Laiti wangeweza nisikia, ningewashauri ccm wasisimamishe mtu kiti cha uraisi 2015 ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Laiti wangeweza nisikia, ningewashauri ccm wasisimamishe mtu kiti cha uraisi 2015 !

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EL MAGNIFICAL, Apr 5, 2012.

 1. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  sina maana kama wameshndwa kutawala na hata kama baadhi ya watu wataamini ivyo lakini sitaki kuamini moja kwa moja hata wao imani yao ipo hivyo kwamba wameshndwa japo kuwa tangu enzi za tanganyika matatizo yamekuwa yale yale kama umasikini, maradhi,ujinga na ubadhilifu wa mali ya umma.
  Ccm ni chama kikonge sana hapa nchini pia ndicho chama tawala mpaka leo hii nchi yetu imetimiza miaka 50 ya uhuru.
  Kwakuwa ikulu si mahala pa biashara na malengo ya vyama vyote vya siasa hapa nchini ni kushika dola na kuleta maendeleo kwa wananchi ningependa kuwashauli ndg zangu wa ccm wasimsimamishe mtu ktk kiti cha uraisi ktk kinyang'anyiro cha uraisi mwaka 2015 badala yake wajikite ktk chaguz za ubunge tu.
  Lengo ni kuvipa nafasi vyama vya upinzani navyo viweze kuunda serikali kuu na kuitawala hii nchi.
  Faida za kufanya hivyo ni pamoja na zifuatazo:-
  1. Ccm ikiwa kama chama kikongwe ktk bara la africa kitajitunzia heshima yake kikiwa ni moja kati ya vyama vikongwe ambavyo havijawai kudondoshwa ktk uchaguzi. Hapa sina maana kwamba 2015 ccm itadondoka wala sipo kishabiki bali ni ukweli usiofichika kuwa idadi kubwa ya watu wamepoteza imani na ccm ikiwa ndio chama tawala kinachoongoza serikali na kuamini ndicho chama kilichosababisha ugumu huu wa maisha uliopo.
  2.kuleta ushindani halisi ktk siasa kwa kuwapa watu uwezo mzuri wa kufanya utambuz ni serikali ipi ilikuwa lege lege. Haiwezekani ccm imekuwa madarakani miaka 50 halafu ushndani ifanye na vyama ambavya havijawahi kukaa madarakani hata mwaka mmoja.
  3. Ccm kitapata mda mzuri wa kujipanga, kujikosoa na kuondoa makundi ndani ya chama.
  4. Kitaweza pia kujisafisha kwa wananchi kwani kitapopata nafasi ya kuwa kambi rasmi ya upinzani mjengoni ni wazi nao watapata fursa kubwa ya kuikosoa serikali na umma utatambua nini wafanyacho.
  5. Itakuwa ni muda mzuri kwao kuzuia machafuko ambayo yamekuwa yakichipua chini kwa chini dhini ya wimbi kubwa la watu maskini ambao wamechoshwa na serikali yao.
  6. Pia kitapata muda mzuri wa kutambua na KUTAFUTA MAJAWABU YA MATATIZO YA WANANCHI.
  7. Pia itafanya umma utambue mapungufu ya wapinzani yapi wawapo madarakani. Hii itasaidia kutambua mwendokasi wa wapinzani ktk utendaji kazi.
  Kwa kuwa UJENZI NI WA NYUMBA MOJA SIAMINI KAMA KUNA UMUHIMU WA KUGOMBEA FITO.
  Siamini kwa miaka 50 kama bado watakuwa na uchu wa madaraka kiasi cha kunipinga kabisa.
  Nawasilisha.
   
 2. d

  dada jane JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hoja nzito ila sijui kama walipokea kwa kulitafakari kwa kina.
   
 3. Amanizzle

  Amanizzle JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Hongera, umejaribu kufikiri nje ya box.. Itakua ni zaidi ya demokrasia kama wakifuata ushauri wako mkuu..wataalam wa mambo ya siasa watatuambia ni aina gani ya demokrasia.
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Bado sana. CCM wana nafasi kubwa sana ya kuibuka washindi 2015 tena kwa kura nyingi sana zaidi ya zile za 2010. Fuatilia kwa makini ushindi wa Chadema katika majimbo yao, utagundua ujanja uliotumika. Si ushindi uliotokana na mvuto wa Chama. Tayari Arumeru wazee wameshajitokeza na kusema vijana wao waliwaibiwa shahada zao huku wakiongozwa na makada wa Chama, so hii inadhihirisha matatizo yanaweza kubaki pale pale, zaidi Chadema wametumia udhaifu wa uteuzi wa CCM jambo ambalo linaweza kurekebishwa. Sijaona Chama ambacho kinaweza kuunda serikali zaidi ya CCM kwa miaka 15 ijao kutokana na umafia wa vyama vya sasa, labda ADC kidogo jana nimesikiliza sera zao walipokuwa kuwa MWANZA.
   
 5. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  CCM Haiwezi kukubali ushauri wako wenye hekima kuu mkubwa!
  Akili yao ni ndogo mno!
  Ni sawa na kujaribu kumfundisha kuku kusoma!
  Japo lengo lako ni zuri,akili yake ni ndogo,ataishia kukudonoa!!
   
 6. kiroba

  kiroba JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu uchambuzi wako ni makini na umeeleweka vizuri sana.
  Tatizo hapa ni kuwa hayo ulioyasema si kama watawala hawayajui, bali wao lengo lao la kuingia ikulu ni kujilinda kwa kutumia kivuli cha serikali kwa mabaya waliofanya.

  Sasa kama watasikiliza ushauri wako ni kama vile watakuwa wameachia waadhibiwe kwa mabaya na maovu waliofanya. Unajua kinachoogopesha sana watawala wetu ni kuwa kama wakiwa nje ya serikali je watapata wapi mtetezi wa kuwakingia kifua kwa mabaya waliotenda?

  Kwa mtazamo wangu sidhani kama ushauri wako utawapendeza na wakaitikia wito wako. Kiujumla waliopo madarakani kwa sasa wana hofu kama serikali ya chama chao ikidondoka watakuwa wageni wa nani?
   
 7. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili ni janga, afadhali upofu wa macho kuliko upofu wa akili, afadhali kiwete wa miguu kuliko kiwete wa ubongo. Kama mpaka sasa hujatambua kuwa kuna mabadiliko, wenye akili tena waasisi wa CCM walishatabanahisha kifo cha chama chao hakika wewe ni sehemu ya R.I.P. CCM.
   
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  hivi unaweza kuwa na timu afu usiipeleke kwa hofu ya kumshinda mpinzani.

  Kama tunajifurahisha ni sawa kusapoti hii ila kiuhalisia haiwezekani.
   
 9. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  dada jane ndio maana nimesema laiti wangeweza kunisikia lakini hii ndio itaonesha jinsi gani kweli wanania ya kujivua gamba na si kuendeleza malumbano kati yao.
   
 10. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  inawezekana pia kikawa kitu kipyaa ktk anga la siasa pia wanaweza wakawa mfano wa kuigwa kwa vyama vingine vya siasa.
   
 11. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkuu sikatai kuwa ccm hawana nafasi ya kushnda, pia umesema hakuna chama cha upinzani kinachoweza kuongoza nchi lakini ujue wananchi ndio watakao pia pia kama watafail kutawala itakuwa faida pia kwa ccm kuludi kwa wananchi na kuwaeleza wapi na kwanini wapinzani wamefail hivyo imani kwa wana ccm itazidi kupanda.
   
 12. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkuu najua wanaweza wakafikili ushauri huu una lengo la kuwadhalilisha lakini hivyo thamani ya ushauri huu ni kama lulu za baadae.
   
 13. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkuu kiroba uyasemayo ni kweli kabisa lakini kadri wanavyozd kukaa madarakani ndivyo wanavyozd kutengeneza list ndefu ya watu wa kuja kuadhibiwa hapo baadae kwani sifikilii kama ccm watatawala milele.
   
 14. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkuu inawezeka isiwezekane lakini mwisho wa yote utakuwa mbaya siasa ni tofauti na michezo kwani michezo hujenga umoja baina ya wana jamii lakini siasa inaweza leta mpasuko ktk jamii hasa inapotumiwa vibaya au watu kuikosea uelewa kwa wakati huo.
   
 15. m

  mama-lokatare Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mawazo mazuri sana !
  lakini tatizo ni nani anayeambiwa !
   
 16. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  neno langu sio torati kwamba lazima litimie....! Kupuuza ni ruksa pia japo nilipenda nieleweke.
   
 17. S

  Son of slave Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina imani wamekusikia mkuu
   
 18. K

  Karry JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  wewe kama ulizamia meli na mtoa mada ndio utaona hakuna kilichofanyika kwa miaka 50, nchi imepiga maendeleo makubwa isipokuwa tunachangamoto ya ukuaji wa miji/idadi ya watu kwa kasi si rahisi kuona maendeleo ya mtu mmoja mmoja, CCM haiwezi kufa kamwe hizo ni dua za kuku
   
 19. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #19
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ushauri wangu ni mzuri japo kidogo unahitaji roho ngumu kuufanyia kazi tatizo huna mapenzi na chama chako ndio maana unahisi nimetukana.
   
Loading...