Land Rover Discovery 4 - Mega thread

Mdudu namuelewa sana huyu kakaa kiume mno..
Screenshot_20190106-030547.jpeg
 
Wakuu kuna hawa jamaa wa arusha waitwa capitalzone wanatengeneza landrover 110 mnawaonaje? Na je? Vile vifaa wanavyotumia ni genuine? Mfano engine na vingine kwenye gari..
 
Wakuu kuna hawa jamaa wa arusha waitwa capitalzone wanatengeneza landrover 110 mnawaonaje? Na je? Vile vifaa wanavyotumia ni genuine? Mfano engine na vingine kwenye gari..
Vifaa ni genuine kutoka Land Rover, wao wanafanya kazi ya kufufua gari kuukuu na kurejesha katika hali nzuri.
 
Wabongo bwana gari kama sio toyota kwao ni shida ,kueni wazi mnaozikosoa zinasubua nini sio mnasema tu nimbovu
 
Mkuu dengue nunua hiyo gari mimi navutia tela nabeba trekta 165Fm au 135mersey ferguson toka mpumalanga mpaka mbeya na haili mafuta na ina nguvu sana ni disco 3 v 6 ina uzito tani 3 halijawahi kusumbua na mwezi huu linatoka tena na trekta kama kawaida...nipm namba nikutumie picha uitume hapa naona mm hapa inasumbua... d 4 mapumziko yamezidi zaidi hizo gari ukiona dereva kafanikiwa kuipindua matairi manne yote yawe juu unapata zawaidi kwa kupelaka hiyo picha Johannesburg Landrover photoshop wataijua...


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani mimi naomba mnisaidie. Naona serikali yetu inazima ndoto za wengi kumiliki usafiri. Yaani kodi hazishikiki kabisa. Kitu kingine...gari inavyozidi kuwa mpya ndo inazidi kuwa na ushuru mkubwa wakati nilifikiri kinyume chake kwamba serikali ita kuwa ina encourage watu wanunue magari ya miaka ya karibuni kulinda mazingira. Lakini leo ukisema ulete gari ya 2017 au 2018 au 2019..Kodi yake ni kizungumkuti. Kwa nini?
 
Jamani mimi naomba mnisaidie. Naona serikali yetu inazima ndoto za wengi kumiliki usafiri. Yaani kodi hazishikiki kabisa. Kitu kingine...gari inavyozidi kuwa mpya ndo inazidi kuwa na ushuru mkubwa wakati nilifikiri kinyume chake kwamba serikali ita kuwa ina encourage watu wanunue magari ya miaka ya karibuni kulinda mazingira. Lakini leo ukisema ulete gari ya 2017 au 2018 au 2019..Kodi yake ni kizungumkuti. Kwa nini?
Bado serikalini kuna fikra na mitazamo ya kijamaa: kwamba kumiliki gari ni ufahari. Hivyo, kuwekwa kwa kodi nzito nzito kwa kufikiria kwamba wamiliki magari ni watu matajiri sana.
 
Usijaribu kununua discovery utaliuguza kila siku. Hayo magari ni spana mkononi, safari moja shamba nyingine garage.

Ni magari mazuri kwa muonekano na nguvu ila hayafai yanaharibika kila siku. Kuhusu mafuta hayanywi yanabugia, ukiongelea discovery unaongelea cc4300 na zaidi, si mchezo. Labda yapo yenye uwezo mdogo fuatilia. Ushauri wangu usichukue discovery.

Nyie sijui hizi maneno mnatoa wapi..?? Mnakaa vijiweni sana bila shaka !!

Kwann ya cc 2700 si discovery ?
 
Kwa kuwa nimeendesha zote hizo mbili kwa kweli Touarag VW ni nzuri na imeipita mbali kwa usalama wa uendeshaji wa discovery
Don't get me wrong, hata land rover ni gari nzuri na zote nimebahatika kuendesha tena za 2018 ( zimeshatoka huku niliko)

Touareg imetulia sana na features zake ni sawa na discovery ila kuna extra zimo kwenye VW
Kwa mfano ukikata kona na taa zinamulika unakopita bit of a trick yaani taa zinageuka amazing
Pia cruise control inakuja kama standard yaani hulipii kama extra

All in all VW iko juu zaidi na sio rahisi pia
Bending lights....hiyo tech ipo kwenye Volvo kitambo....
 
Tatizo mafundi wetu nao wanawadanganya sana watu.. ooh hiyo gari mbovu, sijui injini kimeo.. kumbe wao ndio wako nyuma kiteknolojia na wamezoea garage zetu za chini ya mwembe zinazotengeneza 109 za carburetor.
Siku hizi gari full umeme, mafundi jiendelezeni jamani.
By the way, disco 4 ni mwisho wa njia, sema spea zake sio nyingi na mafundi pia wachache, hivyo ikiharibika ujiandae na mpunga wa kutosha kupata spea nyingine..
Daaah hiyo 109 ndio gari yangu ni V8 engine,nimefunga gearbox ya R380 ni moto mwinginee aisee
 
bobtony Mungu ni mwema utapata tuu na pia zinapungua bei kila miaka inavyokwenda ila Disco 3 sio ghari ni rand 100,000 mpaka 150,000 kama Tsh 16,000,000 kununua tuu mpaka 20milion ila kodi ipo 24milion kwa boda maana hakuna gharama za bandari na viingereza vingine tena na ya 2005 model mpaka 2007 model ndio zipo bei hizo mbele zaidi zipo bei juu...
Land Rover Defender haijawahi kutoka akilini Mwangu. Sidhani Kama kuna off-roader Bora zaidi ya Defender original ( acha hizi new model zao)
 
Kibongo bongo kati ya discovery 3 au vw toureg v6?
Kwa upande wa ulaji mafuta, uimara yaani ambayo haisumbui mara kwa mara na upatikanaji wa spares.

Pia VW Toureg za UK nyingi ni TDI diesel engine (3000cc) wajuzi tofauti ya hizi na hizi nyingine za Petrol (3200, 3500cc) ni nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom