Laini yangu ya Tigo baada ya kuisajili kwa biometric imekuwa na maajabu!

Usingeweza kusajili namba ya mtu labda hiyo line uwe nayo hapohapo wakati unasajili maana kuna code zitatumwa kwenye namba husika ndipo iruhusu zoezi la usajili kuendelea na kukamilika

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
Soma uelewe nilichoandika mbona unawahi kufika kileleni.
 
Usingeweza kusajili namba ya mtu labda hiyo line uwe nayo hapohapo wakati unasajili maana kuna code zitatumwa kwenye namba husika ndipo iruhusu zoezi la usajili kuendelea na kukamilika

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
Kuna watu wanaleta stori za kwenye vijiwe vya kahawa
 
Unapotaja namba unayotaka kusajili lazima kuna namna ya ku verify kwamba namba inayosajiliwa ni ya wewe uliyepo pale. Zaid ya hapo kulikuwa na uhuni tu.
Nilikwambia unaelekea kujua kusoma hilo sina shaka umefanikiwa ila kuelewa ulichosoma bado ni tatizo kwako.
 
Soma uelewe nilichoandika mbona unawahi kufika kileleni.
mkuu nakataa huwezi kusajili namba isiyokuwa yako labda hiyo line uwe nayo maana kuna security code lazima zitumwe kwenye namba husika . Kwa hiyo ulichokisema hapo Juu siyo kweli ni Upotoshaji tu

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
 
Usingeweza kusajili namba ya mtu labda hiyo line uwe nayo hapohapo wakati unasajili maana kuna code zitatumwa kwenye namba husika ndipo iruhusu zoezi la usajili kuendelea na kukamilika

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
Binafsi nimesajili Voda na Halotel. Sikuulizwa hata kama ipo hewani.
Nimewatajia no yangu. Nikawapa kitambulisho. Kwisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu habari za mchana

Mimi ni miongoni mwa watu ambao tulijitokeza mwanzo mwanzo tu wakati wa kuanza zoezi la usajili wa alama za vidole.

Baada ya kukamilisha laini hiyo nikapata sms ya uthibitisho kuwa nimeshakuwa registered.

Lakini Cha ajabu kuanzia wiki iliyopita laini yangu imeanza kunionyesha maajabu makubwa

Mfano mtu akinitumia pesa kwenye tigo pesa yangu Kuna wakati linatokea jina langu na Kuna wakati linatokea jina la mwingine

Yani
Badala litokee jina langu nililosajilia MKUSHI MBISHI

Linatokea jina EFRAIM OLOMI

Hii inaniletea shida Sana kwenye Kaz zangu maana mwingine anashangaa mbona unanipa majina tofauti nabaki na nikijaribu kuhakikisha Ni kweli

Nikiwapigia huduma kwa wateja wananiambia sijasajili kwa alama za vidole na Hilo tatizo la majina hawalijui mpk niende ofsn kwao nami nipo mbali siwezi kufika huko kwa Sasa

Sasa najiuliza
1.mbona nimesajili kwa alama za vidole lakni tigo wanakataa?

2.mbona majina ya hii namba yanakuja ya mtu mwingine na Kuna wakati yanakuja yangu,Yani laini moja ina majina mawili.(imekaaje)

Nikajaribu kuipiga namba yangu hiyo kwa true caller inaleta jina la jamaa huyo EFRAIM OLOMI na picha yake

Sasa mnisaidie maana nahisi Kuna uhuni umefanyika hapa.



Sent using Jamii Forums mobile app
Sio ww pekee yako mm nikibonyeza *106# majina yanakuja mawil tofaut

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu nakataa huwezi kusajili namba isiyokuwa yako labda hiyo line uwe nayo maana kuna security code lazima zitumwe kwenye namba husika . Kwa hiyo ulichokisema hapo Juu siyo kweli ni Upotoshaji tu

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
Tatizo lako unajifanya unajua huku hutaki kuamini huu unaoona ni upuuzi.

Tarehe 18 mwezi huu nafanya usajili wa line yangu hadi unamalizika hizo code hazijatumwa, jana yake tarehe 17 nilijaribu usajili ukashindikana kutokana na changamoto ya mtandao.

Usinibishie kwa kile ambacho nimekiona. Line ya pili nasajili tarehe 21 hiyo siku hiyo kabla ya usajili nilitumiwa code tofauti na awali. Sitaki uamini nami sitaki kuamini unachotetea kila mmoja abaki na msimamo wake.
 
Alafu Jamaa bishi kweli hataki kurekebishwa

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
Kwa hili nitaendelea kukubishia hadi mwisho. "Kama hujawahi kushuhudia uchawi au kitendo cha uchawi siyo sababu ya kuwaambia watu kuwa uchawi haupo"
 
Si wanasema hujasajilli, basi kasajili upya na uhuni wote uliofanyika nyuma utaondolewa kwenye system.
 
Nimesajili wakatuma hizo OTP na EKY wala sijapata kubonyeza *106# nione japo mara moja usajili kukamilika..
Naambulia "Namba yako xxx haijasajiliwa kwa alama za vidole" sijui shida ni nini?
 
Kweli watu tunatofautiana matatizo Mimi tangu nijisajiri kawa alama za vidole kila siku napata salio LA kuongea elfu 2 sijui inatoka wapi ni zaidi ya wiki sasa...
 
Binafsi nimesajili Voda na Halotel. Sikuulizwa hata kama ipo hewani.
Nimewatajia no yangu. Nikawapa kitambulisho. Kwisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
mi Nina laini mbili za voda usajili wa awali nikimanisha bila alama za vidole moja nilisajili kwa jina la mamangu na nyingine kwa jina langu kamili, sasa wakati nakamilisha usajili kwa alama za vidole laini yenye langu ilikubali bila shida ila yenye jina la mama ilikataa na msajili akanielewesha ili usajili ukamalike lazima usajili wa mwanzo angalau majina mawili yaendane na majina ya kitambulisho cha nida. Tofauti na hivyo akanambia laini niliyotumia jina la mama nihakikishe haidaiwi na pia isiwe na hela kabisa ndo naweza kukamilisha usajili kwa jina langu tena kwa kununua laini mpya sio hiyo sasa, ila kuna njemba humu mbishi analazimisha eti unaweza kusajili laini Mtu mwingine.
 
Ww umeambiwa nenda nenda ofsini unaanza kulalamika. unalalamika nini sasa?
Watanzania tupunguze kulalamika lalamika ovyo

Huo mfumo nao una error kama ilivyo mifumo mingine ikitokea case kma yako nenda rekebishiwa uenndelee na mishe zako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usingeweza kusajili namba ya mtu labda hiyo line uwe nayo hapohapo wakati unasajili maana kuna code zitatumwa kwenye namba husika ndipo iruhusu zoezi la usajili kuendelea na kukamilika

Sent from my SM-J700H using Tapatalk
Haya yote niliyapata wakati nasajili code nikampa wakala akakamilisha kazi yake.sasa hiz tafrani zingine ndio sizielewi zimekujaje...halafu sometimes nawaza au nimfuate Yule dada maana wamejipanga na miavuli yao town naweza nikampata akawa wa kwanza kunieleza ama nikamkosa pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo wabongo mmezoeya kuzungushwa sana bila sababu, ndio maana mkirahisishiwa mambo mnaona kama maajabu, iko hivi yaani namba yako isipoendana jina na kitambulisho cha nida automatically system inaukataa usajili so hata ukikosea namba moja usajili hauwezi kukamilika mana majina yatachengana
Sasa mimi kitambulisho Ni changu na laini pia yangu Mimi MKUSHI MBISHI.huko kuendana unamaanisha Nini?

Ama unamaanisha nimepewa namba aliyosajiliwa MTU mwingine?yani hata sielewi...!!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom