Fahamu namna ya kutengeneza lamba lamba za matunda

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
264,052
1,075,461
LAMBA LAMBA ZA PARACHICHI NA MAZIWA :
Mahitaji:
Parachichi 1 kubwa kiasi 1/2

kikombe cha sukari Kopo 1 kubwa

maziwa mepesi ya ( LUNA EVAPORATED MILK ) 1/2 kikombe maji

Maelezo: Katika bakuli kubwa, changanya iliyosagwa parachichi, sukari,maziwa, na maji. Koroga mpaka sukari iyeyuke kabisa. Ongeza sukari zaidi kama ni lazima. Kumbuka kwamba utamu utapungua mchanganyiko ukiganda. Jaza mchanganyiko katika mifuko au vikopo na weka na vijiti katika vikopo. Gandisha katika freezer masaa 4 hadi 6. Baada ya hapo tayari kuliwa.
IMG_20190821_033030.jpg
MAZIWA YA KOPO YA LUNA YANAPATIKANA MADUKANI NA SUPER MARKETS. Enjoy

source Instagram
 
MANGO ICE CREAM / LAMBA LAMBA ZA EMBE :

Maembe 3 makubwa

Mtindi wa vanilla au wa kawaida vikombe 5

Sukari kiasi chako

Maelezo:
Menya embe katakata vipande vidogo vidogo na mimina katika blender. Weka na Mtindi na Sukari. Saga mpaka iwe laini kabisa. Mimina mchanganyiko katika vikopo vya ice cream. Gandisha katika freezer muda wa masaa 6 au 8. Baada ya hapo lamba lamba za embe tayari kuliwa.
IMG_20190821_033020.jpg
Enjoy
 
Wale wakujaribu jaribu vitu vipya hatukawii kusaga na viazi halafu tugandishe tuone itatokea nini.
 
Maziwa haya ya kawaida haiwezekani kutengezea? Au ni lazima niwe na maziwa y LUNA
 
Lambalamba ya embe umesema maembe matatu na mtindi vikombe vitano,swali kwa haya maembe matatu na vikombe 5 vya mtindi naweza kupata lambalamba ngapi?
 
Lambalamba ya embe umesema maembe matatu na mtindi vikombe vitano,swali kwa haya maembe matatu na vikombe 5 vya mtindi naweza kupata lambalamba ngapi?
Naona unalivalia njuga ilo swala,ukifanikiwa utuite tujilambe
 
Kwa wahitaji wa popsicle mould mje nauza 6 ina matobo manne na sita
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom