Laiti mke ama mumeo angeona maisha unayoishi ofisini leo ungekuwa na ndoa bado?

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,778
Kuna wanaume kwa wanawake wengi walio kwenye ndoa wanavyoishi maofisini laiti wenza wao wangekuwa karibu nahisi asilimia nyingi wangekuwa juu ya kitanzi cha ndoa.

Kuna watu maofisini wake kwa waume za watu wanaitana sweetbaby, honey na mbaya zaidi kuna ambao wanashikana shikana kama hawajaolewa ama kuoa na wengine lunch time huamua kujifungia ndani ya ofisi kabisa eti wanapiga story ghafla mazungumzo yanakatika kunaashiria ishara ya ukimya, kama una shida ya dharura utapiga hodi mpaka basi..

Baada ya lunch time unashangaa wanatoka kwa kuagana ati ulikuwa wapi wewe, kilichofanyika mnajua.

Wanandoa embu jiulizeni sasa mnavyojiachia ovyo jamani wakati wewe mke wa mtu ama mume wa mtu unamwita mfagiaji king'ast na mchana mnajifungia ofisini, hizo ofisi kweli ama lah..... Mi nahisi lile saa limoja la lunch linachangia sana kuambukiza UKIMWI kwenye familia. Kumbuka muda huo ni ngumu sana kukumbuka condom ofisini.

Narudia naomba kama umeamua kuoa ama kuolewa jiheshmu, ishi kama uko na mkeo ama mumeo ofisini achana na vijisecretary vinajifanya kukuita bosii bossii waambie bosi mama zao.

Mungu awasaidie kuishi maisha matakatifu na kulinda ndoa zenu hasa kipindi hiki kigumu gonjwa la kunyonyana ndimi limeingia na unakufa kwa kubadilika rangi..

Mungu aturehemu sana, atupe uoga.
 
pdidy umeongea la maana haswaaa..ila swali la kujiuliza kwa nini hiyo hali inaongezeka??? mi nadhani upendo kwa wanaondoa haupo tena ,hizo honey,switii,mpnz wakirudi home hawaitwi , zile attention hazipo, mke asifiwi akipendeza, mume asifiwi, ni vitu vidogo ktk ndoa lakini vina chachu yake , but akiingia ofisini unaambiwa umependeza,handbag yako nzuri, mara hilo shati na tai leo umetokea! no loving msg wala simu kutwa nzima kati mke na mume, matokeo yake watu wanatafuta faraja au hizo attention huko ofisini!! kwa upande mwingine hizo situation zinalinda ndoa za watu coz watu wanarelease tension zao za nyumbani na wanakuwa more relaxed kazini.,ingawa kwa upande mwingine tutakufa sana na ukimwi kama wanandoa hawajirekebishi.
 
Mbona mie nina sweet wangu ofisini ila hatujifungii, nafikiri ni watu na watu, utani maofisini unafanya kazi inakuwa rahisi sana
ni kawaida sana, ila tu kama watu wataamua kwenda mbali na huo utani, na kumbuka watanianao huwa hawana interest ya mapenzi
unaemtamani au kumpenda huwa unakuwa nae mbali, au kuona aibu kuongea mbele yake
 
Duuh kumbe ndivo ilivo? Mie wife haniiti cwty, hny anamwita bosi wake? Anaacha kazi kuanzia kesho.
 
Mbona mie nina sweet wangu ofisini ila hatujifungii, nafikiri ni watu na watu, utani maofisini unafanya kazi inakuwa rahisi sana
ni kawaida sana, ila tu kama watu wataamua kwenda mbali na huo utani, na kumbuka watanianao huwa hawana interest ya mapenzi
unaemtamani au kumpenda huwa unakuwa nae mbali, au kuona aibu kuongea mbele yake
Soulmate.......... Am watching!
 
Mda mfupi ila bado sijaona hiyo unayosema, labda kwa vile mavioo tupu
 
Kweli mke/mume unapete kidoleni unambusu mfanyakazi mwenzako Mdomoni!(nimeshuhudia) hiyo ndo salamu.
 
pdidy umeongea la maana haswaaa..ila swali la kujiuliza kwa nini hiyo hali inaongezeka??? Mi nadhani upendo kwa wanaondoa haupo tena ,hizo honey,switii,mpnz wakirudi home hawaitwi , zile attention hazipo, mke asifiwi akipendeza, mume asifiwi, ni vitu vidogo ktk ndoa lakini vina chachu yake , but akiingia ofisini unaambiwa umependeza,handbag yako nzuri, mara hilo shati na tai leo umetokea! No loving msg wala simu kutwa nzima kati mke na mume, matokeo yake watu wanatafuta faraja au hizo attention huko ofisini!! Kwa upande mwingine hizo situation zinalinda ndoa za watu coz watu wanarelease tension zao za nyumbani na wanakuwa more relaxed kazini.,ingawa kwa upande mwingine tutakufa sana na ukimwi kama wanandoa hawajirekebishi.

nasoma mawazo yako natoa machozi inauma sana sana na hii ni mbaya zaidi pale mtu anapoondoka bila amani nyumban akihisi akifanya hivi ofisini anasahau yale matatizo kumbe wapi akirudi yako vile vile maombi ndio jibu la kuishi na kumheshimu mwenza wako
 
hapa nnapo fanya mimi hayo yapo lakini hilo lakujifungia sijaona na wala halipo, hata kushikana shikana hatujafikia hatua hiyo, tunaishi kama marafiki wa karibu au family, kuitana mpenzi, sweety, honey, wife ni kawaida, lakini wenye mali wasijue.
 
Kwani hamkuona mauno ya wamama aliyokatiwa Jairo aliporejea ofisini? Kuna usalama pale.
 
kweli mke/mume unapete kidoleni unambusu mfanyakazi mwenzako mdomoni!(nimeshuhudia) hiyo ndo salamu.

kwetu kuna kamama kana ako kamchezo tena bosi na kadreva wake ati ukiuliza watu wanadai watani msiwaguse loh huku na pete zao
 
kusema kweli ofisini kunaokoa jahazi sana, unaweza ukawa umekasirika sana hadi
unatamani kukuche uende ofisini, ukifika tu mautani, unacheka mpak jioni ushasahau
machungu...utani ofisini ni kawida sana,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom