Laki tano tu unaweza badilisha historia

Wakuu....

Hata km laki 5 haitoshi, mleta mada katoa somo hapa.....

Endeeleeni kutafuta milion 10 ndo muwekeze
Sawa kabisa,acha waendelee kuisubiri million10 ndo wawekeze,mtu huwezi kuwekeza hela nyingi kwenye vitega uchumi vyako kama huwezi kuwekeza hela kidogo kwa ideas mbalimbali,hapa uliloambiwa changanya na akili zako
 
Dah.....harakati za kitambo sana hizi...kilimo cha whatsapp.... Enhe tuambiane waliotoboa waje watupe mrejesho. Na wale wa vitunguu pia mje.
 
Laki tano, Mshahara wa Ma-Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya TECNO PHANTOM mpya kabisa kwa kujishau Snapchat na Istagram Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya SUBARU mwezi Mzima.... Laki Tano , Bajeti ya HEINEKEN 100 KWA wanywaji wa Pombe... HELA FLANI MBUZI TU ambayo wengi wanaona HAINA ISHU .

Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji.

Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambal inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.

Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6 zaidi ya Mwanzo na Kuexpand Kipato chako mara 6 zaidi ya Mkupuo wa kwanza!

Laki Tano hii ina uwezo wa kulima Matikiti Maji Ekari 2 na zikakupa si chini ya Milion 2 na nusu baada ya SIKU 90!

SHIDA NI: Kila mtu anataka akae mjini AONEKANE SAMAKI SAMAKI, aonekane Muvi Mlimani City, Apost akiwa Escape 1, Apige Snapchat akiwa 777 ... Kila mtu anataka aonekane MDARISALAMA... Yuko mjini

MDADA yupo radhi aishi mjini kwa kuuza mwili wake kuliko kwenda Ruaha Mbuyuni Kuinvest kulima Vitunguu... Ataonyesha saa ngapi CROP TOP yake Mpya kutoka ROBY ONE FASHION? Sistaduu alime vitunguu?? Hapana, bora atafute Danga la Laki 2 akalale nalo!!

Big Up kwa wadada wote wajanja WALIOINVEST KWENYE KILIMO., kila Jumamosi wakati wewe unaona sifa kwenda NEW MAISHA na sehemu nyingine zinazofanana na hizo Wadada wenzako wako RUVU wamekodi mashamba wanalima mpunga, unashangaa Huyu mdada anafanya nini kumbe mwenzio analima.

HESHIMA kwa wanaume wenzangu ambao wamegundua siri kwamba kuuza Sura hakulipi ma wameinvest Shamba, kila weekend wanapotea kwenda kusimamia nyanya na pilipili Bagamoyo.

Utaendelea kuwashangaa wenzio wanatajirika na kudhani kila mtu anauza UNGA hapa mjini, Kilimo ndio unga mpya... nnadhani mkandamizaji amenuunua ile BMW X6 kwa episode za ORIJINO COMEDY? Thubutu, nenda MBARARI umkute amejaa Matope akipalilia Mpunga wake ndo utajua na wewe kwa nini unapanda Bajaji mpaka leo na kubaki kulalamika tu.

AMKA NAONGEA NA WEWE

Je laki 5 yako, unafanyia
70a9b6fc5d2ec1eb9e69893edf004d76.jpg
nini?
laki tano unakunywa bia na kumgegeda Tally hunter ndani ya hotel ya sheraton
 
Haya maandishi kwa mara ya kwanza niliyasoma kwa marehemu Seth, daah jamaa pumzike mahali salama huko alipo
 
Hii ilikuwa laki tano ya mwaka 2016.. vipi inflation huko thamani ya laki tano sasa iko vipi??
 
Ebu lete michongo make saizi ajira watu wanaingia wapya wale wa zamani ni majipu, hapo mpwapwa nikitaka kuanzisha kilimo cha tikiti nipe info je kuna maji ya kutosha kumwagilia? make kuna kipindi nilikwenda kule magugu nikakodi hekta 18 kwa ajili ya kilimo cha mpunga nilichokipata sina hamu tena na kilimo.
Mkuu niko mpwapwa maji ni mengi kuna mashamba mazuri na mito inayo tiririsha maji mwaka mzima na wenyeji hawajaamka sana,najishungulisha na kilimo huku nilikuja mwaka jana nnauzoefu wa kutosha kiasi cha kujua hzo laki tano hazitatosha tikiti heka 2 ila nizao linaloweza kustawi vizuri tu huku
 
Mkuu niko mpwapwa maji ni mengi kuna mashamba mazuri na mito inayo tiririsha maji mwaka mzima na wenyeji hawajaamka sana,najishungulisha na kilimo huku nilikuja mwaka jana nnauzoefu wa kutosha kiasi cha kujua hzo laki tano hazitatosha tikiti heka 2 ila nizao linaloweza kustawi vizuri tu huku
Uko mpwapwa sehemu gani??
 
Back
Top Bottom