Lameck Ditto Moyo Sukuma Damu hadi Nabembea

kambitza

JF-Expert Member
Jul 24, 2013
2,045
1,308
Nabembea

Wanamuziki wachache wenye vipaji nchi hii ni pamoja na huyu kijana Ditto

Ukimsikiliza nyimbo zake ni kama kilevi kinacholevya taratibuuuu anakuchukua kidogo kidogo ukija kushtuka umelewa njwiiiiii

Kama ile Moyoo sukuma damu si vingineeee ilipotoka hadi leo haijaisha, Sasa hivi amenimaliza kabisa na huu wimbo wake mpya bado nabembeaaa nipo hewaniiii nabembea.

Wimbo umetuliaaaaa mashairi, mapigo ya muziki inanikumbusha Soccer Rhumbaaa Dittto weweeee ni balaa ila bahati mbaya kwako ni kuzaliwa kipindi hiki tu cha makiki na maskendo kushika hatamu ya kuufanya wimbo uwe mkubwa shiiiiiiiiiiiiit

Kuna waimbaji wanatoa vinyimbo vibayaaaa vinakuzwa na skendo na kiiikiiis za kipuuzi tu ile isingekuwa hivyo usingeshikika

Huu wimbo nimeupenda sana
 
Japokuwa mimi sio mshabiki wa Bongo flavour, ila kiukweli huyo jamaa anaweza. Ni mkali. Tungo, Sauti, Melody, Rhythm, Swaga, Video nk. viko sawia kabisa katika hiyo nyimbo yake.
 
Aisee nabembea ndiyo nimeusikia juzi atiiiii!
Nipo nyumaa kwelikweli ila huyu,.
Ditto ni fundi aisee!
 
Back
Top Bottom