Lake View School Mwanza mtawasabishia maradhi wanafunzi wenu

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,658
22,255
Tangazo la LAKE VIEW SCHOOL MWANZA linaonesha watoto wanafunzi wakiwa ndani ya bwawa la kuogelea huku wamevaa nguo zao!

Moja ya kanuni za mabwawa ya kuogelea ni kutoingia ndani ya bwawa ukiwa umevaa nguo za kutembelea, inaonekana shule ina bwawa lakini haina mkufunzi wa kuogelea jambo ambalo ni la hatari kwa usalama wa wanafunzi.
 
Bahati mbaya wazazi hawaoni kuwa shule inahatarisha afya za watoto wao, asilimia kubwa ya wazazi hao kama si wote hawajawahi kutumia bwawa la kuogelea na hatari iliyoko kwa mtoto aliyevaa nguo zake zote kuingia ndani ya bwawa, licha ya kuingiza uchafu lakini pia nguo zikilowa zinaongezeka uzito na maji yanaweza yakamzidi nguvu na kusababisha mtoto kuzama.
Ninawashauri wazazi wafuatilie mienendo ya watoto wao shuleni likiwemo tatizo la watoto kujazwa kupita kiasi ndani ya gari za shule jambo ambalo trafiki wanaona si tatizo.
 
Ngoja walete utani,
Wanadhani wanavua sangara,
Halafu sikuhizi matangazo ya shule nyingi yanalalia kwenye Starehe..
Katika mazingira hayo hata mtoto anaenda shule na dha a hio.
 
Back
Top Bottom