Ladies n' Gentleman.....!!!

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,047
21,522
Kwa heshima na taadhima namleta kwenu kijana wangu Imuh Zuzu na ngoma yake ya Endelea. Ni upcoming artist bado ana safari ndefu sana, hivyo nawaomba support ngoma yake hii kwa kuisikiliza tu na kutoa maoni yako. Wapi aboreshe ili aweze fika mbali zaidi
 
Yuko vizuri na ana muonekano wa Kicomedian. Ila namshauri aongeze ubunifu, staili ileile mwishowe watu watamchoka.
 
Yupo vyema ila anahitaji kwenda shule ya muziki ili apate kujifunza wapi pa kupandisha sauti na kuendana sauti na mziki.

Lunatic
 
Kijana wako anafanana na wengi kuanzia uimbaji mpaka beat ya wimbo, sasa kuingia kwenye ngoma iliyokolea tayari, utahitaji kuwa na kitu cha kukutambulisha ili watu wakugeukie.

Hapo kati kati hapo, jamaa wa bongofleva, kila aliyetoka, alitumia signature yake kiasi kwamba ukisikia mdundo tu, unajua mmiliki, ukimuweka Mr 2, Juma Mchopanga, Soggy, Kiroboto, Balozi, Solo, Nigga J, Afande, Inspekta n.k huwezi kuchanganya hata iwaje.

Mad ice, Biziman, Mr Paul, Mr Nice, n.k

Tofauti inakuwepo.

Msukume afanye zaidi ya hapo na ikiwezekana, iwe tofauti na hii iliyopo!
 
Wasanii wa siku hizi wanatengenezwa aisee, hata kama una ngoma ya kawaida au hata mbaya, ukiwa na connection na hela kidogo imetoka hiyo mkuu.

Wasanii wangapi wana ngoma nzuri lakini haziskiki kwenye media...? Watu wana vipaji 'DEEP' lakini hawana connection wala mkwanja sio, vipaji vingi vinaishia kupotea mzee baba.

Ila kwa hiyo ngoma kwa upande back inahitaji more efforts kuweza kuwa kwenye level flani hivi.

Thanks...!
 
Kijana wako anafanana na wengi kuanzia uimbaji mpaka beat ya wimbo, sasa kuingia kwenye ngoma iliyokolea tayari, utahitaji kuwa na kitu cha kukutambulisha ili watu wakugeukie.

Hapo kati kati hapo, jamaa wa bongofleva, kila aliyetoka, alitumia signature yake kiasi kwamba ukisikia mdundo tu, unajua mmiliki, ukimuweka Mr 2, Juma Mchopanga, Soggy, Kiroboto, Balozi, Solo, Nigga J, Afande, Inspekta n.k huwezi kuchanganya hata iwaje.

Mad ice, Biziman, Mr Paul, Mr Nice, n.k

Tofauti inakuwepo.

Msukume afanye zaidi ya hapo na ikiwezekana, iwe tofauti na hii iliyopo!
Ni.ekuelewa mkuu, shukrani kwa honest opinion
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom