Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 975
- 47
Na Imelda Mtema
Source: Global Publishers website
Icon wa Muziki wa kizazi Kipya Bongo aliye Mmiliki wa Machozi Band, Judith Wambura ‘Lady Jaydee' a.k.a Binti machozi, ameuanza Mwaka 2010 kwa nuksi baada ya kufanyiwa kitu mbaya na vibaka waliomvamia usiku kisha kumpora vitu kadha wa kadha...
Tukio hilo lenye tafsiri mbaya juu ya ulinzi wa mastaa nchini, ambalo lilishuhudiwa ‘laivu' na Paparazzi wetu, lilijiri usiku wa kuamkia Jumanne, nje ya Uwanja wa Taifa wa mpira wa miguu ‘National Stadium', jijini Dar mara tu baada ya kumalizika kwa mechi kati ya timu ya Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast maarufu kama Tembo wa Afrika.
Fulu stori ilikuwa hivi, baada ya mechi, Jide aliongozana na mashabiki wengine kutoka nje ya ‘ground' ambapo bila yeye kuwa ‘aweya', vibaka hao walimuweka mtu kati na kuanza kung'ang'ania mkoba wake uliokuwa na Kompyuta ya mkononi ‘Laptop', kamera na kilongalonga chake cha kiganjani.
Katika tukio hilo, kuliibuka ‘timbwili' kubwa huku Jide akitaka kutia ngumu kuachia mkoba wake ambao pia ulikuwa na ‘dokumenti' muhimu.
Baadaye vibaka hao pamoja na ‘mtiti' wa kasheshe walioupata kutoka kwa watu waliokuwa na Jide, walifanikiwa kumtoka mali hizo.
Katika hali ya kuchanganyikiwa, Binti Machozi alionekana ‘kudata kimtindo' kutokana na kutojua aanzie wapi huku kukiwa na ‘nyomi' ya watu waliokuwa wamekusanyika nje ya uwanja huo, tayari kurejea majumbani kwao.
Baada ya ishu hiyo, Jide aliingia kwenye gari lake akiwa na wapambe wake waliokuwa wakimfariji na kuondoka kwa unyonge na haikujulikana mara moja kama alikwenda kuripoti tukio hilo polisi au laa