Lakini DPP tulikushauri ufute hii kesi ya Mbowe haina uhalisia wowote

Mimi kama Wakili mkongwe ndani na nje ya nchi kwakweli sijawahi kushudia kesi yenye vituko na mikamganyiko mingi kama hii inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe na wenzeke.

Yaani Mawakili wa Jamhuri wanajichanganya wanaharibu mambo, mashahidi wanajichanganya hawaelewi ni wapi wanaenda na ni wapi wametoka, maaafisa wa mahakama nao inaonekana wameingia kwenye mambo haya. Yaani mambo ni shaghala baghala.Mbaya zaidi nao wamekutana na mawakili wa upande wa Utetezi nao wako makini sana na hii ndiyo shida inayowapata.

Mhe DPP bado unayo nafasi ya kutosha kuliepushia taifa letu na aibu inayoendelea sasa mahakamani. Ukisema usubiri mpaka mwisho huenda mambo yakaharibika zaidi.
Mmeona mmezidiwa mnakuja kwa njia nyingine ya kumlilia DPP. Hadanganyiki mtu. Hakuna kesi kuondolewa.

Kama mawakili wenu wazuri mna wasiwasi gani. Subirini mshinde kesi. Jiandaeni pia kupokea the worst scenario ya miaka 30 jela.
 
Kwa akili yako unaamini angekuwa hajafuta hadi leo kama mfukoni hawana ushahidi, ushahidi bado unaletwa. kesi hii ina macho hadi ya nchi za nje, wangeona ni ya kijinga wala wasingeendelea nayo, ukiona wameng'ang'ana, omba tu Mungu asamehe mwenyekiti, jua kuna ukweli na ushahidi upo. hivi unafikiri huyo dpp na timu yake yoote hawana akili? na hiyo ni kesi yao ya kwanza kufungua hapa nchin?
Mkuu rudia kusoma ulichokiandika. Kuna mhimili uliojichimbia zaidi kuliko mingine. Mizizi yake inatafunwa na mdudu, subiri anguko la pamoja na huyo dpp.
 
hatutaki kumuona mtu anaye panga mipango ya kuvuruga amani ya nchi yetu.
akae huko huko gerezani.
 
Mimi kama Wakili mkongwe ndani na nje ya nchi kwakweli sijawahi kushudia kesi yenye vituko na mikamganyiko mingi kama hii inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe na wenzeke.

Yaani Mawakili wa Jamhuri wanajichanganya wanaharibu mambo, mashahidi wanajichanganya hawaelewi ni wapi wanaenda na ni wapi wametoka, maaafisa wa mahakama nao inaonekana wameingia kwenye mambo haya. Yaani mambo ni shaghala baghala.Mbaya zaidi nao wamekutana na mawakili wa upande wa Utetezi nao wako makini sana na hii ndiyo shida inayowapata.

Mhe DPP bado unayo nafasi ya kutosha kuliepushia taifa letu na aibu inayoendelea sasa mahakamani. Ukisema usubiri mpaka mwisho huenda mambo yakaharibika zaidi.
Wewe "Wakili mkongwe", halafu usifahamu kwamba kesi hiyo si hao unaowataja kujichanganya?

Labda ungekazia zaidi kwenye hilo la wahusika wa kesi kujidhalilisha mbele ya macho ya wananchi na jumuia nzima ya kimataifa.

Ukipata muda, jaribu kujikita upande huo kwa udadavuzi wako.

Haya ya mashahidi, DPP, mapolisi, n.k.,hawa hawana la kufanya, bali kutimiza waliyoagizwa na walio juu yao. Na kama unavyoifahamu hali ya nchi yetu, wote hao wanaoagizwa hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kusimamia anachokiamini ndani ya dhamira yake, maana tumboni ndiko kunakotoa maamuzi yake, badala ya kichwani.
 
Na kati ya mawakili waliofeli kuwaajili, kibatala. kwanza hanaga hekima na professionalism ya sheria, ana hasira na analeta siasa tu. anawadanganya wengi ambao hawajui sheria na procedure za mahakamani kwa mambo ambayo hayaamui kesi na ndiyo wanayomshangilia nayo. subiri kesi iishe, si lazima itarushwa humu judgment yake.
eti kukata miti, eti maandamano yasiyoisha ni ugaidi. Labda kuna la ziada mbele, ngoja tusubiri. Angalia hii halafu ndipo ujue ugaidi ni nini. Tuombe yasifike huku kwetu, maana Dodoma itaonekana ndogo
Triple suicide bombers target Ugandan capital
 
Mkuu waambie hao wanafikiri watu wote hawana akili na Kibatala anawazingua tu hakuna la maana analoliongea humo mahakamani
Ha he vile vichina vyaako vingine vimiguu ka vya spoku utamuachia nani maana baragumu imrshapulizwa unahitajika bwana makalio makubwa
 
Humjui Kibatala. unamwona tu kwenye mitandao. sio wakili mzuri kama unavyofikiri. nasema hivi wazi kwasababu ndiye atakayemponza mbowe. mngefanya uchaguzi sahihi kwa mawakili mbona wapo wengi tu na wazoefu? labda kwasababu na yeye ni mwanachadema mwenzenu mliogopa kuzungukwa.
Punguwani wewe huelewi kitu
 
wewe ni mjinga unayeitakia tz mabaya, unatamani hayo yatokee dodoma? jaribu uone funza wewe.
Ndio magaidi eanavyofanya lakini wenye akili za funza kama nyie munadharilisha nchi kwa kesi za kuchongea kufarahisha matumbo yenu
 
Kwa akili yako unaamini angekuwa hajafuta hadi leo kama mfukoni hawana ushahidi, ushahidi bado unaletwa. kesi hii ina macho hadi ya nchi za nje, wangeona ni ya kijinga wala wasingeendelea nayo, ukiona wameng'ang'ana, omba tu Mungu asamehe mwenyekiti, jua kuna ukweli na ushahidi upo. hivi unafikiri huyo dpp na timu yake yoote hawana akili? na hiyo ni kesi yao ya kwanza kufungua hapa nchin?
Unastahili ku-chapwa kama kibaka
 
Na kati ya mawakili waliofeli kuwaajili, kibatala. kwanza hanaga hekima na professionalism ya sheria, ana hasira na analeta siasa tu. anawadanganya wengi ambao hawajui sheria na procedure za mahakamani kwa mambo ambayo hayaamui kesi na ndiyo wanayomshangilia nayo. subiri kesi iishe, si lazima itarushwa humu judgment yake.
Yaani mambo yanayoamua kesi eti Kibatala asijue wewe kikaragosi ndio ujue.

Kesi feki kama hii huwezi ukamlaumu wakili wa utetezi kwa sababu haiamuliwi kwa kufuata misingi ya sheria ila matakwa ya utawala.
 
Hata kama wana ushahidi dhidi ya hii kesi lakini aina ya ugaidi wanao tuhumiwa nao sio ugaidi unaojulikana na dunia.
Labda tuseme ni ugaidi wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom