LADY JAY DEE amtupia Ruge jiwe la gizani kufuatia kauli yake kuwa walishamalizana


Mr. Hussein Juma

Mr. Hussein Juma

Verified Member
Joined
Mar 5, 2012
Messages
717
Likes
449
Points
80
Mr. Hussein Juma

Mr. Hussein Juma

Verified Member
Joined Mar 5, 2012
717 449 80
Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, alidai kuwa vituo vyake vinaweza kuanza kucheza kazi za Lady Jaydee iwapo akiwaruhusu wafanye hivyo.

Kupitia Instagram, Lady Jaydee ameijibu ofa hiyo kwa dongo lililowaendea wasanii waliowahi kumshirikisha kwenye nyimbo zao lakini kwa kuogopa kuingia matatani na kituo hicho chenye nguvu nchini, walifuta sauti yake.

“Kwahiyo wale mlio omba collabo sijui feat baadae mkaenda kufuta chorus zangu mtafanyaje ? Habariiiiiiiiiii zenu buaaaaaana [HASHTAG]#SawaNaWao[/HASHTAG] [HASHTAG]#TofautiNaHesabuZao[/HASHTAG],” aliandika Jide.

Ruge alitoa kauli hiyo Ijumaa iliyopita kwenye mahojiano na kipindi cha XXL.

“Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige, jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tukikutana, nimuombe tena [Lady Jaydee] kama tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu,” alisema.

Ruge pia alisema ana muda mrefu hajawahi kukutana na Lady Jaydee, japo amedai ‘hata leo nikipata nafasi ya kahawa nitashukuru sana kwa huo mwaliko.’

Wiki kadhaa zilizopita Ruge na Joseph Kusaga walishinda kesi ya kuchafuliwa (defamation) iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Lady Jaydee na muimbaji huyo kuamriwa kuwaomba radhi.

“Tunashukuru walau tulishinda ile kesi lakini at least ilitengeneza mfano wa watu kuelewa kwamba tusipende kutuhumu vitu kama watu huna uhakika. Bahati nzuri pia hata katika hiyo kesi alisema mwenyewe hajawahi kusikia tunasema, aliambiwa na watu. Lakini ni mambo yashapita hayo.”
 
Mwanga Lutila

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2016
Messages
2,864
Likes
7,086
Points
280
Mwanga Lutila

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2016
2,864 7,086 280
Ukiweza kugombana na Ruge pamoja na Clouds lakini bado ukasonga mbele kimuziki basi wewe ni Commando.

Huyu dada amevuka kisingiti hicho, maana wengi wameshindwa wakipigwa biti kidogo tu wanarudi kuwalamba miguu.
 
Blank page

Blank page

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2015
Messages
4,124
Likes
2,246
Points
280
Blank page

Blank page

JF-Expert Member
Joined May 28, 2015
4,124 2,246 280
bhana,si weka stor yote apa...ach roh mbay mi nakasimu kang tecn siwez,kuingia kw blog yako.uko kw promo y blog nin?
 

Forum statistics

Threads 1,274,151
Members 490,601
Posts 30,502,798