Laini moja ya simu inawezekana kumilikiwa na zaidi ya mtu mmoja na kuwa hewani?

man dunga

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
3,179
5,514
Mara kadhaa kaka akinipigia ananiambia mbona namba yako kuna mtu huwa anapokea.Basi nikawa napuuzia kuwa labda huwa anakosea. Ni line ambayo ina zaidi ya miaka 8 na nimesajili kwa kutumia kitambulisho cha NIDA.

Basi juzi juzi jamaa mwingine ananiambia mbona namba yako kuna mtu mwingine anapokea ikipigwa.Ikabidi nianze kufuatilia.Nikaipiga namba yangu kutumia simu hiyo hiyo ilimo line ila kwa kutumia mtandao mwingine. Duuh jamaa akapokea na nikamsalimia na kukata simu.

Ikabidi niwapigie wenye mtandao na kuwaelewesha lakini wananijibu kwamba inawezekana nime forward call lakini mimi nikiangalia kwenye setting forward call ziko disabled.

Je, waungwana nifanyeje maana ina onekana kabisa line moja inamilikiwa na watu wawili?
 
Haiwezekani kabisa kuna shida ya kimtandao mahali..mimi pia nina shida na line yangu nikiwa offline tu ukinipigia unaambiwa huna muda wa maongezi na voda wameshindwa kabisa kulitatua hili tatizo
Ni line ya voda vile vile pia kaka ananiambia akiipiga namba yangu anaambiwa hana salio wakati salio lipo.
 
Haiwezekani kabisa kuna shida ya kimtandao mahali..mimi pia nina shida na line yangu nikiwa offline tu ukinipigia unaambiwa huna muda wa maongezi na voda wameshindwa kabisa kulitatua hili tatizo
Mkuu, hilo tatizo maana yake ni kwamba kumewekwa divergence kwenye simu yako ambayo ni namba ya kigeni , kwamba ukiwa haupo hewani ipige kwenye namba hiyo sasa lazima imwambie anaepiga hana salio.

Mara nyingi tatizo hili hutokea kwa watu wanaonunua simu za Mtumba (used abroad) kunakuwa na namba ipo tayari by default.

Pia wakati mwingine hutokea mtu akipiga na ukiwa hupatikani inasema namba unayopiga sio sahihi , hili ni tatizo hilohilo.
 
Hivyo vitu ni vya kawaida rekebisha kwenye setting tu.
Uzuri wake ni kuwa hiyo hali inajitokeza mtu akikupigia , jiuliza kwa nini ela ikitumwa inakuja kwako badala ya kwenda kwa yule Mwingine.

kwa hiyo cheza na setting hiyo hali imewah kumtokea mtu wa karibu yangu tulipomuuliza kumbe alikuwa ni jirani Yake huko kijijini kwao
 
Achana na hao wanaokwambia nenda pm umehackiwa. Nenda customer service desk utatuliwe ishu yako.

Kuna namba ilikua inanitumia sms kuniomba hela ya shule hua ananiita Dada Tumaini. Siku hiyo nimepiga hiyo namba kapokea mshkaji akasema yeye ni mwalimu na wanafunzi hutumia simu yake kuwasiliana na wazazi au walezi wao.

Nikamuambia basi mtafute mwanafunzi mwenye dada anaitwa Tumaini mwambie huo ujumbe hua naupata mimi na siyo anayemlenga. Siku kadhaa mbele jamaa akanipigia akaniambia kashamuelezea mwanafunzi wake.
 
Ni line ya voda vile vile pia kaka ananiambia akiipiga namba yangu anaambiwa hana salio wakati salio lipo.
Kumbe hili tatizo sio mimi tuu..na adhani pia namba yangu inaingiliana na nyingine kuna mtu juzi WhatsApp kanitumia risiti za malipo na maelezo marefu akini refer mimi kama mkuu wa chuo
 
Mkuu, hilo tatizo maana yake ni kwamba kumewekwa divergence kwenye simu yako ambayo ni namba ya kigeni , kwamba ukiwa haupo hewani ipige kwenye namba hiyo sasa lazima imwambie anaepiga hana salio.

Mara nyingi tatizo hili hutokea kwa watu wanaonunua simu za Mtumba (used abroad) kunakuwa na namba ipo tayari by default ,

Pia wakati mwingine hutokea mtu akipiga na ukiwa hupatikani inasema namba unayopiga sio sahihi , hili ni tatizo hilohilo
Mimi simu yangu sio mtumba na sijawahi kuwa na simu hizo zilizotumika kabla nje au ndani ya nchi
 
Screenshot_20210309-111445.jpg
 
Hatua ya kwanza sitisha kabisa kufanya miamala ya pesa kwa kupitia hiyo line
 
Mara kadhaa kaka akinipigia ananiambia mbona namba yako kuna mtu huwa anapokea.Basi nikawa napuuzia kuwa labda huwa anakosea. Ni line ambayo ina zaidi ya miaka 8 na nimesajili kwa kutumia kitambulisho cha NIDA

Basi juzi juzi jamaa mwingine ananiambia mbona namba yako kuna mtu mwingine anapokea ikipigwa.Ikabidi nianze kufuatilia.Nikaipiga namba yangu kutumia simu hiyo hiyo ilimo line ila kwa kutumia mtandao mwingine. Duuh jamaa akapokea na nikamsalimia na kukata simu.

Ikabidi niwapigie wenye mtandao na kuwaelewesha lakini wananijibu kwamba inawezekana nime forward call lakini mimi nikiangalia kwenye setting forward call ziko disabled.

Je waungwana nifanyeje maana ina onekana kabisa line moja inamilikiwa na watu wawili .
Haiwezekani sema mda mwingine wanajisahau
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom