Lambert ang’aka bungeni, mtambo wa Barakoa MSD ulivyoitia hasara Serikali

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994

Lambert ang’aka bungeni, mtambo wa Barakoa MSD ulivyo itia hasara Serikali​

Mtanzania
May 12, 2021

Mbunge wa Viti Maalumu Agnesta Lambert, akichangia bungeeni jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mbunge wa Viti Maalumu Agnesta Lambert amesema mtambo wa kutengeneza barakoa ulionunuliwa na Bohari ya Dawa nchini (MSD) kwa zaidi ya Sh million 600 umeonekana kuitia hasara Serikali kwakuwa imeshindwa kutimiza malengo.

Aidha, mbunge huyo amesema kuwa serikali ilinunua mtambo huo kwa lengo la kuzalisha barakoa millioni 4 kwa mwezi lakini cha kushangaza mtambo huo mpaka septemba mwaka Jana ulizalisha barakoa 320,000 badala ya malengo yao ya kuzalisha barakoa 504 kwa mwezi.

Lambert aliyasema hayo Mei 11, 2021 bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto iliyowasilishwa Jana.

“Naiomba Serikali ifanye Uchunguzi wa kina kuhusiana na ununuzi wa huo mtambo wa kutengeneza barakoa wa MSD, tumenunua kwa pesa nyingi lakini cha kushangaza mtambo huo umekuwa ukizalisha chini ya kiwango,” amesema Lambert.

Aidha, Lambert alisema yeye amejikita katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) iliyosema mtambo ulionunuliwa kwa pesa nyingi lakini umeshindwa kukidhi malengo kusudiwa.

“Kwa mujibu wa ripoti ya CAG baada ya MSD kuona mtambo huo unashindwa kuzalisha idadi ya barakoa tarajiwa waliamua kununua compressor nyingine ambayo hata hivyo haikuweza kuzalisha barakoa walizokusudia Jambo lililopelekea wananchi kukosa barakoa za kujikinga dhidi ya Corona,” alisema Lambert.

Lambert alisema kutokana na sintofahamu hiyo, ameitaka Serika kufanya Uchunguzi wa kina,kujua kama kweli mtambo huo ulinunuliwa kwa pesa hiyo.

Aidha Mbunge huyo ameitaka Serikali kulipa deni la Sh billioni 256 wanalodaiwa na MSD ili waweze kuagiza dawa.

“Serikali imekuwa na usugu wa kulipa madeni ya MSD, bajeti iliyoidhinishwa mwka 2019,2020 ilikuwa Sh bilioni 200 lakini Serikali haikupeleka hata shilingi moja, hali inayopelekea MSD kushindwa kununua dawa na Vifaa tiba jambo linalohatarisha maisha na afya za Watanzania alisema Mbunge huyo.
 
Bunge letu ni la watu wapuuzi na wanafiki wakubwa!

Kwanini asianze na hoja ya hasara ambayo wao wanatutia kwa kugawiana magari ya kifahari kila baada ya miaka mitano na kulipana jumla ya mishahara na marupurupu ambayo sio proportional na uchumi wa nchi yetu
 
Maccm ni majizi wakubwa.
Tunapigwa kila mahali

Nalog off
 
Afande pale MSD ni shida tupu!!! Kazi yake ni kusikiliza majungu tu ya akina Robert Biah ambae ameshindwa kuitumia taaluma yake ya ukaguzi ipasavyo na ku-dwell kwenye kufitini tu wafanyakazi unnecessarily!

Afande achana na vijitu kama vya akina Frank Nkone, wanakupoteza!!
 
Bunge letu ni la watu wapuuzi na wanafiki wakubwa!

Kwanini asianze na hoja ya hasara ambayo wao wanatutia kwa kugawiana magari ya kifahari kila baada ya miaka mitano na kulipana jumla ya mishahara na marupurupu ambayo sio proportional na uchumi wa nchi yetu?
Hapo atakuwa hajapewa posho
 
Bunge letu ni la watu wapuuzi na wanafiki wakubwa!

Kwanini asianze na hoja ya hasara ambayo wao wanatutia kwa kugawiana magari ya kifahari kila baada ya miaka mitano na kulipana jumla ya mishahara na marupurupu ambayo sio proportional na uchumi wa nchi yetu?
Nireteeni Ngwajimaaaaaa...........
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Twende taratibu...lifespan ya huo mtambo ni muda gani? Na Wao wameplan kua by what time ndo watapata ROI yao? So far kwa barakoa walizotengeneza 320,000 km wanauza 500 washatengeneza 160m..which is not that bad...huwezi tengeneza barakoa 4m km hakuna soko, una produce according to the demand( Rule of demand and supply).
Wabongo wenyewe kuvaa barakoa tu ni mtihani. Hapo inabidi watoke maofisini waende wakatafte soko ktk inchi jirani, wakitegemea soko la ndani watatengeneza izo 4m per month then watazima mitambo for the following month wakisubiri ziishe kwanza.
 
Afande pale MSD ni shida tupu!!! Kazi yake ni kusikiliza majungu tu ya akina Robert Biah ambae ameshindwa kuitumia taaluma yake ya ukaguzi ipasavyo na ku-dwell kwenye kufitini tu wafanyakazi unnecessarily!

Afande achana na vijitu kama vya akina Frank Nkone, wanakupoteza!!
Robert si ameshastaafu tayari, au? By the way hoja za ukaguzi sio majungu kwa kuwa hoja huibuliwa tokana na kanuni za utendaji zilizotungwa.
Mara nyingi wakaguzi wengi huonekana wanapiga majungu kwa kuwa wakaguliwa huwa hawapendi mapungufu ya kiutendaji yawekwe bayana, mwisho wa siku mkaguzi naye anayo kazi ya kutoa ripoti ambayo ndio hasa inayoelezea hoja zinazohitaji majibu, Majungu sio proffesional na ni mjinga tu atasikiliza.
 
Haya maumivu ukisoma ni 😭 😭 watu wanacheza na ela ya serikali kama wanachezea chenji zao za mifukoni .
 
Haya mambo ndo maana watu tunaona hela za tozo watu watazipiga tu leo huko waziri mkuu analia na mtu kajenga barabara km 1.8 kwa bilion 5 na ushee huku kuna tena milion 600 kuna siku tutachoka tutaingia mtaani maana hela yetu mnaichezea sana.
 
Lambert ang’aka bungeni, mtambo wa Barakoa MSD ulivyo itia hasara Serikali​

Mtanzania
May 12, 2021

Mbunge wa Viti Maalumu Agnesta Lambert, akichangia bungeeni jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mbunge wa Viti Maalumu Agnesta Lambert amesema mtambo wa kutengeneza barakoa ulionunuliwa na Bohari ya Dawa nchini (MSD) kwa zaidi ya Sh million 600 umeonekana kuitia hasara Serikali kwakuwa imeshindwa kutimiza malengo.

Aidha, mbunge huyo amesema kuwa serikali ilinunua mtambo huo kwa lengo la kuzalisha barakoa millioni 4 kwa mwezi lakini cha kushangaza mtambo huo mpaka septemba mwaka Jana ulizalisha barakoa 320,000 badala ya malengo yao ya kuzalisha barakoa 504 kwa mwezi.

Lambert aliyasema hayo Mei 11, 2021 bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto iliyowasilishwa Jana.

“Naiomba Serikali ifanye Uchunguzi wa kina kuhusiana na ununuzi wa huo mtambo wa kutengeneza barakoa wa MSD, tumenunua kwa pesa nyingi lakini cha kushangaza mtambo huo umekuwa ukizalisha chini ya kiwango,” amesema Lambert.

Aidha, Lambert alisema yeye amejikita katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) iliyosema mtambo ulionunuliwa kwa pesa nyingi lakini umeshindwa kukidhi malengo kusudiwa.

“Kwa mujibu wa ripoti ya CAG baada ya MSD kuona mtambo huo unashindwa kuzalisha idadi ya barakoa tarajiwa waliamua kununua compressor nyingine ambayo hata hivyo haikuweza kuzalisha barakoa walizokusudia Jambo lililopelekea wananchi kukosa barakoa za kujikinga dhidi ya Corona,” alisema Lambert.

Lambert alisema kutokana na sintofahamu hiyo, ameitaka Serika kufanya Uchunguzi wa kina,kujua kama kweli mtambo huo ulinunuliwa kwa pesa hiyo.

Aidha Mbunge huyo ameitaka Serikali kulipa deni la Sh billioni 256 wanalodaiwa na MSD ili waweze kuagiza dawa.

“Serikali imekuwa na usugu wa kulipa madeni ya MSD, bajeti iliyoidhinishwa mwka 2019,2020 ilikuwa Sh bilioni 200 lakini Serikali haikupeleka hata shilingi moja, hali inayopelekea MSD kushindwa kununua dawa na Vifaa tiba jambo linalohatarisha maisha na afya za Watanzania alisema Mbunge huyo.
Katika Maelezo yake kama amejijibu kwa nini lengo halifikiwi. Kama msd inaidai serikali inawezekana haina hela za kutosha za kununua Mali ghafi. Kutofikia lengo inachangiwa na sababu nyingi sana.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom