Laini zangu mbili zote zimezima

mfate42

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
3,768
4,259
Wajumbe habari za jioni,.nimekuja kuomba msaada kwa wajuvi..tatizo lilizanza juzi laini yangu ya tigo ilizima ghafla,.ikawa haisomi kwenye simu..nikajua tatizo Ni simu ila nlipoiweka kwenye simu nyingine,.ikawa haisomi pia.

Sasa Leo pia laini yangu ya voda na yenyewe imezima Kama mshumaa,.ghafla haisomi kwenye simu yangu na Mpesa nlikuwa na kiasi kidogo Cha fedha..tatizo litakuwa Nini?

Laini zangu zote mbili zimezima Kama mshumaa..na sijui chanzo Ni Nini,.au kampuni za simu wameamua kunifanyia rafu kwenye hili..??
 
Mimi yangu ya tigo ilizima juzi kati tu apo nikaenda kkoo Kwenye ofisi zao waka renew mpya kwa sh 1000....adi leo sjajua tatzo lilikuwa nini Mana sinaga mchezo wa kuitoatoa
 
Du
Mimi yangu ya tigo ilizima juzi kati tu apo nikaenda kkoo Kwenye ofisi zao waka renew mpya kwa sh 1000....adi leo sjajua tatzo lilikuwa nini Mana sinaga mchezo wa kuitoatoa
Du Asante Sana kwa taarifa..mi mwenyew nimeshindwa kujua sababu kabisaa,.mwanzo nlijua imechunika..lakin sivyo
 
DuDu Asante Sana kwa taarifa..mi mwenyew nimeshindwa kujua sababu kabisaa,.mwanzo nlijua imechunika..lakin sivyo
Umezisajili kwa kitambulisho chako mwenyewe?? Kama mtu alikusajilia kwa kitambulisho chake ndio atakuwa kaenda kuzizima au zimezimwa kama ilivyoekezwa na TCRA
 
Nlitumia kitambulisho Cha mke
Mkuu hiyo ndio sababu. Huruhusiwi kutumia kitambulisho cha mtu mwingine kusajili laini. Pili mtu anapokuwa na laini zaidi ya moja, hiyo laini ya ziada hairuhusiwi kutumika kwenye simu, inatakiwa kutumika kwenye mashine kama vile GPS, Modem au machine nyingine ambayo ili ifanye kazi lazima utumie sim kadi.

Ushauri:
Tafuta kitambulisho chako na usajili laini zako
 
Du,.Asante mkuu.ngoja nifatilie namba yangu nida..mana nahisi hata hi moja ya halotel wanaweza kuizima nayo nikakosa contact zang muhim..
 
Back
Top Bottom