara ya pili kufanyika kwa wizi huo ndani ya mwaka mmoja.
Kimsingi mkuu wa shule hiyo ameshindwa kuisimamia shule hiyo kongwe nchini kutokana na kukosa uzoefu wa kazi hiyo sambamba na kukosa ushirikiano na afisaelimu sekondari wa Moshi mjini. Kutokana na kukidhiri kwa wizi huo, afisaelimu sekondari moshi manispaa na mkuu wa shule hiyo wamegoma kutoa ushirikiano katika utatuzi na upatikanaji wa computer hizo.
Tunashauri taasisi muhimu za uchunguzi zifanye uchunguzi wa kina na mkuu wa shule na afisaelimu sekondari moshi manispaa wapishe uchunguzi. Ili haki iweze kutendeka. Pia ikumbuke kuwa shule hiyo ilifanyiwa ukarabati za zaidi ya Tsh billion moja ambapo hakuna value for money.
Na mhasibu wa shule hiyo, alivyomaliza ukarabati wa shule hiyo ,alihamishiwa shule nyingine kongwe iliyoanza tena kukarabatiwa kwa Tsh 900milion. Kwa mantiki hiyo kuna mlolongo mkubwa wa upigaji wa fedha za umma na wizi wa mali ya umma ndani ya shule hiyo.