Nyama Hatari
JF-Expert Member
- Apr 11, 2008
- 219
- 12
Nyie mlio elimika mbona hamkuuliza sisi tunaoishi hapa kwa nini tunaona hii habari ina mapungufu mpaka tumesema hivyo?? Kwa taarifa yako sio tu kwamba habari na misingi ya kesi yenyewe inaacha maswali mengi bila majibu; bali hata hao walimsaidia huyu dada TAWA nao wana maswali ya kujibu…ndio maana nimeuliza kati ya hizo 56,000 victim mwenyewe Elizabeth amepokea kiasi gain? Unaweza kunipa jibu mkuu wewe uliyeelimika, ndio nyie mnaoamini 100% kila kitu kama kilivyoandikwa achieni wengine wanaoweza kusoma between the line.
I know better to say what I said na bado nasema tena, huyu dada amefundishwa kusema hayo aliyasema. Angalia taratibu za kupata visa ya domestic worker UK then uje nikuelimishe kwa nini hii kesi ina walakini. Kwa kuongezea, UK ni nchi inayoongozwa na Sheria ukiwa makini unaweza kunufaika na Sheria hizi kama ambavyo naamini kwenye hii kesi kuna watu wamenufaika.
Fairplay,
Kama unaamini kuna wabongo wamejilipua UK kwa michongo..kwa nini unashindwa kuamini kuwa hii kesi inawezekana ni mchongo pia. Jambo usilolijua waulize wenyeji badala ya kujifanya mjuaji.
Kwanza, ni mapungufu gani ambayo habari hii inayo? hebu tuambie basi. Pili, ni maswali gani hayo "mengi" ya kujibu? Tuorodhoshee moja hadi lingine. Tatu, tafadhali "tuelimishe" jinsi ambavyo kesi hii ina "walakini" vis-a-vis taratibu za maombi ya visa za mfanyankazi wa nyumbani.
Hata kama kiasi fulani cha compensation ya pauni 56,000 aliyotunukiwa huyo dada ingetumika kwa gharama za kuendesha kesi au mambo mengineyo, la msingi ni kwamba madai ya mlalamikaji yamefanikiwa kushinda mbele ya sheria ya UK.
Kwa kumalizia, kama unafahamu kwa kinaga ubaga undani wa kesi hii hadi kudai kwamba kesi hii ni "mchongo", basi tufahamishe vipingamizi vyako dhidi ya mlalamikaji kushinda hii kesi na siyo kutuletea argument za kipuuzi za dizaini ya "wabongo kujilipua UK kwa michongo".