Lakini kwanini ?

uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,700
1,415
Hivi kwanini gari za polisi zinaendelea kuitwa 'difenda' huku nyingi siku hizi zikiwa Landcruiser ?

Hivi kwanini vituo vya mafuta vinaitwa ''sheli' huku tukifahamu kampuni ya Shell haipo nchi ?

Hivi kwanini simu za mkononi vijijini wanaziita 'nokia' hata kama ni kampuni ingine ?

Hivi kwanini watu husema barabara ya Morogoro road hata kama barabara maana yake ni 'road' ?

Hivi kwanini ukitaka kushuka kwenye daladala ambapo hamna kituo useme 'msaada' mbona kupanda wanasimama popote ?

ongezeni zingine.

hivi kwa nini mtu bado anajikakamua kuishangilia arsenane wakati ilishapigwa nane.

sio kwenu tu! Hata huku kwetu wapo. eti peni wanaita biki, hata kama ni aina nyingine ya peni

hivi kwa nini mtu bado anajikakamua kuishangilia arsenane wakati ilishapigwa nane.

Hivi kwa nini mtu anaendelea kuishangilia barcelona wakati ilishawahi kuzabwa 11-1 na Real Madrid?

Hivi kwanini kalamu wanafunzi wanaziita bic wakati bic ni jina la kampuni ya kutengeneza kalamu za wino nchini kenya?Hivi kwanini dawa ya kung'arishia kiatu mnaita kiwi wakati kiwi ni jina la mojawapo la kampuni zinazotengeneza dawa za ku-shine viatu?

Hivi kwa nini wao bado wanajiita wazanzibar wakati tanganyika ilikufa na zanzibar.au ni ule mchezo wa tule chako kwanza changu baadae halafu unalala mbele?

hiv kwann magari madogo hku vijijini wanayaita vitaksi wakati taksi ni gari zozote zinazotoa huduma za usfr wa haraka na kwa nini mabasi wanayaita coaster wakati coaster ni magari ya toyota

Bukta is a sports clothing brand which was founded in 1879...lakini mpaka leo kaptura yoyote inatupiwa jina la bukta?...hata kipande cha jinsi..lmao!!

lakini pia watu shoprite wakimaanisha supermarket yoyote, wakati shoprite ni jina la supermrket...

hivi kwanini gali ya kusafirisha abiria inaitwa dala dala wakati nauli ya dala ishapitwa na wakati!

Hivi kwanini gari za polisi zinaendelea kuitwa 'difenda' huku nyingi siku hizi zikiwa Landcruiser ?

Hivi kwanini vituo vya mafuta vinaitwa ''sheli' huku tukifahamu kampuni ya Shell haipo nchi ?

Hivi kwanini simu za mkononi vijijini wanaziita 'nokia' hata kama ni kampuni ingine ?

Hivi kwanini watu husema barabara ya Morogoro road hata kama barabara maana yake ni 'road' ?

Hivi kwanini ukitaka kushuka kwenye daladala ambapo hamna kituo useme 'msaada' mbona kupanda wanasimama popote ?

ongezeni zingine.

nina ka nokia kadogo aina ya siemen, kazuri wewe.!

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom