Laiti kama kule Hai angekuwepo mwanaume kama Saidy Mwamwindi

Labda jamii imeelemika sana sasa....Daid M alikuwa jabali hakutaka ujinga wala dharau hao wachaha Hai vipi dogo amewapandia vichwani hivyo hadi wake zenu amewala ni dharau
 
Kwa ujumla dondoo nyingi kwenye uzi huu ni sahihi. Kujazia tu nitataja za ziada zifuatazo.

Dr Kleruu alikuwa Mkristu, msomi wa Kichaga mwenye PhD aliyefanywa kuwa Mkuu wa Mkoa Iringa mwezi Januari 1971 akihamishwa kutoka Mtwara. Alikuwa mpenzi wa siasa ya Ujamaa iliyokuwa ikihamasisha vijiji vya Ujamaa. Siku ya tukio ilikuwa Krismas, tarehe 25 Desemba 1971. Mwamwindi alikuwa Mwislamu ambaye siku hiyo alikuwa akilima shambani kwake kwa trekta.

Hapo shambani kulikuwa na makaburi ya wahenga wa Mwamwindi ambayo ni mojawapo ya sababu iliyomfanya Mwamwindi aendelee kulihifadhi shamba hilo. Katika majibizano, Dr Kleruu alidiriki kuyakashifu makaburi hayo, kitu ambacho kilimuudhi sana Mwamwindi na kuamua kumuulia mbali Mkuu huyo wa Mkoa.

Baadhi ya vitu vilivyojitokeza upande wa utetezi katika kesi hiyo ya mauaji ni vifuatavyo:
1. Dr Kleruu, Mchaga ambaye hakufuata 'mila' za kabila lake za kwenda 'kuhiji' nyumbani kwao wakati wa Krismas.
2. Dr Kleruu, Mkristu ambaye anachagua kufanya kazi siku ya Krismas, kuhimiza utekelezaji wa zoezi la vijiji vya Ujamaa.
3. Mkuu wa Mkoa anaendesha gari yeye mwenyewe peke yake umbali wa takriban km 40 kwenda shambani kwa Mwamwindi.
4. Dr Kleruu kukashifu makaburi ya wahenga. Wazee kadhaa wa kabila la Mwamwindi waliitwa na kuthibitisha kuthamini huko kwa makaburi.
5. Kwa kuwa Mwamwindi alikuwa Mwislamu, haikuwa ajabu kwake kuwa analima siku ya Krismas.

Baada ya kumuua, aliuweka mwili kwenye buti la gari alilokuja nalo Mkuu wa Mkoa na kuendesha hadi kituo cha Polisi mjini Iringa. Hapo akawaambia polisi waende wakachukue 'mbwa wao' kwenye buti. Mwamwindi akashikiliwa kwa uchunguzi na kesi ikaanza kusikilizwa. Ilidumu miezi kumi tu Mwamwindi akapatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia. Akahukumiwa kunyongwa na hukumu hiyo ikatekelezwa.
 
Nje kidogo. Nilikuwa nasoma kitabu Homo deus. Humo ametajwa Nyerere na sera yake ya mashamba ya ujamaa. Anasema kuwa kabla ya hiyo sera Tanzania ndiyo ilikuwa muuzaji mkubwa wa chakula katika Africa. Baada ya hiyo sera kuanza nchi ikaingiwa na njaa hadi kuwa muagiza chakula. Sera mbovu kabisa, hata China ilifeli vibaya na kuua mamilioni.
 
Nikiwa form 6 nilikuwa nasoma Gazette la rai. Rai ile ngumu ya kina salva
Nilikutana na makala iloandikwa na majid mjingwa kuhusu huyu mtu.
Nalishukuru gazet la rai
Umenikumbusha Rai ya miaka ya 90 mpaka 2005.
Rai ya Jenerali,
Kitakwete Kitabaganda,
John Rutayisingwa.
Salva Rweyemamu
Johnson Mbwambo

Chini ya uhariri wa John Bwire

Siyo mchezo aisee. haitakuja kutokea.
 
Unahimiza watu wajichukulie sheria mkononi badala ya kuripoti kwa vyombo husika, you are mentally exhausted, take a rest.
Hivi ni chombo gani cha Dola kingekusikiliza wakati ule?

Hukusikia kuwa mkuu wa Mkoa alipuuzwa hadharani, angekusikiliza nani, OCD au RPC?

Tena unaenda kumshitaki mwana wa mfalme!

Huko ni kujitafutia kifo.
 
Huwa nafuatilia tuhuma zote alizotuhumiwa Sabaya nabaki kujiuliza
What if kingetokea kidume kama Mohamed Mwamwindi kule Hai ..kingebadili historia yote ya Hai na kila kiongozi akipelekwa Hai anakuwa na adabu kabisa...
Said Abdallah Mwamwindi
 
Nje kidogo. Nilikuwa nasoma kitabu Homo deus. Humo ametajwa Nyerere na sera yake ya mashamba ya ujamaa. Anasema kuwa kabla ya hiyo sera Tanzania ndiyo ilikuwa muuzaji mkubwa wa chakula katika Africa. Baada ya hiyo sera kuanza nchi ikaingiwa na njaa hadi kuwa muagiza chakula. Sera mbovu kabisa, hata China ilifeli vibaya na kuua mamilioni.


Ni policy iliyoleta umasikini mkubwa sana
Na baadhi ya watu walikufa
 
Basi wahehe wakisoma huu uzi vichwa vinavimba balaa...

Ila tuseme ukweli wahehe wanajielewa. Wakisema no, ni noo kweli.

Dr. Hassy Raphael Kitine msomi, waziri wa zamani, DG TISS wa zamani anawaelewa vizuri sana walichomfanya 1995. Hajarudi tena!
Walimfanya nini?
 
Back
Top Bottom