laiti viongozi na vijana wa chadema wangekuwa serious kama mpiganaji Julius Mtatiro wa cuf!!

Jospina

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Messages
2,420
Likes
253
Points
180
Jospina

Jospina

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2013
2,420 253 180
Julius Mtatiro ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Tanzania Bara.Nilikutana na Julius Mtatiro mwaka 2006 nilipojiunga UDSM.Tukio la kwanza llilonifanya kumfahamu zaidi Julus Mtatiro ni pale wanafunzi wa mwaka wa kwanza (baadhi) walipoamua kufanya mgomo kwa sababu ya kucheleweshewa fedha za kujikimu kutoka Bodi ya Mikopo.

Mtatiro akajitokeza na kuzungumza na wanafunzi kwa ujasiri na kuahidi kusaidia kutatua tatizo hilo.Na uongozi wa chuo ulipotaka kuwasimamisha masomo baadhi ya wanafunzi kwa kushiriki katika mgomo usio halali,Mtatiro na wenzake walisaidia sana,na baadaye hakuna mwananfunzi aliyesimamisha au kufukuzwa.

Baada ya hapo kuna mtiririko wa matukio mengi ambayo yalinidhihirishia kwamba huenda Mtatiro akawa mmoja wa vijana hazina kwa Taifa letu kwa siku za usoni.Kwa waliopita UDSM katika kipindi ambacho Mtatiro alikuwa mwanafunzi,wawe maadui au marafiki,watakubaliana na mimi kwamba Mtatiro alijitolea maisha yake kwa kutetea na kusimamia haki za wanafunzi.Hata ushindi wa Deo kuwa Rais wa DARUSO,ulichangiwa kwa kiasi kikubwa sana Julius Mtatiro.

Binafsi nilikuwa natofautiana na Julius Mtatiro kwenye mambo kadhaa,lakini hilo halikunifanya kutotambua mchango mkubwa wa harakati pale UDSM.Moja kati ya mafanikio ambayo tuliyapata kutokana na harakati,ni kuifanya serikali kufuta sera mikopo ya asilimia 40,ambapo baadaye ukaanzishwa utaratibu wa madaraja,japo nao ulikuwa na kasoro kadhaa.Katika hili kuna jasho la moja kwa moja la Julius Mtatiro.

Tangu hapo namwona Julius Mtatiro kama mpiganaji,mpambanaji,jasiri,mtu ambaye yuko tayari kwa lolote hasa kwa kusimamia ukweli,mtetea haki za wanyonge na mpenda mabadiliko.Najua wapo watu watakosoa haya,lakini lazima watu wajue kwamba hakuna aliyekamilika.Ni vema kuwa na mtazamo chanya.

Kutokana na historia ya wapambanaji wengi kujiunga na vyama vya siasa baada ya masomo,nilijua wazi Mtatiro angejiunga na vyama vya siasa hasa upinzani.Lakini sikuwahi kufikiria hata siku moja kwamba Mtatiro angejiunga na Chama cha Wananchi,CUF.Nilijua angejiunga na CHADEMA,pengine kutokana na upepo na uhusiano na baadhi ya wanachadema.Nilipoona Mtatiro anajiunga na CUF na kupewa cheo nilishtuka.

Baadaye,badala ya kumshangaa Julius Mtatiro kujiunga na CUF,nikamwona ni shujaa.Wakati anajiunga na CUF hadi sasa,Chama Cha Wananchi kimedumaa na kusinyaa.Hivyo kuchagua CUF badala ya Chadema,ni ujasiri mkubwa.Maana kama angechagua Chadema,pengine ingekuwa sababu ya upepo kuliko imani.

Pamoja na kwamba kuna madai kwamba Mtatiro alijiunga na CUF kama ajira kuliko imani,bado naona uamuzi wa Mtatiro ni wa kijasiri sana,tofauti na vijana wengi wanaofuata upepo.Hata hivyo Mtatiro anatakiwa kudhibitisha kwamba hakuenda CUF kwa sababu ya ajira bali kwa sababu ya imani/itikadi.

Swali ambalo linabaki kichwani mwangu,ni Mtatiro anaamini katika nini hasa?Nimeaingalia CUF kwa muda mrefu sana.Nimesoma Katiba yao.Nimesoma sera na itikadi ya chama.Nimeangalia uongozi wa juu wa CUF ukiongozwa na Prof.Lipumba.Nikawaangalia akina Jussa,Duni,Malim Seif.Kwa mbali sana nikaona tofauti kubwa sana ya kimsimamo na kiitikadi kati ya Mtatiro na akina Jussa.Mwisho nikaziona CUF mbili,Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.Kwa upande wa Tanzania Visiwani,mizani kati ya CUF na CCM iko sawa.

Lakini kwa upande wa Tanzania Bara ambapo Mtatiro anahudumu kama Naibu Katibu Mkuu,CUF inachechemea.Na kwa bahati mbaya sana akina Malim Seif,Duni,Jussa n.k hawana mpango na Tanzania Bara.

Na hapa ndipo naona Mtatiro ana kazi ngumu zaidi kuliko hata Katibu Mkuu ambaye kwa sasa ni sehemu ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Hivyo ni kazi ya akina Mtatiro kuimarisha CUF Tanzania Bara ili kuweza kuleta siasa sa upinzani wa kweli.Kwa vyovyote itakavyokuwa,kama Mtatiro yupo CUF kwa imani/itikadi au ajira,bado kazi ya kuimarisha CUF inabaki mikononi mwake.

Binafsi naona jukumu hilo naona analiweza akiachana na tabia yake ya kutoambilika,na kuachana na siasa za kutukanana na vyama vingine vya upinzani.Mtatiro atakavyofanikiwa kujenga na kuimarisha CUFupande wa Tanzania Bara atakuwa shujaa wangu kwa mara ya pili,mara ya kwanza alikuwa shujaa wangu pale UDSM.

Hilo linawezekana kama Mtatiro ataamua kujifunza kutokana na makosa yake mwenyewe na makosa ya vyama vingne vya upinzani,n kutokuwa na haraka au tama ya kushika madaraka makubwa zaidi kwa muda mfupi kama vijana wengine.Namtakia kila la kheri Julius Mtatiro katika harakati za kuijenga na kuimaarisha CUF.

IMEANDIKWA NA BABA TUSAJIGWE (MUGO)
MAPAMBAZUIKO TANZANIA
 
K

Kipoporu

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2013
Messages
351
Likes
1
Points
33
K

Kipoporu

JF-Expert Member
Joined May 2, 2013
351 1 33

Ataachaje kufanya kazi kwa bidii ili hali ni pandikizi la MAGAMBA ndani ya CUF, na analipwa kwa hilo?
 
palalisote

palalisote

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2010
Messages
8,346
Likes
60
Points
0
palalisote

palalisote

JF-Expert Member
Joined Aug 4, 2010
8,346 60 0
anapigania ulibelali?
 
masanzu

masanzu

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2013
Messages
607
Likes
134
Points
60
masanzu

masanzu

JF-Expert Member
Joined May 6, 2013
607 134 60
Mlibelali huyo hatumtaki na inavyoonekana na wewe ni mlibelali au jamaa anakulibelali nini mbona umemsifia sana
 
H

hans79

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2011
Messages
3,802
Likes
26
Points
145
H

hans79

JF-Expert Member
Joined May 4, 2011
3,802 26 145
Serious ndo nn? Vp nawe alikupa posho alochukua toka magamba?
 
Forum statistics

Threads 1,274,221
Members 490,631
Posts 30,505,121