Lady Jaydee afanyiwa kitu mbaya

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
975
47
Na Imelda Mtema

Icon wa Muziki wa kizazi Kipya Bongo aliye Mmiliki wa Machozi Band, Judith Wambura ‘Lady Jaydee' a.k.a Binti machozi, ameuanza Mwaka 2010 kwa nuksi baada ya kufanyiwa kitu mbaya na vibaka waliomvamia usiku kisha kumpora vitu kadha wa kadha...

Tukio hilo lenye tafsiri mbaya juu ya ulinzi wa mastaa nchini, ambalo lilishuhudiwa ‘laivu' na Paparazzi wetu, lilijiri usiku wa kuamkia Jumanne, nje ya Uwanja wa Taifa wa mpira wa miguu ‘National Stadium', jijini Dar mara tu baada ya kumalizika kwa mechi kati ya timu ya Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast maarufu kama Tembo wa Afrika.

Fulu stori ilikuwa hivi, baada ya mechi, Jide aliongozana na mashabiki wengine kutoka nje ya ‘ground' ambapo bila yeye kuwa ‘aweya', vibaka hao walimuweka mtu kati na kuanza kung'ang'ania mkoba wake uliokuwa na Kompyuta ya mkononi ‘Laptop', kamera na kilongalonga chake cha kiganjani.

Katika tukio hilo, kuliibuka ‘timbwili' kubwa huku Jide akitaka kutia ngumu kuachia mkoba wake ambao pia ulikuwa na ‘dokumenti' muhimu.

Baadaye vibaka hao pamoja na ‘mtiti' wa kasheshe walioupata kutoka kwa watu waliokuwa na Jide, walifanikiwa kumtoka mali hizo.

Katika hali ya kuchanganyikiwa, Binti Machozi alionekana ‘kudata kimtindo' kutokana na kutojua aanzie wapi huku kukiwa na ‘nyomi' ya watu waliokuwa wamekusanyika nje ya uwanja huo, tayari kurejea majumbani kwao.

Baada ya ishu hiyo, Jide aliingia kwenye gari lake akiwa na wapambe wake waliokuwa wakimfariji na kuondoka kwa unyonge na haikujulikana mara moja kama alikwenda kuripoti tukio hilo polisi au laa

Source: Global Publishers website
 
Maelezo yanayoonyesha mazingira ya tukio ni kweli kwamba ulinzi haukuwepo kabisa, hivyo watu aliokuwa nao inaonyesha kwamba walikuwa ni wapambe kwa maana ya mtaani yaani marafiki, na sio kwa maana ya ulinzi.

Pole JD, usitembee na Laptop usiku tmk watu hatujala na hakieleweki kukuacha inakuwa ngumu. Pole sana.
 
Watu wengine bwana, utakwendaje uwanja wa taifa na lap top kama siyo ubishoo aaa, kwani Jaydee hajui kwamba uwanja wa taifa uko wilaya ya Temeke.

Jamani sisi wote ni wana DAR na tunayajuwa maeneo yetu, infact kwa sasa hakuna cha Masaki wala cha Upanga, wala cha Mbagala kote ni sawaaaaa tu. Vibaka wako kila sehemu.

Kuna kundi la vijana wa kiarabu na kihindi wao wanaiba wakiwa ndani ya magari yao, hutembelea nyumba zenye misiba yotee iliyoko Oyestrbay, Masaki, Upanga nk na kuvunja magari na kuiba kila watakachokuta ndani ya gari. Polisi wanalijuwa hilo ila hawajafanikiwa kuwakamata, kwani mbinu zao ni za hali ya juu sanaaaaa na huiba kwa speed isiyo ya kawaida kabisa.

Ndugu zangu watanzania ni lazima tuwe macho sana na mali zetu, pia kujuwa unakwenda sehemu gani na hutakiwi kubeba vitu gani.

Pole Jaydee ila kuwa muangalifu sana nchi na mji wetu wa DAR umebadilika sana, sana, sana, hakuna usalama.
 
Sasa uwanja wa Taifa na Laptop!Sina hakika na vitu alivyoibiwa kwani tumezoea watu wakiibiwa utawasikia nilikuwa na kompyuta,mastercourse,billwate n.k hata kama huyo aliyeibiwa anashinda njaa kwa kutokuwa na pesa!
Pole sana jide lakini ongea ukweli.
 
Pole sana inauma ku loose doc. hakuwepo mumeo awape za uso? na hukuwa na ile spray ya kina mama(mays spray) kwa ajili ya vibaka? laptop ya nini uwanjani au inarecord mpira na mavocal?
 
Maelezo yanayoonyesha mazingira ya tukio ni kweli kwamba ulinzi haukuwepo kabisa, hivyo watu aliokuwa nao inaonyesha kwamba walikuwa ni wapambe kwa maana ya mtaani yaani marafiki, na sio kwa maana ya ulinzi.

Pole JD, usitembee na Laptop usiku tmk watu hatujala na hakieleweki kukuacha inakuwa ngumu. Pole sana.

wapambe wenyewe hawa hapa http://www.ladyjaydee.blogspot.com/
 
Pole sana inauma ku loose doc. hakuwepo mumeo awape za uso? na hukuwa na ile spray ya kina mama(mays spray) kwa ajili ya vibaka? laptop ya nini uwanjani au inarecord mpira na mavocal?

Mbona yeye anaoneka ndio ananguvu kuliko huyo mumewe? kama yeye aliwashindwa mumewe angechemsha kabisa.
 
Sasa uwanja wa Taifa na Laptop!Sina hakika na vitu alivyoibiwa kwani tumezoea watu wakiibiwa utawasikia nilikuwa na kompyuta,mastercourse,billwate n.k hata kama huyo aliyeibiwa anashinda njaa kwa kutokuwa na pesa!
Pole sana jide lakini ongea ukweli.

alikuwa anawapa apdeti wanablogu wake laivu from ze stediam! hapa inabidi tumpe kahongera kwa kuwahabarisha wanablogu wake maskini ambao zey kant afodi kuingia uwanjani.
 
alikuwa anawapa apdeti wanablogu wake laivu from ze stediam! hapa inabidi tumpe kahongera kwa kuwahabarisha wanablogu wake maskini ambao zey kant afodi kuingia uwanjani.
Kama ni hivyo nampa Bigup commando jide.
 
alikuwa anawapa apdeti wanablogu wake laivu from ze stediam! hapa inabidi tumpe kahongera kwa kuwahabarisha wanablogu wake maskini ambao zey kant afodi kuingia uwanjani.

Ajifunze kutoka kwa wenzake wazoefu... uwanja wa taifa siyo sehemu ya kuingia na vitu vya thamani bila maandalizi
 
Ajifunze kutoka kwa wenzake wazoefu... uwanja wa taifa siyo sehemu ya kuingia na vitu vya thamani bila maandalizi
haka kadada kanapenda maujiko. na inawezekana mzimu wa jf umeanza kumuandama, if zis iz ze kesi inabidi aje aapolojaiz au et listi achangie japo kidola 10 ili jf tumsamehe mambo yake yawe saafi agein.
 
Duh, hiyo heading nilidhani watu 'wamekula mzigo':rolleyes:!
 
alikuwa anawapa apdeti wanablogu wake laivu from ze stediam! hapa inabidi tumpe kahongera kwa kuwahabarisha wanablogu wake maskini ambao zey kant afodi kuingia uwanjani.
Sidhani kama kuna ukweli wowote kuhusu kauli yako hii!
 
Hao walinzi walikuwa wanafanya nini?
Hana walinzi, ila ni wapambe! tena alikuwa nao wengi tu siku hiyo...cheki picha hii hapa chini..

i1512_jdwapambe.JPG

Sidhani kama kuna ukweli wowote kuhusu kauli yako hii!
nimefuatilia tena ni kweli hako kahabari kangu ni bogaz, chanzo changu cha habari kimechemsha! inabidi nifatilie tena kwanini kaenda na kalaptopu uwanjani?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom