Lamine Moro ateuliwa kuwa Captain mpya wa Yanga

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,714
45,098
Hatimaye klabu ya Yanga ambayo haina kocha, imemteua beki kisiki Lamine Moro kuwa Nahodha mpya wa kikosi hiko.

Bakari Mwanyeto pamoja na Mukoko watakuwa manahodha wasaidizi.

Nini maoni yako juu ya uteuzi huu? Nini hatima ya Haruna Fadhili Hakizimana Niyonzima ambaye amevuliwa unahodha klabuni hapo?
 
Hivi hujui mwenyekiti wetu naye ni kocha? Sasa unasemaje timu ya wananchi haina kocha!
 
Utopolo ni kama binti anayebalehe kwa kutafuta kiki,akipita mbele za wanaume wengi lazima atingishe wowowo aonekane.Hawamsubiri hata kocha yaani timu haipo organized wanajiamulia tu.

Wakati ule hamna kocha wao wameshasajili wachezaji wote ,leo wamemfukuza wanamteua nahodha mpya wakati wanasubiri kocha mpya
 
Only in Tanzania
Kwa nini ? timu za Ulaya macaptain wanapatikanaje kama ingekuwa hivyo si kila kocha akija atahitaji kuwa na Captain wake. Kubali au kataa mchakato wa kumpata Captain una mambo mengi sio lazima kocha ateue hata wachezaj some time wanapigiana kura, au uongozi wa timu unaamua tu mtu fulan basi.
 
Wanastahili! Inakuaje uwe na manahodha ambao hawana uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza?

Kama huyo Niyonzima mwenyewe tangu aoe mke wa pili wa Kibongo, ndiyo amekua urojo urojo tu. Lamine Moro ni kazi kazi yule! Mukoko naye ni mchezaji mwenye hamasa uwanjani.

Mwamnyeto naye ana uhakika wa kuanza kwenye kikosi cha kwanza! hivyo amestahili pia kuwa nahodha msaidizi. Hivyo Deus Kaseke na huyo Niyonzima watusamehe tu kwa sasa.
 
Back
Top Bottom