Laiti kama kweli Mungu hayupo... Nini itakuwa hatma ya viumbe wanyonge?

when humans began living in larger groups, they may have created gods as a means of enforcing morality. In small groups, morality can be enforced by social forces such as gossip or reputation. However, it is much harder to enforce morality using social forces in much larger groups. Matt Rossano indicates that by including ever-watchful gods and spirits, humans discovered an effective strategy for restraining selfishness and building more cooperative groups.

..makes sense to me lakini haibadili nachoamini.
Bosi Michembe Huu ni mfano wa "coginitive dissonance" at work.

Mtu anapewa explanation ya "the invention of god" anakubali ina make sense, lakini hataki kubadili maoni yake kuhusu imani kwa mungu.

Kwa sababu imani imekuwa kama ushabiki wa Simba/Yanga. Hata timu yako ikifungwa kwa sababu haina uwezo hubadili timu. Utatoa kisingizioa chochote tu.
 
Last edited by a moderator:
Kuthibitisha ni ngumu kwasababu ya viwango vyetu vya imani na uelewa, utamthibishia vipi mtoto wa darasa la kwanza kuwa 'sum of exterior angles of a polygon is 360'?
Ataelewa?
Uthibitisho wangu utakuwa kiimani zaidi tatizo litaanzia hapo

Na kwa nini the sum of exterieor angles of a polygon iwe 360' na sio 361' au pungufu ya 360'?
 
Na miongoni mwa watu wapo wanaobishana juu ya Mwenyezi Mungu bila ya ilimu, na wanamfuata kila shetani aliye asi. 22:3

Enyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka ya kufufuliwa basi kwa hakika sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na manii, kisha kutokana na kipande cha damu iliyoganda, kisha kutokana na kipande cha nyama chenye umbo na kisichokuwa na umbo,ili tukubainishieni.

Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi "TUNACHOKITAKA" mpaka muda uliowekwa,kisha tunakutoeni kwa hali ya mtoto mchanga,kisha mfikie kutimia akili.

Na wapo katika nyinyi wanaokufa,na wapo katika nyinyi wanaorudishwa kwenye umri wa unyonge kabisa, hata mtu awe hajui kitu baada ya kuwa anakijuwa.

Na unaiona ardhi imetulia kimya lakini tunapoyateremsha maji juu yake, usisimka na kututumuka, na kumea kila namna ya mimea mizuri. 22:5 al- karim

Siku zote unapolisikia jambo usiangalie lile jambo latoka wapi au nani kalisema. Bali angalia uzito wa lile jambo. Mwenyezi Mungu hufanya atakalo ili kuuonyesha uwezo wake. Wewe usiyetaka lichomozeshe jua kutoka Magharibi kuelekea mashariki.

Sio tu hujajibu swali.

Hujafanya hata jitihada za kuanza kujibu.
 
mimi mKristo naamini(Imani) Mungu yupo, jibu la swali lako ni uwepo wa shetani.

Shetani katokeaje? Uwezekano wa ulimwengu kuwa na shetani kauumba nani? Mungu aliyeumba vyote na kuona vyote mwanzo mpaka mwisho alishindwa kumzuia shetani?

Kama kila kitu kilianza kwa mungu, shetani naye kaanza kwa mungu, kama shetani kaharibu ulimwengu wa mungu, na mungu kamruhusu shetani kuwepo na kuharibu, utamlaumu vipi shetani wakati mungu alikuwa na uwezo wa kuzuia na hakuzuia?


Maovu yalikuja baada ya uumbaji, binadamu ameumbwa na amepewa utashi.

Siulizi maovu yamekuja lini. Nauliza pale mungu alipokuwa naumba ulimwengu, anaweka initial parameters, kwamba ndege waweze kupaa angani kwa mbawa zao, binadamu wasiweze kupaa bila msaada wa teknolojia, lilipokuja suala la "uovu uwezekane au usiwezekane", kwa nini alichagua uwezekane badala ya kuchagua usiwezekane?

Unaelezeaje watu wanaokuwa na itikadi tofauti za kisiasa? Vipi ambao wanatambua haki za mashoga na wanaopinga hayo mambo?

What is the point of this question? Unataka kulinganisha watu wasio na uwezo wa vyote na mungu mwenye uwezo wa vyote?

Maovu yote yanatokana na sisi wenyewe binadamu.

Hakuna kinachotokea duniani bila ya ruhusa ya mungu.Kwa nini mungu karuhusu maovu kutokea?



kwanini za kibinadamu ziwe ndogo kubwa ni zipi?

Kwa mujibu wa wanaoamini mungu kubwa ni za mungu. Lakini tukiangalia tunaona mungu ana morality ndogo kuliko binadamu.

Daktari akiwa na uwezo wa kuzuia mama asizae mtoto mwenye kilema, tunamtegemea azuie. Kwa nini mungu anaruhusu watoto wazaliwe na vilema?
Umetumia neno kibinadamu na inabaki hivyo kwamba kwa akili zetu ni ngumu kuelewa ufanyaji kazi wa Mungu.

"Deus ex machina". Kwa nini mungu atuumbe na akili ndogo zisizoweza kumuelewa halafu tusipomuelewa na kuhoji uwepo wake tuambiwe tunakufuru na atatupeleka motoni?

Unaweza kumkataza mwanao kwenda shule kusoma calculus, halafu kumpa mtihani wa calculus, kisha akishindwa utake kumhukumu? Kwamba wanadamu ahtuwezi kumuelewa mungu (kama yupo) ni kosa la nani hapa?

Kwasababu tunaamini basi siku zote kwa lolote linalotokea mwisho wa siku ukuu wa Mungu utajidhihirisha

Kuamini hakuhitaji maswali, unaweza kuamini chochote, hata ukisema unaamini jiwe ni mungu ni sawa tu.

Kinachohojiwa hapa ni kujua.

Wewe unajua kwamba kuna mungu?

Unajua tofauti ya kuamini na kujua?
 
upepo hauonekani lakini ni kitu unachoweza kuhisi na kusikia ila uwepo wa mungu ni jambo la kufikirika zaidi

MBWA WA MANZESE, hii kauli yako hapa inatosha kuthibitisha kuwa Mungu yupo. Soma uliyoyaandika. Soma kwa mara ya pili. Je ipad, pc, au simu ya mchina unayotumia kuandika na kuweza kupachika bandiko lako hapa JF zimejitengeneza kwa kubati bahati tu(coincidences) tu? Au zimeundwa/ zimetengenezwa?

Sasa soma uliyoyaandika kwa mara ya tatu.Baadae Jiulize swali hili upepo ,ambao inaonekana unakubali upo, na mfumo mzima wa dunia/ulimwengu , jua, mwezi, na sayari zake, bahari,maji, anga,mimea na watu vinawezaje kujitengeneza wenyewe? Kiwanda cha Coca cola tu ni lazima kijengwe/kiundwe.!

Kama kweli una hisia za kuhisi upepo kwa nini usiwe na hisia za kuona, kuhisi, kuonja mpangilio na mwenendo wa ulimwengu na vilivyomo ndani yake? Kama huna hisia hizo ,hata tafakuri huna?

Jicho lako, kama una macho, unaelewa mpangilio wake, lilivyoumbika? Moyo wako unafahamu ulivyoumbika na unavyofanya kazi? Mfumo wa damu unavyofanyakazi katika mwili wako, umeshakaa na kufikiri? Unafikiri ni mpango wa kubahatisha bahatisha tu?

Akitokea mtu akikwambia MBWA WA....eee, hii suti na tai unaiona hii? Imejileta, imejitengeneza wenyewe tu, haina mshoni, wala designer...Mtu huyo utamuonaje? Utamwitaje?

Hivi unataka Mungu afanane na nani? Au nini?
Leta maana yako ya "Mungu"?
Unavyofahamu wewe, "Mungu" ni nini au nani?
 
Sio tu hujajibu swali.

Hujafanya hata jitihada za kuanza kujibu.

Nimejaribu kukupa mifano ili nione akili yako unaishughulishaje katika kuunganisha baina ya hili na lile, lakini nimeona bado katika uwelewa ni sifuri. Lakini kidogo kidogo utaelewa bibie.

Hayo yote unayoyahoji ni katika dalili ya kuonyesha uwepo wa Mwenyezi Mungu. Mungu anaumba apendavyo yeye na wala si upendavyo wewe. That's why wewe akakuumba kuwa mwanamke. Kwa nini usilalame kuwa mwanamke na badala yake unahoji kwa nini Mungu kaumba walemavu? Unadhani kuwa ulemavu ni makosa ya uumbaji? Kama ni hivyo basi huenda na wewe umekosewa kuumbwa badala yake ulistahili uwe mnyama au kiumbe chengine chochote kisichokuwa katika umbo hilo ulilonalo.
 
Nimezaliwa katika familia ya maaskofu na wachungaji, waliosoma theolojia.Sio wa vichochoroni. Nyumbani walikuwa wakipishana watu wa nasaba za kiaskofu na kardinali. Sio tu wanachambua biblia, bali pia the etymology of the original greek.

Nimeanza kubisha uwepo wa mungu takriban miaka 18 iliyopita.Chimbuko lake ni kusoma falsafa ya dini. Kuanzia na kitabu cha "Philosophy of Religion: An Anthology". Kuna mdau Al-Watan kakiweka sehemu hapa JF.

Tangu nipate kuanza kubisha sijawahi kupata majaribu ya maana kwa sababu kila nikifikiria nakuwa na maswali haya ya logic ambayo sijapata majibu.

Ukitaka kujua kwamba inawezekama kwa binadamu kuendelea kubisha uwepo wa mungu hata kwenye matatizo kasome historia ya Primo Levi. Myahudi aliyekamatwa na NAZI na kuwekwa kwenye concentration camp akisubiri kuwekwa kwenye gas chambers auawe. Hakupata sababu kuacha kubisha habari ya uwepo wa mungu hata alipokuwa anasubiri kuuawa.

Ningependa kujua kwamba mungu yupo na ana uwezo wote. Hili lingemaanisha ultimate responsibility ni yake
Lakini kwa bahati mbaya hakuna ushahidi kwamba tuna bahati hiyo.

Tumebaki kujifariji kama yule mtoto yatima anayesema baba yake mfalme.
nashukuru kwa majibu yako,..binafsi naheshimu watu wote,waaminio na wasioamini uwepo wa Mungu maana wana sababu zao either za msingi ama zisizo za msingi za kufanya hivyo....
 
Hatma ya viumbe hawa wasiotendewa haki na sheria wala binadamu nini? nadhani swali hili la msingi, kuhusu uwepo au kutokuwepo kwa Mungu majibu hayawezi kupatikana iwapo kanuni za kutafuta majibu zinatofautiana upande mmoja unatumia logic upande mwingine imani hapo majibu kazi ngumu Labda Tuanze kujenga Imani kwa pande zote ili tukubaliane na jinsi ya kujua uwepo wa Mungu. nimesoma biblia tangu mwanzo ilitumika Imani zaidi kuliko logic katika kujua uwepo wa Mungu sasa Kiranga ataelewa somo hili la imani???
 
Last edited by a moderator:
Bosi Michembe Huu ni mfano wa "coginitive dissonance" at work.

Mtu anapewa explanation ya "the invention of god" anakubali ina make sense, lakini hataki kubadili maoni yake kuhusu imani kwa mungu.

Kwa sababu imani imekuwa kama ushabiki wa Simba/Yanga. Hata timu yako ikifungwa kwa sababu haina uwezo hubadili timu. Utatoa kisingizioa chochote tu.

Kuelewa kwanini mtu anasema maji ni meupe haikufanyi kukubaliana nae kwamba maji kweli ni meupe
 
Hatma ya viumbe hawa wasiotendewa haki na sheria wala binadamu nini? nadhani swali hili la msingi, kuhusu uwepo au kutokuwepo kwa Mungu majibu hayawezi kupatikana iwapo kanuni za kutafuta majibu zinatofautiana upande mmoja unatumia logic upande mwingine imani hapo majibu kazi ngumu Labda Tuanze kujenga Imani kwa pande zote ili tukubaliane na jinsi ya kujua uwepo wa Mungu. nimesoma biblia tangu mwanzo ilitumika Imani zaidi kuliko logic katika kujua uwepo wa Mungu sasa Kiranga ataelewa somo hili la imani???

kwa nn na nyinyi msianze kujifunza somo la logic alafu ndio tueleweshane?
 
Nimejaribu kukupa mifano ili nione akili yako unaishughulishaje katika kuunganisha baina ya hili na lile, lakini nimeona bado katika uwelewa ni sifuri. Lakini kidogo kidogo utaelewa bibie.

Hayo yote unayoyahoji ni katika dalili ya kuonyesha uwepo wa Mwenyezi Mungu. Mungu anaumba apendavyo yeye na wala si upendavyo wewe. That's why wewe akakuumba kuwa mwanamke. Kwa nini usilalame kuwa mwanamke na badala yake unahoji kwa nini Mungu kaumba walemavu? Unadhani kuwa ulemavu ni makosa ya uumbaji? Kama ni hivyo basi huenda na wewe umekosewa kuumbwa badala yake ulistahili uwe mnyama au kiumbe chengine chochote kisichokuwa katika umbo hilo ulilonalo.

Kuzaliwa na matatizo au ulemavu chanzo chake nini?
 
biblia is the most controversal book u can read, wakat cain amefukuzwa na mungu kwa kumuua abel alikua akimsihi kua anaogopa kule anakoenda wasije kumuua... swali alikua anamuogopa nani kama dunia ilikua haina watu? na huo mji alioenda bibilia inasema alipata na mke je huyo mke alitoka wapi? it seems apart from bustan ya eden kulikua na mji mwingine upande huo!!!
 
Hii inaitwa "Deus ex machina".

Inapokuwa vigumu kumuelezea mungu au kukielezea kitu, kwa sababu ni utunzi wa zamani uliojaa contradictions , unasema tu "mungu haelezeki" au "hiki hakieleweki kwa akili ua kibinadamu".

Wewe umejuaje hilo? Kwa akili gani?

Kiranga, unakuwaga na tendency ya ku-overlook vitu vidogo sana ambavyo huviwezi halafu unarukia vikubwa sana na complicated wakati hata vidogo huviwezi. Hapo ulipo wewe hujui kama ni kilema au si kilema, hukuwa na uwezo wa kuamua/kujua uzaliwe, hukuwa na uwezo wa kuamua/kujua uzaliwe na na baba yupi na mama yupi, hukuwa na uwezo wa kuamua uzaliwe wapi, kabila gani, rangi gani, ....., na bado huna uwezo wa kuamua usife (you are by all means mortal and can't avoid it), na zaidi huna uwezo wa kujua/kuamua ufe lini. Mbali na hivyo hapo uliopo wewe ni kiumbe mwenye mwili ambao uko nao miaka yote hiyo tangu uzaliwe lakini hata hujui nini exactly kinaendelea ndani ya system ya mwili wako, ukiugua lazima ukamuona daktari akutibu (siyo akuponyershe). Halafu mimi ninavyojua wewe upo pasipokuwa na ridhaa ya wewe kuwepo, upo tu na unasubiria kutokuwepo baadaye pasipo maamuzi yako, ...., list ya mambo ni ndefu mno. Sasa haya yote ndugu yangu yako BEYOND YOUR UNDERSTANDING, do not you think you are being unfair and unreasobaly a poor reasonig person kama utalazimisha ya Mungu yote uyajue wakati hata haya ya kwako uliyonayo siku zote miaka 50 au 60 tangu umezaliwa huyajui? Hii ni simple logic tu ya kibinadamu, ambayo anaweza akawa nayo hata mtoto mdogo. Mind you, IN THE SPRITUAL REALM ESPECIALLY WHERE GOD IS IN FULL OPERATION, NOT ALWAYS ARE LOGICAL THINGS TRUE (AND VICEVERSA), AND NOT ALWAYS ARE ILLOGICAL THINGS WRONG (AND VICEVERSA). However, since you do not like it that way, keep on fumbling, groping things in the dark while thinking you will get their true picture that way
 
Hatma ya viumbe hawa wasiotendewa haki na sheria wala binadamu nini? nadhani swali hili la msingi, kuhusu uwepo au kutokuwepo kwa Mungu majibu hayawezi kupatikana iwapo kanuni za kutafuta majibu zinatofautiana upande mmoja unatumia logic upande mwingine imani hapo majibu kazi ngumu Labda Tuanze kujenga Imani kwa pande zote ili tukubaliane na jinsi ya kujua uwepo wa Mungu. nimesoma biblia tangu mwanzo ilitumika Imani zaidi kuliko logic katika kujua uwepo wa Mungu sasa Kiranga ataelewa somo hili la imani???

Hapo ulipoandika kwa kutumia keyboard ni logic system tayari.

Kama unataka kutumia imani, fumba macho halafu upapase keyboard tu kwa kuamini kwamba mawazo yako yataanikika kama unavyotaka.

Halafu uone matokeo.
 
najua ayo yoote, ila tatzo ni kuwa yote uliyoeleza ni baada ya kuamini kuwa Mungu yupo, ila hapa mada inahusu uwepo wa Mungu, yakishakuwapo makubaliano ya uwepo huo ndo unaweza kuleta QUOTES ZA IYO BIBLIA. aS FAR AS BIBLIA IMEANDIKWA NA WANADAMU, basi inaweza leta mashaka maana hoa walioandika hawasemi nani na wapi walipewa ayo maagizo...ivi tangu usome biblia ni wapi kumeandikwa insturction kuwa watu flani waandike maandiko ayo ndo yatakuwa infinity, ni wapi?alaf ni wapi kumeandikwa Q'uran ndo dira ya dunia? unawaambiaje wale watu walioishi zaidi ya miaka milion mbili kabla ya Kristo?yaan kuanzia walioishi 5 B.C? kwa wale walioishi kuanzia 0 years yaani A.D i.e ANNUAL DOMINI or in the year of the Lord, watakuwa na msimamo wa kristo ila je walioishi kabla?miaka 622 later ndo Mtume Mohammad akaanza utabiri, akafanya Hijja uko Medina akitokea Makka, je kabla ya safari yake waislam waliishi na imani gani?je walikuwepo waislam? ebu nieleweshe in those lines my brethren.

Dedicatin: sikiliza nyimbo ya...DINI TUMELETEWA BY aFANDE Sele. Thanks.
Kabla huja-querry kuwepo au kutokuwepo, unatakiwa ujiulize na upate majibu ya maswali haya ya msingi kwanza. Je, wewe upo au haupo? Na kama upo, ni nani/nini kilichosababisha wewe uwepo? Na kama haupo, kwa nini unadhani hivyo (na kama una"dhani kuwa haupo", huoni kuwa kitendo hicho cha kudhani kuwa haupo, tayari kinakufanya uwepo?). Ukishayajibu maswali haya, ambayo yanakuhusu wewe mwenyewe namna unavyojielewa, it's when unaweza ukapata sasa na hiyo legacy ya kuhamia kwa wengine na kujadili hilo swala ambalo unataka majibu yake!
 
Na kwa nini the sum of exterieor angles of a polygon iwe 360' na sio 361' au pungufu ya 360'?

hahaaa.. will the next question be "kwanini mtoto azaliwe kilema"?

Kama ndivyo yote yanajibika kisayansi na yakijibika kisayansi hata kiimani yanajibika.
 
Huyu kiranga ni wakala wa shetani amesoma urusi musimsikilize wala musisome poste zake ataupotosha umati,yeye eti anataka mungu azuie maasi ?na hali ya kuwa amemuumba binaadamu na akili atumie akili yake vizuri bila kumwaga damu,kufanya dhuluma na uadui nk bali ukiitumia akili vibaya utaadhibiwa siku ya kiyama
 
Back
Top Bottom