Laiti Mwl Nyerere angekua hai angelazimika kutoka ufafanuzi lengo la kupingania uhuru wa Afrika.

Tselm

JF-Expert Member
Oct 22, 2013
229
73
Baada ya kupitia mawazo, hisia, mitazamo mbalimbali ya watanzania katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari hususani katika kipindi hiki ambacho S.A na dunia kwa ujumla inaomboleza kifo cha Mandela, Mwl.JK Nyerere angekuwa hai angelazimika kutoa ufafanuzi lengo la TZ kupigania uhuru wa Afrika hususana South Afrika.

Wapo watazania wanaotaka fidia, hawa wana mawazo kwamba TZ ilipo sasa ni kwa sababu ya kutumia muda na rasilimali zake nyingi kwa ajili ya ukombozi wa bara la Afrika hususani S.A., wapo watanzania wanaotaka sifa tu, mfano kuingizwa kwa TZ katika historia ya ukombozi/uhuru wa S.A itakayoifanya TZ kutambulika mchango wake na vizazi vya S.A, kutajwa ktk matukio makubwa kama la hivi karibuni.

Laiti Mwl. angekuwa hai angewaambia wtz hivi "unapotoa sadaka mkono wako wa kushoto usitambue km kuna shilingi ngapi" "TZ ingepewa sifa na tambulika zaidi dunia Zima kama historia ya ukombozi wa S.A ingeelezwa na waafrika kusini wenyewe na sio TZ kupitia rais wake kama vile waafrika kusini hawajui/ hawakumbuki au unawalazimisha kutambua mchango wetu ktkmmafanikio yao.

Mwl. angelazimika kutoa ufafanuzi uhusiano wa kupata uhuru kwa Afrika na kuendelea kwa Taifa lake TZ maana wajukuu wanaona wivu nchi waliyoipigania imeendelea, sasa wanaifananisha na wakoloni ambao wamesababisha TZ kuwa masikini.

Mwl. Wajibu wtz hawa hukuwa unatafuta fidia/sifa/historia ila watanzania wote kupata hawabu mbinguni.
 
Back
Top Bottom