Nyundo Kavu
Senior Member
- Dec 6, 2011
- 186
- 85
Wadau, nimefuatilia threads mbalimbali humu jamvini tangu show mbili zilizo andaliwa na moja ya wakongwe wa muziki wa kizazi kipya hapa Bongo kupita. Ukweli ni kwamba, nashangazwa sana jinsi baadhi yetu tunavyoshindwa kukubali kwamba mmoja ya hao alimfunika mwenzie na kwa sababu tumekulia katika jamii ya ubishi basi tumeendelea kubisha na kutokubali kwamba bibie Judith Wambura Mbibo kafunika.
Kuna wanaosema eti mahadhi ya muziki ya wakongwe hawa kwenye "game" ni tofauti, sikatai lakini tukumbuke walikuwa na wanamuziki wa ladha tofauti waliowasindikiza kwa hiyo si sababu ya mmoja amzidi au aanguke kwa sababu hiyo.
Kuna mwandishi mmoja wa radio alidai eti show ya Khamis Mwinjuma ilikuwa inahitaji watu 400 tu...! mhh, hivyi inawezekana kweli!? kwa nini basi achukue ukumbi mkubwa? kwa nini walikuwa wanabembeleza wanafunzi wa IFM wanunue tiketi kwa bei ya chini ili hak\li waingie kujaza ukumbi?
Kama nilivyosema hapo juu, kwa sababu tumezaliwa kubisha hata kutokuwa na uhakika na unachobisha basi kuna watakao endelea kubisha na hili na wala si kurekebishana na kuukubali ukweli.
NB:
Kwa nini Mwana FA hakuchagua tarehe tofauti ilihali anajua mwanamuziki tena mkongwe mwenzie amechagua tarehe hizo? Alafu kuhusu Jide kumuita "Mwana Fatuma" ilifuatia Mwana FA ku-"tweet" kuwa show ya JayDee ni kama "fund-riser"...! Sasa kweli mlitegemea huyo dada akae kimya?
Mimi naona huyu ndugu yetu akubali tu pamoja na elimu aliyo nayo anahitaji ajiendeshe mwenyewe na si kuendeshwa na watu wachache watakao mtema wakishajua amechoka.
Nawakilisha....!